Usafiri wa treni Dar watimia

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Adha ya msongamano wa foleni barabarani kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam huenda ikapungua makali kuanzia mwezi ujao treni ya abiria kutoka Steshenni hadi Ubungo itakapoanza kutoa huduma.

Uzinduzi wa usafiri wa njia ya reli kutoka Stesheni hadi Ubungo ulifanywa jana na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba.

Treni hiyo yenye mabehewa sita itakuwa na uwezo wa kubeba jumla ya abiria 900. Kila behewa litakuwa na abiria 80 waliokaa na itakuwa ikifanya safari tatu asubuhi na tatu jioni.

Kwa maana hiyo, treni hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria wanaobebwa na mabasi ya Toyota Coaster 22 kwa safari moja na kusafirisha abiria 5,400 kwa siku.

Hata hivyo, nauli za usafiri huo zitajulikana baada ya kufanyika kwa kikao kati ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na usafiri huo kuanza rasmi Oktoba.

Katika uzinduzi huo, treni hiyo iliyoondoka Stesheni saa 6:00 mchana na kusimama katika vituo sita ilifika Ubungo saa 6:45, ilikuwa imebeba umati wa wakazi ambao walikuwa wakishangilia.

Wakazi hao walisikika wakiimba nyimbo za kumsifu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye aliahidi kuanzishwa kwa usafuri wa treni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupunguza msongamano barabarani.

Mmoja wa wakazi wa Buguruni, Juma Abdallah, alisema kuwa usafiri wa treni utakuwa mkombozi kwa wananchi wengi kutokana na kutumia muda mfupi.

Hata hivyo, alisema serikali itapaswa kuangalia uwezekano wa kuhakikisha kuwa nauli treni inapangwa ambayo wengi wataimudu.

Treni hiyo yenye namba TRL 6407 iliyobeba wananchi pamoja na wafanyakazi wa TRL katika mabehewa sita ilisimama katika vituo vya Kamata, Buguruni, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Tabata Relini, Mabibo na Ubungo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari hiyo, inayochukua dakika 45, Dk. Tizeba aliwataka wakazi waishio pembezoni mwa maeneo ya reli ya Stesheni na Ubungo kuondoka mara moja kabla nguvu ya serikali kutumika kuwahamisha katika maeneo hayo.

Dk. Tizeba alisema wakazi wote waliojenga umbali wa mita moja kutoka reli hiyo inapopita waondoke mara moja na kwamba hawatalipwa fidia yoyote.

“Wakati wa uzinduzi leo tumegundua kasoro kadhaa katika vituo, hivyo tunaanza kurekebisha kasoro hizo na mwezi Oktoba mwaka huu safari zitaanza,” alisema Dk. Tizeba.

Ahadi ya kuanzishwa kwa usafiri wa treni ilitolewa na serikali miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya kupunguza msongamano katika barabara za Dar es Salaam.

Hata hivyo, utekelezaji wake ulishindikana hadi baada ya Dk. Mwakyembe alipiteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Mpango wa usafiri wa treni pia unakusudia kuanzisha usafiri wa kutoka Pugu hadi katikati ya Jiji.







CHANZO: NIPASHE

 
Hebu tupiamo na mapicha basi...tuione hiyo treni yenyewe!
 
Hebu tupiamo na mapicha basi...tuione hiyo treni yenyewe!
Angalia kiambatanisho... aidha haina ubora wa HD
 

Attachments

  • dar-tren.jpg
    dar-tren.jpg
    11.6 KB · Views: 396
  • Thanks
Reactions: SMU
Mungu wangu weeee!

Hiyo migari moshi ndiyo ile ya zamani iliyokuwa inatumika kwenye reli ya kati!
 
Duh walau sasa tuna mawaziri wanaotoa ahadi na kuzitekeleza hongera sana waliofanikisha mipango yoe hadi leo tunaona treni ikijizatiti kutoa huduma za usafiri wa treni katikati ya jiji la Dar.
 
Aisee babaangu watu wa dar mtakuwa na rahaa nawaombea nauli iwe 250 kwanzia stesheni hadi mbezi mwisho,,ila nawasiwasi na wamiliki wa daladala na madereva wanaweza ngowa vyuma ya reli kukwamisha usafirishaji
 
mmmmmmmmmmmmmh mie nasubiri nione jinsi itakavyoongeza msongamano wa magari..... Ila kamradi kazuri kuna watu wataotoka kimaisha hapo......full kuchakachua mapato
 
Ndo mana walitaka kumrestisha huyu baba,kwasababu ni jembe kweli,sio bla bla vitu vinaonekana.kwakweli mwakyembe na magufuli ni mfano mzuri.
 
Back
Top Bottom