Usafiri wa Train raha tupu!

Mchokozi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
215
29
Leo kwa mara ya kwanza nimepanda City train na kwa sasa niko nyumbani nimepumzika na familia yangu mara baada ya kumaliza kazi saa 9:30, kweli usafiri wa Train ni raha kwani ingekuwa dala dala ningekuwa bado na sota kwenye foleni. Hongera sana Dr Mwakyembe kwa kusimamia mawazo na maamzi yako.
 
Unakaa wapi?

Umepanda toka wapi hadi wapi??
 
ngoja waje chadema uone matusi yao mana rohooo inawauma hapo noma ...mana wanawaza muda wote jk ashindwe kutimiza ahadi

Acha propaganda wewe kwani CDM ndio hawataki maendeleo? Nchi kwanza vyama baadae,kama ulikuwa hujui lengo la cdm ni kufufua viwanda na miradi yote iliyokuwepo enzi za mwalimu pia kubuni mpya lengo ni kutoa ajira kwa vijana na sio zile zenu za kuokota makopo mil 1......
 
Lowassa nae aje apande treni aone kazi aliyofanya Dr mwakiyembe! issue ya richmonduli imekwisha.Lowasa please njoo upande treni ya mwekyembe
 
Hongera sana Dr Mwakyembe, jitahidi na treni ya kati ianze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.
 
ngoja waje chadema uone matusi yao mana rohooo inawauma hapo noma ...mana wanawaza muda wote jk ashindwe kutimiza ahadi

Nakuheshimu sana mkuu KIBE ,napita nisijekuharibia siku mkuu, kauli hizo!!!!?
 
Last edited by a moderator:
ngoja waje chadema uone matusi yao mana rohooo inawauma hapo noma ...mana wanawaza muda wote jk ashindwe kutimiza ahadi

Kumbe JK ndo alimwambia Mwakyembe atengeneze treni ya daladala! sikujua mie
 
ngoja waje chadema uone matusi yao mana rohooo inawauma hapo noma ...mana wanawaza muda wote jk ashindwe kutimiza ahadi

Hebu tingisha kichwa chako je unasikia kuna nn? Kuna k2 kinatingishia tingishika au usikii chochote. Ukisikia k2 kinatingishika jua kumejaa maji ukiona kimya ujue kuna hewa 2

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ni hatua nzuri sana kwa mwakyembe. Hongera zake kwa kusimamia mawazo yake. Kwa hili ui-tikadi nauweka pembeni, cha msingi asimamie zaidi uboreshaji wa huduma maana wenye kuathirika na foleni ni watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kivyama.
 
ngoja waje chadema uone matusi yao mana rohooo inawauma hapo noma ...mana wanawaza muda wote jk ashindwe kutimiza ahadi

Kwa kuwa wivu ni kitu kibaya sana......Nilikuwa siamini ulichoandika lakini kwa majibu uliyoyapata wacha niamini
 
Naona Wivu sisi wa Bunju Boko na Tegeta tunatamani tungepata na sisi kwa sababu Wenye Daladala za Route hii jioni wanatupa shida sana.
wanakatisha Route na kutufungia milango Jioni.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mwakyembe amedhubutu na ameweza. Hao mawaziri wengine wanafanya nini? Chamsingi tutoe maoni ya namna ya kuboresha huduma hii ya usafiri wa treni jijini DSM.

kwa upande wngu mie nampa big up mwakiyembe,pomoja na matatizo aliyapata bado ni mzima sana na ni mbunifu mzuri.
ANGALIZO;
lengo lako ni kupnguza msongamano wa magari dsm,ila nashauri pindi ile project ya magari yanayoenda kasi ukiisha ni vizuri aone tena umuhimu wa kuamisha ubungo bus terminal kwenda eneo lingine ambalo sii karibu na mjini na hilo eneo watumie kpaki magari madogo yatokayo ubungo,kimara,mbezi,mwenge,kibangu na kwingineko wapaki magari yao hapo ubt na wakapande train kwenda mjini na ambaye atapenda kutumia barabara kwenda mjini ni lazima alipe ada fulani ambayo ni kubwa ili kila mtu alazimike kupaki gari kwa kuhofia ada,hapo kwa kiasi fulani tutapunguza foleni ktk jiji la dar.
aksante naomba kuwasilisha wakuu wa jf.
 
Back
Top Bottom