Usafiri wa PIKIPIKI upigwe marufuku

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Zibaki pikipiki za kawaida za maofisini na private . Lakini sio hizi za biashara ya kubeba watu. Hawa vijana waofanya hizi biashara bado hawaja qualify kubeba abiria na kuingia barabara kubwa na hawana heshina na barabara .na wengi wao wanavuta BANGI na kunywa VIROBA. Na kama zitaruhusiwa basi ziwe za nje ya barabara kubwa . Au ziishie huku vichochoroni.
 
usipomuelimisha usitegemee miujiza kubadilika kwani mitz ndio ya hivihivi tu..
 
yawezekana kweli wanavuta Baaaaaangili maana wakati mwingine kwenye barabara kubwa kama mandela utakuta pikipiki inaovateki gari halafu inalichomekea, unataraji nini?
 
Wakipigwa marufuku mtaani hakutakalika, maana wizi na mauaji yataongezeka............!!
 
Zamani kidogo (kabla ya mabo ya bodaboda) pikipiki ilikuwa inaheshimiwa, ukiona pikipiki (kwa vijijini) basi huyo ni bwanashamba, mratibu elimu, afisa ..., yaani watu wenye elimu zao lakini sasa zinaendeshwa na kila mtu na zinaonekana kuwa kero. Kwanza jina lenyewe la bodaboda linamaanisha hali ya kutofuata utaratibu, lilianzia huko mkoani Mara, ni usafiri unaokufikisha uendako bila kufuata njia rasmi. unapita njia za panya ilimradi kufika.
 
wewe acha upuuzi! kwa sababu ya ukimwi watu wapigwe marufuku kufanya ngono. tatizo una jump try. THINK BRO! AJIRA HIYO!
 
Amini usimiani kwa majirani wetu ajali za pikipiki nyingi mno hadi wametenga wodi maalum ya majeruhi wa bodaboda! Pikipiki zipigwe marufuku, zinatumaliza.
 
wakorofi sana hawa waendeshaji wa bodaboda, ni rahisi mno kuwapamia, hawajali sheria za barabarani wala nini, mradi wanataka waendeshe wanavyofikiria wao, ikitokea amechomeka kwa dreva ambae hajamwona au ambae gari lake break sio poa, parapanda inalia mda ule ele
 
Ni ajira na usafiri kwa watu wa hali ya chini . Lakini hata taa barabarani hawazifuati eti nao wanachomekea .jamani vijana wanaisha
 
Zibaki pikipiki za kawaida za maofisini na private . Lakini sio hizi za biashara ya kubeba watu. Hawa vijana waofanya hizi biashara bado hawaja qualify kubeba abiria na kuingia barabara kubwa na hawana heshina na barabara .na wengi wao wanavuta BANGI na kunywa VIROBA. Na kama zitaruhusiwa basi ziwe za nje ya barabara kubwa . Au ziishie huku vichochoroni.

we unataka hawa vijana waanze tena kutuvunjia nyumba zetu usiku?
 
hawa jamaa kwa kweli hata mi nakubaliana na nyie wanatakiwa watolewe kwenye barabara kuu kwa sababu sio tu wanahatarisha maisha ya abiria zao bali wanahatarisha maisha ya wenye magari maana hawa jamaa hawaangaliagi magari wanapita popote tuu...wapewe barabara zao au wapigwe marufuku
 
Harafu wakishakuchomekea kwenye gari bahati mbaya ukamgonga. Ukisimama wakikukata kwa jinsi walivyo na umoja wanakuua
 
Back
Top Bottom