Dar-Mbeya -Dar (Return ticket) ni Tsh. 249,000/=(including tax & other charges).
Songwe mpaka mjini ni dakika 20, usafiri unategemeana na wewe unataka utumie nini, lakini kuna shuttle sh. 5,000, taxi sh. 15,000 -20,000, daladala sh. 500, pia kuna coaster zinazotoka Tunduma ni sh. 1,000, pikipiki ni sh. 3,000.
Angalizo, usafiri wa daladala, coaster za Tunduma na pikipiki unapatikana nje kabisa ya uwanja (yaani kwenye barabara kuu ya Mbeya -Zambia).
Ukifika mjini, nauli toka Mbeya mjini mpaka kyela ni sh. 3,500 (coaster) na ni mwendo wa dakika 45.
Kwahiyo kwa uchawi wa mzungu, kutoka Dar mpaka Kyela kwenye mchele wa ukweli utatumia masaa 2 na dakika 35.
Ukienda kwa njia ya Magufuli (barabara/basi), utatumia masaa 12 mpaka Kyela, lkn utafaidi kuona vivutio vya utalii mbugani Mikumi, Ruaha, misitu ya Mufindi, milima ya kitonga n.k.
Ni matumaini yangu kuwa nimejibu maswali yako.