Barabara mbaya sana hii,sababu ni kuwa uendeshaji wakati wa usiku ni shida kwa sababu ya taa za magari kuwa kali sana zinamulika dereva machoni tahadhari inatakiwa sana hasa usiku ukizingatia magari ya siku hizi mwanga wa taa ni mkali sana labda iwe kwa ajili ya shughuli maalum kama mbio za magari.lakini kwa matumizi ya public haifai.Pili ni kuwa baada ya mapungufu haya kuonekana ndiyo sababu barabara za siku hizi zinatengenezwa kwa mzunguko(meandering) ili magari yasiwashiane taa kwa muda mrefu vilevile kupunguza mwendo kasi kwani hujui utakachokutana nacho katika kona inayofuata au utauona mwanga wa taa kwa pembeni kabla ya kuifikia kona.