Kibongo bongo ni vigumu sana kuwa na viwango vya juu vya usafi wa mwili.
Kwanza, hakuna elimu ya kutosha kuhusu usafi wa mwili. Watu hawajui hata tofauti ya deodorant, antiperspirant deodorant, na body spray.
Pili, vitendea kazi na viwezeshaji hakuna vya kutosha. Havipatikani kiurahisi. Hebu nenda hapo kwa Mangi uulizie kama ana astringent (kama hata unaijua ni nini).
Tatu, maisha magumu. Watu hawana bajeti ya kutosha kuwawezesha kununua vitu ambavyo si muhimu sana katika uhai wao sembuse viondoa harufu, visafisha kinywa vya ziada, na kadhalika?
Nne, miundomsingi isiyoaminika. Maji kukatika hovyo, sehemu zingine ndo hayatoki kabisa. Kwingine hutoka bila mpango maalumu hivyo kulazimika kuyategea kimachale machale. Umeme nao haueleweki.
Tano, kutokuwa na mazoea ya kwenda kufanyiwa physical kila mwaka.