Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Feb 17, 2010.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Walter Sawe

  TANGU Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani (2005), nimekuwa nikifuatilia staili ya Chama tawala Cha Mapinduzi (CCM), kinavyotumia njia mbalimbali kujisafisha.

  Hakuna ubishi kwamba CCM ina mbinu nyingi katika kujisafisha na baadhi ya njia inazotumia, zinavutia, zinachekesha, zinashangaza na kutafakarisha.

  Ni staili ambayo inazua maswali yasiyo na majibu au yenye majibu yasiyoridhisha kwa umma wa Watanzania kama ilivyotokea hivi karibuni mjini Dodoma.

  Binafsi safari hii nimejiuliza maswali kadhaa kwamba CCM inajisafisha na nini? Ni uchafu gani inaojaribu kujisafisha? Uchafu huo umeingiaje? Na umeingizwa na nani?

  Ikumbukwe kuwa tangu tuhuma dhidi ya viongozi wa CCM zitolewe pale Mwembe Yanga, Temeke, Septemba 15 mwaka juzi na viongozi wa upinzani, ikiwahusisha na ufisadi wa aina mbalimbali, kuanzia ule wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Richmond na nyumba za serikali.

  Katika utawala wao wa miaka minne tu, ufisadi umekithiri serikalini, huku rais na mawaziri wake, wakiutetea waziwazi hata kwa kutumia mamilioni ya fedha za umma kuzunguka mikoani kuhadaa wananchi.

  Wananchi maskini na wanaharakati wamekuwa wakipuuzwa, huku baadhi ya viongozi wakitoa kejeli mbalimbali kwamba kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi.

  Ndani ya miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, viongozi wametumia madaraka yao vibaya kuliko miaka kumi ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne.

  Kutokana na hali hiyo, wapo wana CCM wanaosema bila woga kutaka Rais Kikwete asiongezewe muda kwa madai kuwa ameshindwa kuchukua maamuzi magumu dhidi ya mafisadi ndani ya serikali yake.

  Naipongeza ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe na kusababisha Lowassa na mawaziri wengine wawili kuachia ngazi.

  Je, kuondoka kwa Lowassa, Kikwete atapona? Umma wa Watanzania tuliliangalia suala la Richmond kwa haraka na kummwagia tuhuma zote Lowassa kana kwamba yeye alikuwa peke yake!

  Kwanza, Lowassa alikuwa mtumishi na mteule wa rais na mtekelezaji wa maagizo ya Rais. Kwa mujibu wa Katiba yetu, waziri mkuu hawezi kutekeleza suala lolote kitaifa ambalo hajaagizwa na rais, halafu rais asimfukuze kazi.

  Sawa, Richmond imeonyesha maagizo ya Lowassa na shinikizo lakini Lowassa angekuwa kajituma tu bila kutekeleza agizo au makubaliano angefukuzwa kazi na Rais? Haya na mengine mengi ukweli unabaki palepale kwamba usafi wa Lowassa ndio uchafu wa CCM.

  Namalizia makala yangu hii kwa kuwaeleza umma wa Watanzania kuwa kuna mambo ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne mazuri ambayo wanajivunia ni matunda ya Lowassa.

  Mara zote ndani ya serikali na ndani ya chama, Lowassa alikuwa mtendaji, msimamiaji na mtekelezaji. Mwanzo wa makala yangu nilisema usafi wa Lowassa ni uchafu wa CCM.

  Napenda Watanzania wenzangu wapenda haki tuelewe kwamba Lowassa kama kiongozi alikuwa habanwi kwa ufisadi bali kwa uwajibikaji wa pamoja kama msimamizi mkuu wa shughuli za serikali, Watanzania tumekuwa wepesi wa kusahau mambo.

  Wakazi wa Shinyanga na Kahama watamkumbuka Lowassa akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo alidiriki kuwa tofauti na Wamisri na kuwapatia maji kutoka Ziwa Victoria na yapo hadi leo. Hiyo ni kazi ya Lowassa.

  Ni Lowassa huyuhuyu alifuta umiliki wa viwanja vya tajiri mmoja, ambapo leo ndipo yamejengwa majengo ya PPF, International House, ni Lowassa aliwafukuza nchini City Water mwaka 2005, baada ya kushindwa masharti na kuilipa serikali sh bilioni 15.

  Ni Lowassa huyuhuyu aliyesimamia shule za kata, hata kama walimu hakuna.

  Ni Lowassa huyuhuyu aliyesimamia chakula cha njaa kikasambazwa kila tarafa, kata hadi kijijini.

  Ni Lowassa huyuhuyu aliyepunguza foleni jijini Dar kwa utaratibu wa njia tatu hadi leo upo na nyingine zikapanuliwa kwa maelekezo yake.

  Lowassa ameonyesha uungwana wa hali ya juu. Yeye ameamua kujiuzulu wadhifa aliokuwanao. Ingawa jamii imekwisha kuamini hayo yaliyosemwa sana juu yake, bado anayo nafasi.

  Nimalizie makala hii kwa kuchavusha fikra zetu. Rais Kikwete aliwahi kusema yaliyomkuta Lowassa ni ajali ya kisiasa. Naamini Lowassa alipokuwa akifanya maamuzi mengi kati ya niliyoyataja hapo juu, tulimshangilia na kumsifia kana kwamba kiongozi shupavu. Nauliza, je, utamaduni huu wa kumalizana utatupeleka wapi?
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Natumaini haujatumwa Mkuu

  Kama CCM ni Chafu, Lowassa ni msafi ki-vipi? Katika CCM hakuna msafi - hata hao wanaojiita "Wapambaji au Wapambanaji" ndani ya CCM ni yale yale - wakikaa kama kamati ya Chama kujadili mada yoyote ni lazima ipite hata kama imeoza!

  Hebu tuweke utani kando!
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 1,052
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  ==
  Baba Enock

  Kwa yaliyotokea Dodoma wiki hii, nashawishika kiasi kuamini kuwa ufisadi ni wa CCM si wa Lowasa. Time will tell, Lowasa atasafishwa kwa gharama nzito ya CCM. Haiwezekani watu wakaenda Dodoma wakiitwa mafisadi, wakarudi baada ya siku mbili wakiitwa watakatifu.
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  CCM ni mafisadi na sio Lowasa na nadiriki kusema kuwa Lowasa alikuwa msafi ila alifanya hivyo kwa ajili ya wakubwa wake
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  LOWASA hasafishiki maana kashindwa kututhibitishia kwanini yeye hakuhusika na madudu ya Richmond, huyu ni Fisadi kabisa, hana hadhi mbele ya UMMA , ingekuwa China leo wangekuwa mamemzikia mbali kwa kumnyonga........Baba Enock Lowasa ni kimeo.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  alikuwa Mchapakazi sana, ila amejawa na tamaa sana, maisha yake yana utata nwingi, hatufai.
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sasa hapa nani ni mchafu??ni Lowassa au CCM na mfumo wote?? hapa ndio watu makini na hasa Chama cha CHADEMA waje wasema juu ya kauli kama hizi. RICHMOND kwetu sisi hajaisha kabisa mpaka wote wafikishwe mahakamani na kuona ni nani yupo sahihi na sio vikao vya secret kama hivi
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  CCM na wanachama wake wate ni kikwazo, ila kuna wachama mmoja mmoja wao wamejitokeza kuwa mafisadi papa zaidi, hawa ni Rostam AZIZI, lOWASSA, Karamagi na wenzao wengine na mashabiki wao kama kina Makamba, Mahanga .
  Lowasa hasafishiki, maana kazungukwa na wezi wa mali ya UMMA, na yeye anahusika , maana wamejitahidi kujisafisha kupitia vijarida vyao pale Kijiweni New Habari..............lakini wapi, umma umewajua, kuwa ni wezi watupu.
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Labda yeye amemua kukaa kimnya ndio maana inakuwa shida sana leo hii na pia kama anngeamua kusema basi yangekuwa makubwa sana ila ila kama sisi Watanzania wakiamua kusema basi ndio dawa yao na wao hata waseme wao walikuwa kimnya sana. Hakuna hata mmoja msafi ndani ya CCM
   
 10. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  "15% wanaipenda CCM, 15% wanaichukia CCM, na 70% ni wafuata mkumbo" By J.K, Chairman of CCM!!
  Nakushauri ushawishike 85%(wanaoichukia na wafuata mkumbo) njaa ndio zinazowasumbua! Ndio maanda wanapiga makele ya ufisadi, na uchaguzi unapokaribia wanakaa kimya kusubiri msaada toka kwa hao waliowaita mafisadi!!
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Josh, watu wengi hudhani kuwa haongei, anaongea sana, anatumia vyombo habari vya RA, Na Karamagi, kama ni msomaji mzuri utang'amua kuwa hata makala zingine jamaa hujikunja kuziandika, ni ngumu kuthibitisha ila kimantiki inawezekana......
  Lowasa kama yeye shujaa kweli aibuke hadharani na sikuendesha vita vya msituni, vya kuwatumia waandishi njaa.
  kweli Lowasa hapaswi kuwaza kurudi mamlakani kama Waziri Mkuu, Makamu wa Rais ama Raisi, huyu hakujizulu kwa sababu ya uwajibikaji ama kwa makosa yaliyotendwa na wasaidizi wake, alijiuzulu kwa aibu na fedheha ya kula Rushwa na kupokea milungula ktk kuipendelea Richomonds.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,524
  Likes Received: 576
  Trophy Points: 280
  Anayemwita Lowassa ni msafi:

  1. Au wewe ni mtoto sana yaani hukuwepo wakati Nyerere anamwita Lowassa Mwizi. Na hii ilikuwa ni kabla ya EPA na kabla ya Mkapa hajawa Rais.

  2. Una kumbukumbu fupi sana.

  Lowassa hajaanza kwenye Richmonduli. Lowassa kaanzia AICC Arusha na alipofika wizara ya Ardhi akamaliza kazi. Richmonduli walikuwa wengi na alikuwa kaanza kutafuta pesa za kugombea Urais na si kujilimbikizia maana kama miradi, basi wajukuu wake hawana wasiwasi na umasikini. Labda aje kichaa awafilisi mali zao.
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kweli umekumbusha sakata hilo, ambapo JK Nyerere alimwita mwizi hadharani mbele ya watu, hakukanusha, na amebaki kuwa mwizi hivyo mpaka leo, alikula nyama ya mtu, basi hawezi kuacha kirahisi.
   
 14. Prisoner

  Prisoner Senior Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi namsapoti MH. Lowassa tena angegombea urais mimi kura yangu nampa kwani kweli Fisadi sio Lowassa Fisadi ni Sisiem
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wewe upo sahihi kabisa maana ukifika wakati wa uchaguzi ndio kelele zinakuwa nyingi sana na pia ni hatari sana katika taifa ketu na kuona kama kweli wanataka kuwataja mafisadi tu
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  kuna mkubwa tena ndani ya ccm zaidi ya lowasa???????

  hebu tuache utani saaa zingine jamani..................
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nakuja kwa staili nyingine kabisa ninamuona Lowassa kama masiha wetu aliyeletwa kuikomboa nchi yetu simwiti masiha kwa wema wake au kwa matendo aliyotufanyia wakati wa uongozi wake ila kwa kufanya kazi ambayo hata yeye hajui kuwa anaifanya kukisambaratisha chama kilichoshika hatamu kwa kutumia Richmond atakapomaliza hii kazi tutamshukuru kwa hilo na kumuomba akapumzike kwani madaraka yeye hayawezi
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mimi naona watu hawa wanatuzuga sana sisi Watanzania na kwa mambo haya basi sisi kama Watanzania tukatae ujinga huu na zuga kama hizi na pia. Walikuja hapa na kusema mengi sana juu ya mambo ya Richomond na leo wote ni wamoja ila WAMELIPOTEZEA TAIFA LETU PESA NYINGI SANA. hii ni dhuruma kubwa sana. Kuna haja ya kukataa mambo haya mimi nasema basi CCM wote ni wachafu makuu wangu
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Utaamuaje kukaa kimya wakati unachafuliwa na wewe mwenyewe unaamini kwamba hukuhusika? :confused: Kapewa nafasi chungu nzima ya kujisafisha na kutueleza Watanzania nini hasa kilichojiri katika sakata la Richmond lakini hadi hii leo ameamua kuwa bubu. Kumbuka kimya kirefu kina mshindo. WOTE ndani ya CCM ni mafisadi wakubwa na wanaipeleka nchi yetu pabaya.
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sisi tunasema EL ni fisadi wao CCM wanasema hakuna hata mtu mmoja fisadi ndani yao je tujue lipi. alifanya hivyo ili kulinda wakubwa wake wa kaya na mkuu wa kaya pia. maana kwa suala hili katk taifa imara na vyama vya upinzani imara tungeitisha uchaguzi mkuu mapema na kuona serikali yote inatoka au kuangushwa kabisa. Yeye alikuwa kimnya aliamua kilinda kitumbua cha mkuu wa kaya
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...