Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM

Binafsi EL kama binadamu yoyote yule anamapungufu yake. Kwenye hili la Richmond nahisi amelivalia junga kwa sababu anaona ameonewa. RA ni beneficiary wa Richmond. ametake cover nyuma ya EL kupunguza mashabulizi kwake.
CCM pamoja na viongozi wake, wanamatatizo makubwa ya kutoa maamuzi magumu. Hivi issue ya Chenge inahitaji mjadala? Katika utawala bora , M/kiti angemuita na kumwambia aresign kutoka kwenye chama. Mpasuko ndani ya CCM ni kwa sababu hamna mtu ambaye yuko tayari kuchukua action kuhusiana na major issues zinzaotokea.
 
Sisi tunasema EL ni fisadi wao CCM wanasema hakuna hata mtu mmoja fisadi ndani yao je tujue lipi. alifanya hivyo ili kulinda wakubwa wake wa kaya na mkuu wa kaya pia. maana kwa suala hili katk taifa imara na vyama vya upinzani imara tungeitisha uchaguzi mkuu mapema na kuona serikali yote inatoka au kuangushwa kabisa. Yeye alikuwa kimnya aliamua kilinda kitumbua cha mkuu wa kaya

Kama kweli hakuhusika basi ni bora kuuweka hadharani ukweli wa mambo badala ya kuendelea kuubeba msalaba usiomuhusu. Kama kuusema ukweli kungesababisha Serikali ivunjike basi nadhani Watanzania wengi tungeliunga mkono hilo la Serikali ya kisanii kuvunjika ili kuwepo na uchaguzi mwingine. Fumbo mfumbie mjinga......

Have a great day :)
 
Huyu lowassa kimeo, lini tutam ignore na kumtupa kwenye dusty bin!

Hasafishiki, ni mwizi na mpenda madaraka hatari sana huyu jamaa lol
 
Mimi naona watu hawa wanatuzuga sana sisi Watanzania na kwa mambo haya basi sisi kama Watanzania tukatae ujinga huu na zuga kama hizi na pia. Walikuja hapa na kusema mengi sana juu ya mambo ya Richomond na leo wote ni wamoja ila WAMELIPOTEZEA TAIFA LETU PESA NYINGI SANA. hii ni dhuruma kubwa sana. Kuna haja ya kukataa mambo haya mimi nasema basi CCM wote ni wachafu makuu wangu

Hapo umenena mkuu. Nilikuwa na wasiwasi kuwa thread inataka kumtenganisha EL na chama chake na kumpa usafi asio nao. Ukitaka kuwafafanua hawa CCM usichague kazi au kauli zao vipande vipande (cherry picking). Piga uchambuzi wa ujumla (holistic) ndipo ukweli utakapokudhihirikia kuwa vingi wanavyofanya vina mkakati mahsusi wa ulaji.

Usidanganyike na kelele za shule za kata, kilimo kwanza, zinduka, vocha za mbolea, umeme wa dharura, n.k. huku utendaji ukiwa haba. Yote hayo ni kutupiga kiza ili tusione ufisadi ndani yake au kudai maendeleo ya kweli kutokana na mapato ya taifa. Kwa rasilimali tulizonazo, serikali makini TZ ingeweza kufanya mambo bora zaidi katika ujenzi wa shule za maana, mifumo ya umeme wa uhakika, kilimo chenye tija, miundombinu imara ya barabara na reli, n.k.
 
alikuwa mchapakazi sana, ila amejawa na tamaa sana, maisha yake yana utata nwingi, hatufai.
huyu bwana kwa kweli ni mchapakazi sana lakini kwa kutumia kigezo chochote huwezi kumtoa katika kundi la mafisadi waliopo tanzania hivi sasa. Kwa ufupi huyu bwana ni fisadi na hafai kupewa nafasi yeyote ya juu kimaamuzi kwa sababu atakomba kila kitu.
 
Hapo umenena mkuu. Nilikuwa na wasiwasi kuwa thread inataka kumtenganisha EL na chama chake na kumpa usafi asio nao. Ukitaka kuwafafanua hawa CCM usichague kazi au kauli zao vipande vipande (cherry picking). Piga uchambuzi wa ujumla (holistic) ndipo ukweli utakapokudhihirikia kuwa vingi wanavyofanya vina mkakati mahsusi wa ulaji.

Usidanganyike na kelele za shule za kata, kilimo kwanza, zinduka, vocha za mbolea, umeme wa dharura, n.k. huku utendaji ukiwa haba. Yote hayo ni kutupiga kiza ili tusione ufisadi ndani yake au kudai maendeleo ya kweli kutokana na mapato ya taifa. Kwa rasilimali tulizonazo, serikali makini TZ ingeweza kufanya mambo bora zaidi katika ujenzi wa shule za maana, mifumo ya umeme wa uhakika, kilimo chenye tija, miundombinu imara ya barabara na reli, n.k.
Kuna haja ya kupata watu makini na sio kama ilivyo sasa hivi. Wewe ukiona unakula na watu kama hawa na kukaa meza moja nao eti kupunguza mpasuko basi sisi wote ni wagonjwa. Kama mtu fisadi basi kufungwa maana hapa ni hasara kwa taifa na sio kwa CCM kama ilivyokuwa leo katika siasa za Tanzania/ Labda aje Dr.SLaa na aseme yeye juu ya mambo haya. Na sisi wananchi tutaendelea kuhoji mpaka watu wote walihusika na mambo ya ajabu kufugwa na kushatakiwa kama raia wengine vile walihusika na hasara katika Taifa letu.EL na RA na CCM wote ni wamoja hivyo hakuna jipya juu ya mambo haya
 
nimekwisha choka na uozo wa Tanzania yetu. Huwa nikikaa na kumfikiria Edward Lowasa alivyoingia madarakani na akiwa anahutubia wananchi akisema ndege ya uchumi wa tanzania sasa inapaa??? Huwa mpaka nacheka kwa hasira!!
 
haya ndio mauza uza ya Tanzania na serikali yake hivyo kuna umuhimu sana wa kujua hatma ya watu hawa. isiwe ni huruma ya mtu binafsi ila ni kwa watu
 
haya ndio mauza uza ya Tanzania na serikali yake hivyo kuna umuhimu sana wa kujua hatma ya watu hawa. isiwe ni huruma ya mtu binafsi ila ni kwa watu
ukitaka kuwajua raia wataifa fulani mwangalie kiongozi ama viongozi wao wajuu kitaifa..............unajua viongozi wetu wanaghiliba nyingi, ujanja ujanja.
wamechukua taswira halisi ya watanzania halisi, kupenda majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
LOWASA hasafishiki maana kashindwa kututhibitishia kwanini yeye hakuhusika na madudu ya Richmond, huyu ni Fisadi kabisa, hana hadhi mbele ya UMMA , ingekuwa China leo wangekuwa mamemzikia mbali kwa kumnyonga........Baba Enock Lowasa ni kimeo.
Wananyonga tu mtu akihukumiwa kwa haki. Lowassa kapewa "hearing" wapi na nani???/
 
Kama kweli hakuhusika basi ni bora kuuweka hadharani ukweli wa mambo badala ya kuendelea kuubeba msalaba usiomuhusu. Kama kuusema ukweli kungesababisha Serikali ivunjike basi nadhani Watanzania wengi tungeliunga mkono hilo la Serikali ya kisanii kuvunjika ili kuwepo na uchaguzi mwingine. Fumbo mfumbie mjinga......

Have a great day :)
Mbona utetezi wake aliompa Sitta kauwekwa kwenye rirpoti ya Richmond?
Katika dili la Richmond Lowassa amewekewa kiasi gani kwenye account au alikuwa apate ngapi? Watu waliopokea mpaka mahela kwenye account zao wala hawana kazi nao, wao wako na Lowassa, hii inatoa picha kuwa tatizo hapa si kupinga ufisadi bali ni kupinga mtu kama mtu.
 
Maneno yako kuntu kwa yule ambae hana uvivu wa kufikiri wala fikra mgando.
 
Wananyonga tu mtu akihukumiwa kwa haki. Lowassa kapewa "hearing" wapi na nani???/
aLIPEWA NAFASI YA KWANZA KUCHANGIA mjadala wa Richmond..akasema kuwa anaonewa,....."
nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana
..."
hiyo ilikua ni kilio chake...sasa hapo palikua mahala sahihi kutuambia ninini mchele, ninini mbumba, mwanaume chozi la madaraka likamtoka.
kwakweli Lowassa anapakujieleza, bahati mbaya anatumia vibaya vyombo vya habari vya RA, KARAMAGI katika kutaka kutuaminisha kuwa yeye si FISADI, na kwamba alionewa tu, rejea Tahariri ya leo katika gazeti la Mtanzania..hasafishiki labda akaogelee kwenye pipa la ACID.
 
hakuna cha lowassa wala ccm aliye msafi wote wananuka halufu ya ngozi iliyoyolekwa ikiwa mbichi
 
Huyu lowassa kimeo, lini tutam ignore na kumtupa kwenye dusty bin!

Hasafishiki, ni mwizi na mpenda madaraka hatari sana huyu jamaa lol

Mkuu Tumain, hakuna atakayetupwa kwenye dustbin. Hawa mafisadi wanafahamu kwa kina madhambi mengi yaliyofanyika ili kuhakikisha jamaa anaingia Ikulu na ndiyo yanawapa kiburi cha hali ya juu ya kuleta tafrani ndani ya CCM ili kuhakikisha wabaya wao wote wananyamazishwa ili wao wawe Vinara ndani ya chama hicho. Mkuu wa kaya analijua hilo ndiyo maana hatii neno kuhusu mafisadi hao maana akijaribu kuwajia juu tu na wao kuamua liwalo na liwe na kuanika kila kitu hadharani kuhusu madhambi yaliyofanywa katika safari za kuelekea Ikulu 2005 basi itakuwa patashika nguo kuchanika wala hakutakuwa na cha msalie mtume. Nchi itawaka moto na kundi lote la mtandao kuumbuka.
 
Kuna haja ya Watanzania kujua na kuona kukataa kabisa hali kama hii ya kutuzuga kama hivi ilivyo sasa hivi maana kuna kila dalili za aina ya kuwafanya watanzania ni wazembe.
 
Mambo ya CCM waachie CCM wenyewe, mie sina chama so simulaumu yoyote, I take things in my own hands
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom