USA Yaahidi dola millioni 212 Gaza

USA Yaahidi dola millioni 212 Gaza

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,574
Reaction score
53,613

  • Saa moja iliyopita
Mshirikishe mwenzako

140915021339_john_kerry_tour_arab_countries_512x288_getty.jpg
John Kerry Katikati na viongozi wa mataifa ya kiarabuMarekani imeahidi dola millioni 212 za msaada ili kusaidia kulijenga eneo la Gaza katika mkutano wa kuomba msaada mjini Cairo.
Utawala wa Palestina unaomba dola bilioni 4 kulijenga eneo la Gaza baada ya siku hamsini za mapigano kati ya Israel na Hamas.
Takriban raia laki moja wa Gaza walipoteza makaazi yao katika vita huku miundo msingi pia ikiharibiwa.
Awali marais wa Palestina na Misri waliitaka Israel kudumisha amani ya mda mrefu.
Waliitaka Israel kuikabidhi Palestina ardhi walioiteka katika vita vya mwaka 1967 na kukubali suluhu kwa wakimbizi wa Palestina ili Israel Kutambulika.
Mgogoro huo wa wiki saba katika eneo la Gaza ambao uliisha baada ya makubaliano mnamo tarehe 26 Agosti,ulisababisha mauaji ya Wapalestina 2100 wengi wao wakiwa raia ,wanajeshi 67 wa Israel pamoja na raia sita wa taifa hilo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John kerry amesema kuwa huku msimu wa baridi ukikaribia ,maelfu ya raia wa Palestina walioachwa bila makao wanahitaji usaidizi wa haraka.

USA:Yaahidi dola millioni 212 Gaza - BBC Swahili

Waangalie nyuso zao! Waonesha hivi hivi wajinga!
 
140915021339_john_kerry_tour_arab_countries_512x288_getty.jpg

John Kerry Katikati na viongozi wa mataifa ya kiarabu

Marekani imeahidi dola millioni 212 za msaada ili kusaidia kulijenga eneo la Gaza katika mkutano wa kuomba msaada mjini Cairo.

Utawala wa Palestina unaomba dola bilioni 4 kulijenga eneo la Gaza baada ya siku hamsini za mapigano kati ya Israel na Hamas.

Takriban raia laki moja wa Gaza walipoteza makaazi yao katika vita huku miundo msingi pia ikiharibiwa.

Awali marais wa Palestina na Misri waliitaka Israel kudumisha amani ya mda mrefu.
Waliitaka Israel kuikabidhi Palestina ardhi walioiteka katika vita vya mwaka 1967 na kukubali suluhu kwa wakimbizi wa Palestina ili Israel Kutambulika.

Mgogoro huo wa wiki saba katika eneo la Gaza ambao uliisha baada ya makubaliano mnamo tarehe 26 Agosti,ulisababisha mauaji ya Wapalestina 2100 wengi wao wakiwa raia ,wanajeshi 67 wa Israel pamoja na raia sita wa taifa hilo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John kerry amesema kuwa huku msimu wa baridi ukikaribia ,maelfu ya raia wa Palestina walioachwa bila makao wanahitaji usaidizi wa haraka.

Chanzo: BBC

http://www.bbc.co.uk/…/…/2014/10/141012_gaza_marekani_msaada
 
hata hivyo Katar walisema watapajenga Gaza: US ni kiherehere chake tu, kwani ni kesho Hamas watarudi kuharibu miundombinu...
 
Awa watu nawashangaa kila mwaka wanapigana harafu kila mwaka wanakusanyana kukusanyana ela kuijenga Gaza.

umefika wakati wazuie uaribifu wa Gaza si ambavyo wanafanya sasa.
 
Namsuribi Mr.Membe aliyedai wapalestina ni Ndugu zake nifahamu naye kahaidi kiasi gani... Ndugu hatupwi?
 
hata hivyo Katar walisema watapajenga Gaza: US ni kiherehere chake tu, kwani ni kesho Hamas watarudi kuharibu miundombinu...
sio kiherehere! abass mwenyewe kaomba. basi hata kabla ya yeye kuomba qatar wangeenda! jumla ya $5.4bn zimekuwa pledged na wafadhili. pesa zote hizo zitarudi magharibi. simple economics!
 
Back
Top Bottom