USA vs CHINA: DUNIANI KUMEKUCHA.

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
218
Reaction score
319
Huu ni mpambano wa teknolojia ya uchukuzi. Huku USA wakijivunia uvumbuzi/ubunifu wa bwana Elon Musk ambaye anakubalika sana kwa sasa duniani, Mtu huyu anafanya uvumbuzi mwingi wa kisayansi kama vile magari ya umeme, kusafirisha watu kwenda sayari ya mars kwa mfupi na linalo vitia zaidi ni ubunifu wake wa treni ya mwendo kasi mithili ya mwanga, hii ni Teknolojia ya Hyperloop inayo kusudia kufanya trein isafiri katika tube lenge vacuum/ombwe. Hii ni kufanya trein isafiri bila ukinzani wa hewa toka katika angahewa hii yetu(atmosphere) na itakapo kamilika itakua na mwendo kasi wa km1200 kwa saa. Hii ni sawa na kusafiri toka Kigoma mpaka Dar wa Salaam kwa saa moja.
Wakati hayo yakisherekewa na Wamarekani , hiko China Chini ya Shirika la Sayansi na Teknolojia ya usafiri wa Anga, Wamekuja na mkakati kabambe kabisa kabisa. Wachina wanabuni teknolojia ya usafiri wa haraka zaidi kwa kuchanganya teknolojia ya Trein ya umeme/sumaku na Teknolojia ya ndege na hivyo kuunda Trein inayo paa/ruka"The Flying Trein" Trein hii inatarajiwa kuwa na mwendo wa KM4000 kwa saa, Sasa kwa Trein hii ya Mchina unatoka Kigoma Mpaka Dar es Salaam kwa dakina kumi na tano tu (robo saa).Yaani ukikaa kimya chai basi Unapo maliza watu wanakua tayari wamefika Dar toka Bukoba.
Tuombe uzima ili Tuone mwisho ya yote nani ataibuka Mshindi.
 
Wachina ni matapeli tu.Hawajawahi kuwa na teknolojia yao hasa inayoeleweka.Sanasana wanategemea wageni wanaotorosha teknolojia kutoka USA na Ulaya.
Tatizo mchina akiangalia teknolojia flani, basi yeye anauwezo wa kuiboresha mara1000 na kumzidi mbali originator wake.

Mfano, angalia teknolojia ya mawasiliano alivyoibadilisha na kuirahisisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mchina akiangalia teknolojia flani, basi yeye anauwezo wa kuiboresha mara1000 na kumzidi mbali originator wake.

Mfano, angalia teknolojia ya mawasiliano alivyoibadilisha na kuirahisisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Anakuwa akitambulishwa mchina ndiye mmliki lakini nyuma ya pazia wapo wenye umiliki halisi.Hivi kwa kumtazama tu mchina kweli anaweza kuvumbua kitu cha maana zaidi ya mabakuli ya udongo?
 
Inapendeza sana...

Nilitaka kushauri na sisi tupeleke wasomi watakoiba huo ujuzi na kirudi nao hapa Tanzania tuunde vya kwetu...

Nimekuja kukumbuka hata wakifanya hivyo na wakarudi na huo ujuzi hawatapewa support yoyote...


Cc: mahondaw
Hapo ndio tatizo Mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…