USA na mashambulizi ya kutumia Drone

USA na mashambulizi ya kutumia Drone

Keyboard_Warrior

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
6,108
Reaction score
10,480
Heshima kwenu wakongwe..!

Nilishawahi kuangalia series fulani ya Wamarekani, kwenye hiyo series kuna askari mmoja ambaye alikuwa ni Pilot wa ndege zisizokuwa na rubani ndani yake (Drones), kuna siku huyo askari alipewa kazi ya kumlipua mtu mmoja aliyedhaniwa kuwa ni gaidi, alifanya kama alivyoagizwa na wakuu wake akarusha bomu kutoka kwenye drone akamlipua mtu yule. Lakini kumbe kulikuwa na makosa, yule mtu aliyelipuliwa hakuwa gaidi, hivyo aliuawa kimakosa.

Leo nilikuwa naangalia series ya Homeland, niko season ya 4 episode ya kwanza, kwenye hii episode CIA wanafanikiwa kumuona gaidi wanayemuwinda muda mrefu, huyo gaidi yupo ndani ya jengo, kuna tukio la kifamilia lilimfikisha pale. CIA wanaamua kulipua jengo ili kumuua yule gaidi, lakini ndani ya jengo kulikuwa na watu wengine wasio na hatia, hivyo watu wasio na hatia wanalipuliwa pamoja na gaidi yule.

Kwenye jengo kulikuwa na watoto wadogo na wakina mama pia.

Nakuja kwenye lengo la uzi huu:

1) Hivi ni kweli USA huwa wanafanya mission za namna hii?
Au ni maigizo tu hamna kitu kama hiki?

2) Kama ni kweli, huwa wanawajibishwa kwa matatizo yanayojitokeza baada ya kukamilika mission za namna hii?, kwenye matatizo namaanisha madhara ya missions za namna hii kwa watu wasio na hatia.

3) Je, kuna sera au taratibu zozote zilizowekwa na UN juu ya matumizi ya drones za kivita kwa nchi zinazomiliki drones hizo?
 
Us hana ndugu anashindwaje kufanya hivo... collateral damage
Lakini hiyo "collateral damage" si inachangia ugaidi kutoisha..?
Kwasababu ikitokea mauaji ya wasio na hatia ni lazima ndugu za hao waliofanyiwa mauaji watafute namna ya kulipa kisasi kwa kuidhuru USA na raia wake..!
 
USA huwa hanaga huruma na raia ambao sio wa nchi yake ile kusema aliacha kushambulia Iran sababu angeua raia wengi niuongo tu alipima maji kaona kina kirfu kageuza,USA ataua hata watu 30 sababu kuna mmoja anamtafuta.
 
Hayo ma2kio ni ukweli m2pu MKUU Halafu Hkuna wakuwawajibisha Maana Wao Sindio wanajiita Polisi Wadunia Waliivamia IRAQ kisa eti kuna silaha za suku na mpala leo hawajazipata na bado wa2 wanakufa umeona ama kusikia wap kama jamaa wana wajibishwa na yyte ?!


Us Tukiwa tunalalama yakwamba wanaua watu wasokua nahatia hua watu hawaelewi ama huona kama tunaleta udini

US Kama anataka ww ufe bila ya sababu alimuradi 2 kutimiza malengo yake basi lazma ufe 2 haijalishi nn wala nn MKUU


US WAUAJI
 
Missions za namna hiyo zipo lakini mara zote kitu kinachoitwa Evaluation hufanyika ili kujiridhisha na kujua kiasi cha madhara yatakayoweza kudhibitiwa na kisha ndipo shambulizi la aina hiyo hufanyika pale ambapo njia nyinginezo zimeshindikana kutokana na sababu mbalimbali.

Katika mpango wa kukabiliana na ugaidi kuna baadhi ya maamuzi hufanyika mapema ili kuzuia madhara makubwa zaidi. Mfano. Kuna sheria mbalimbali za kukabiliana na ugaidi zinazolipa Jeshi ruhusa ya kuzitungua kwa makombora ndege hususani za abiria iwapo zimetekwa na magaidi hata kama zina abiria wengine (wasio na hatia) ndani yake.

Hiyo ni kwa ajili ya kuzuia madhara makubwa zaidi kama yale ya Septemba 11, 2001 yasiweze kutokea. Hapo Jeshi litalazimika kutumia SAM ama Heat Seeker kuitungua ndege husika pale ambapo juhudi za kuilazimisha kutua salama zimeshindikana.

Hilo si kwa Marekani tu bali hata katika baadhi ya nchi zingine kama vile Urusi pia ina mpango huu maana katika suala la ugaidi si jambo la kutegemea sana kwamba kutakuwa na Demand ya Ransom baada ya utekaji kufanyika. Mara nyingi magaidi wamekuwa Trained hata katika Suicide Missions ambapo inayalazimu majeshi ya mataifa mbalimbali nayo kuja na mbinu mbadala kukabiliana nao kabla hawajadhuru idadi kubwa ya raia.
 
Drone inasaidia kufanya mashambulizi sehemu ambayo ni ngumu Sana kwa jeshi kufika kutokana na kuofia maadui.
Pasipo drone mashambulizi Kama Yale ya visima vya mafuta vya Saudia yasingefanyika
 
Back
Top Bottom