US: Kikundi kinachodhaminiwa na IS cha Msumbiji kisipodhibitiwa, uasi unaweza kuhamia Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Marekani imetahadharisha hili kuwa makundi ya wanamgambo yameendelea na operesheni zake nchini Msumbiji katika eneo la Kaskazini la Cabo Delgado huku yakiungwa mkono na wanamgambo wa Islamic State.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia vijiji mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mkuu wa operesheni maalum ya Marekani barani Afrika Meja Jenerali Dagvin Anderson, amewaambia wanahabari kuwa kundi hilo limekuwa likipata msaada kutoka nje, hali inayolifanya kundi hilo kuwa hatari zaidi.

''Tumewashuhudia katika kipindi cha miezi 12 mpaka 18 wakiimarisha uwezo wao wao, wa mashambulizi, na kutumia mbinu ambazo hutumika pia katika maeneo mengine ya ulimwengu- Mashariki ya Kati ambako kuna makundi yenye uhusiano na Islamic State'', alisema Jenerali Anderson

Uasi wa wanamgambo wa kiislamu waliojitokeza katika kona ya mbali ya Msumbiji umegeuka kuwa vita vya wazi katika wiki za hivi karibuni, na ripoti za mauaji ya watu, kukatwa kichwa na kutekwa nyara kwa miji miwili katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado, aliandika mwandishi wa BBC Africa Andrew Harding mwezi Mei

Watu wenye silaha walitembea taratibu katikati ya majani marefu, wakipita kando ya jengo kubwa jeupe wakionekana kutosumbuka kabisa na mlio wa risasi.

Wengi wakiwa na silaha na walivaa aina mbalimbali za mavazi yaliyoonekana kuwa ya jeshi la Msumbiji. Milio michache zaidi ya risasi ilisikika kwa mbali na mmoja alipaza sauti ''Allahu Akbar''- Mungu ni Mkubwa.

Picha ya video, iliyopigwa mwezi Aprili kwa simu ya mkononi wilaya ya Muidumbe ulikuwa ushahidi wenye nguvu kuwa mzozo uliokuwa gizani katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji sasa umekuwa katika eneo la wazi kabisa kwa namna ambayo ni ya hatari.

Video ya pili, iliyochukuliwa majuma machache kabla, ilimuonesha mtu mmoja aliyekuwa amekufa, askari akiwa amelala kwenye dimbwi la damu. Kamera kisha zikatembea na kunasa mwili mwingine, kisha mwili mwingine ukiwa chini ya gari nyeusi ya polisi, kisha ikarekodi mwili wa nne ukiwa sehemu ya wazi, na kisha rundo kubwa la silaha kwenye eneo ambalo linaonekana kuwa ghala la silaha la polisi au jeshi.

Wana uhusiano wa karibu kiasi gani na Islamic State?

Picha hizo za video zilipigwa katika eneo la bandari Mocimboa da Praia, ambalo lilidhibitiwa kwa muda na wanamgambo tarehe 24 mwezi Machi. Siku mbili baadae, wanamgambo hao walidhibiti mji mwingine muhimu wa Quissanga.

''Sasa wana silaha na magari, yanayowafanya waweze kutembea kirahisi na kufanya mashambulizi kwenye eneo kubwa. Na hutumia sare za wanajeshi. Hivyo, watu huchanganyikiwa na kuogopa,'' anasema Askofu wa kikatoliki wa Pemba, Luiz Fernando Lisboa.

Mashambulizi makubwa mawili ya kijeshi ni ushahidi kuhusu mabadiliko ya mipango ya kundi hilo lifahamikalo kwa jina al-Shabab, ingawa halina uhusiano na kundi la wanamgambo wa kisomali wenye jina sawa na hilo, lenye uhusiano na al- Qaeda.

Kundi hili lilitumia miaka miwIli iliyopita kutekeleza operesheni zao mafichoni, likivishambulia vijiji vya mbali , ikishambulia misafara ya kijeshi iliyo kwenye doria kwenye barabara zilizo pweke, vitendo vya kigaidi dhidi ya jamii za vijijini, na kusababisha watu 200,000 kuyakimbia makazi yao, lakini lilikuwa kwa kiasi kikubwa halioneshi sababu ya kufanya vitendo hivyo, wala uongozi wake wala madai ya kundi hilo.

Picha za video kutoka pande za wilaya ya Mocimboa da Praia na Muidumbe kwa haraka ziliingizwa katika filamu za propaganda za kundi la wanamgambo wa Islamic State (IS), iliyorushwa na shirika la habari la Amaq.

IS imedai kuhusika na mfululizo wa mashambulizi nchini Msumbiji, nchi ambayo 18% ya raia wa nchi hiyo ni waislamu, na linaonekana kuhamasisha operesheni zake ambazo zimekuwa zikiweka alama zake katika maeneo kadhaa barani Afrika.

Uasi katika eneo la Cabo Delgado, ambalo ndio kitovu chake, ni sehemu ya harakati za kundi la IS , limeaminiwa na wanamgambo wenyewe ambao waliapa hadharani kulitumikia mwaka jana.

Uhusiano huu hutoa faida kwa pande zote mbili
Lakini katika video tofauti, iliyosambaa mwaka huu na kusambaa sana kwenye WhatsApp nchini Msumbiji, kiongozi wa wanamgambo alitoa ufafanuzi zaidi juu ya hatua za kikundi hicho.

Wakazi wamelalamika kuhusu kubaguliwa
''Tunadhibiti miji kuonesha kuwa serikali ya leo haina usawa. Inawadhalilisha masikini na kuwapa faida wakuu,'' alisema mwanaume mmoja mrefu, ambaye hakufunika uso wake akiwa amevalia sare za rangi ya kaki, akiwa amezungukwa na wapiganaji wengine.

Alizungumza wakati wote kuhusu uislamu, na shauku yake ya kuwa kwenye ''serikali ya Kiislamu, na si serikali isiyo na watu wasioamini'' lakini pia alieleza kuhusu madai ya unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Msumbiji, na mara kwa mara alisema kuwa serikali ''haitendi haki''.

Wafuatiliaji wa mambo wanasema kuwa kuanza kwa uasi nchini Msumbiji ni sawa na operesheni za uasi za kundi la Boko Haram Kaskazini mwa Nigeria, kikundi ambacho kimekuwa kikitekeleza vitendo vya kigaidi dhidi ya jamii nyingi nchini humo, lakini pia imekuwa chaguo mbadala la vijana wasio na ajira na waliochanganywa na namna hali ya mwenendo mbaya wa maisha na mifumo ya kifisadi.

Wakazi wa Nanduadua wakipita katika eneo lenye mabaki ya msikiti unaodaiwa kuharibiwa na vikosi vya kijeshi vya Msumbiji

CHANZO CHA PICHA,ADRIEN BARBIER

''Kwa mara ya kwanza walizungumza na Umma,'' alisema mwanahistoria nchini Msumbiji, Prof Yusuph Adam, ambaye amesema kuwa video hizo ziliipa ujazo hoja kuwa mgogoro wa Cabo Delgado umechochewa zaidi na masuala ya ndani.

''Jeshi tangu awali ...lilikuwa likiwapiga watu, kuwafunga,, kuwatesa. Kuna hofu miongoni mwa waislamu waishio eneo hilo. Wanatengwa kwa kuwa watu wanawafikiria kuwa wajinga.

''Tatizo ni kuwa kuna kundi la vijana wasio na ajira. Ikiwa tutatatua ...matumizi ya nguvu, rushwa, na ikiwa tutakuwa na mfumo thabiti wa haki nina uhakika tutatatua shida hii haraka,'' amesema Profesa Adam.

Hapo awali serikali ya Msumbiji ilitaka kupunguza uasi huo, na kuwaondoa wanamgambo kwa makosa ya uhalifu, na kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika mkoa huo. Lakini hali hiyo inabadilika.

Baadaye, serikali ilianza kuajiri maafisa wa usalama wa kigeni - inadaiwa kutoka Urusi, Marekani na Afrika Kusini - kusaidia jeshi kumaliza uasi, lakini bila mafanikio yoyote makubwa.

Kuna wasiwasi kuwa mzozo huo, ukishughulikiwa vibaya, unaweza kuenea katika nchi jirani ya Tanzania, na labda hata Afrika Kusini.

Mmiliki wa duka na watoto

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Athari za kiuchumi
Makampuni ya gesi- yamesitisha kuwekeza mabilioni ya fedha katika maeneo ya pwani ya Cabo Delgado - moja ni kwa sababu ya kukosekana kwa hali ya usalama, lakini pia kuporomoka kwa bei ya gesi.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, suluhu ya mgogoro itategemea utawala mzuri na uwazi katika masuala ya uchumi, usawa katika umiliki ardhi, ajira na mgawanyo sawa wa mapato yatokanayo na gesi.

''Makampuni ya kimataifa yanataka kujua kama wanaweza kuchukua hisa zao, lakini wanapaswa kuwaangalia wakazi wa eneo hili,'' alisema askofu wa Pemba.

''Na serikali inapaswa kufahamu kuwa ni muhimu sana kuwa rasilimali hii lazima iwanufaishe watu na isiwe chanzo cha vitendo vya rushwa,'' aliongeza.

BBC Swahili
 
Hao wavaa kobasi wakiingia tu Tz ndiyo itakuwa mwisho wao...sie tuna andaa kundi maalumu la commando wanacheza nao kama wale wa kibiti na ole wako uwe kati ya watu ulio wapokea hapo kijijini utakuwa na wewe ni watu wasio julikana. hiyo operation itakuwa ya nyumba kwa nyumba na kazi inafanyika ucku asubuhi watu wanaendekea na ujenzi wa taifa kama kawaida mbona watarudi tu msumbiji.
 
Ukichunguza kwa ndani sehemu nyingi ambazo hawa IS wameshamiri huwa kuna mkono wa U.S. Wasiwasi wangu tu hili lisijekuwa ni plan ya U.S kuisambaratisha Mozambique na Tz hasa interest ikiwa ni natural gas. Huo ukanda kwa pande zote yaani kaskazini ya Msumbiji na Kusini mwa Tz kuna reserve kubwa ya natural gas.

Hivyo tusilichukulie vyepesi hili hasa kipindi hiki cha chaguzi ambapo mara nyingi vyombo vyote vya usalama macho yanakuwa kwenye hilo tu. Najaribu kufikiria kwa sauti tu
 
Hao USA wasijifanye kujitekenya kisha wanacheka wao wenyewe

Wao ndio wahusika wakubwa sana ambao sana dhamini hivyo vikundi mbali mbali vya ugaidi duniani kwaajili ya kulinda maslahi yao au kupora Mali za taiga Fulani

Kwahiyo waache janja janja ya kujifanya wana Ipa taarifa dunia kuhusu kinachoendelea kule msumbuji wakati waweza kukuta wao ndio wahusika wakuu wa hilo kundi la kigaidi
 
Hao USA wasijifanye kujitekenya kisha wanacheka wao wenyewe

Wao ndio wahusika wakubwa sana ambao sana dhamini hivyo vikundi mbali mbali vya ugaidi duniani kwaajili ya kulinda maslahi yao au kupora Mali za taiga Fulani

Kwahiyo waache janja janja ya kujifanya wana Ipa taarifa dunia kuhusu kinachoendelea kule msumbuji wakati waweza kukuta wao ndio wahusika wakuu wa hilo kundi la kigaidi
'Wao ndio wahusika wakubwa sana ambao sana dhamini hivyo vikundi mbali mbali vya ugaidi duniani kwaajili ya kulinda maslahi yao au kupora Mali za taiga Fulani'.

Imeisha hio mzee baba,naunga mkono hoja.
 
Hao wamarekani Hao wanataka gesi na madin yao mbona waasi siku zote wanaenda sehem zenye Mali?


Pia magaid kuingia Upande wetu sio kazi Rahis mana msitu wote Upande ule wa Tanzania ni kambi za jeshi na hapa Ruhusiw shughul za kijamaa maeneo Yale wakitaka kuingia labda wapitie Dar
 
'Wao ndio wahusika wakubwa sana ambao sana dhamini hivyo vikundi mbali mbali vya ugaidi duniani kwaajili ya kulinda maslahi yao au kupora Mali za taiga Fulani'.

Imeisha hio mzee baba,naunga mkono hoja.
Ahsante mkuu ... Hawa jamaa wanawafanyaga watu misukule sana
 
Dah kwa sababu ya uwepo wa mafuta na gas huko msimbiji si salama Tena, tatizo sio ajira tu, Ila ni makampuni ya ulaya na Marekani kutumia shida za wananchi kuanzisha uasi wao kwa wao ili kujinufaisha kiuchumi kwa rasilimali hizo.. wamarekani tuacheni jamani hatuwataki,,,
Kama ajira hata kwenu hamna
 
Back
Top Bottom