profesawaaganojipya
JF-Expert Member
- Apr 21, 2015
- 1,484
- 3,127
Russia imetumia kombora la kisasa kabisa lisilozuilika la hypersonic, kuharibu ghala la silaha nchini Ukraine.
USA NA NATO hawana mfumo wa kuweza kulizuia au kuliangusha kombora hilo, NATO wote tumbo joto, USA anajipendekeza kwa mchina ili amgeuke Russia, na Mchina kakomaa na swahiba wake Russia.
====
Waziri wa Ulinzi wa Urusi amethibitisha kuwa nchi yake imetumia bomu hatari la hypersonic kwa mara ya kwanza kulishambulia na kuliteketeza ghala la silaha nchini Ukraine.
Bomu aina ya Hypersonic lina uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilomita 4,900 kwa saa na kuongeza kasi hadi kufikia kilomita 12,350 kwa saa, likiwa pia na uwezo wa kubeba kichwa cha mzinga wa nyuklia chenye uzito wa kilo 480 ambayo ni mara 33 ya bomu lililoshushwa na Marekani katika ardhi ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Putin amelielezea bomu hilo kama silaha muhimu kwenye mapigano na kuinadi kuwa inaweza kusafiri mara kumi zaidi ya spidi ya sauti na kwamba hakuna nchi ya Magharibi hata moja yenye teknolojia ya kuzuia bomu hilo kupitia mfumo wa usalama wa anga.
Bomu hilo lina uwezo wa kusafiri umbali (range) wa kilometa takribani 2011 huku likiwa na uwezo wa kusababisha madhara makubwa mahali litakapotua ambapo kwa miaka mingi, Urusi imekuwa ikipinga matumizi ya silaha za masafa marefu aina ya hypersonic.
Meja Jenerali wa jeshi la Urusi, Igo Konashenkov amesema licha ya bomu hilo, Urusi pia ilitumia makombora kusambaratisha ngome ya majeshi ya Ukraine iliyopo karibu na bandari ya bahari nyeusi ya Odesa.
Naye msemaji wa vikosi vya anga vya majeshi ya Ukraine Yuri Ignat amethibitisha kuwa ni kweli ngome yao imeshambuliwa lakini hakuwa na taarifa ni aina gani ya makombora yalitumika kushambulia eneo hilo.
Global Publishers