Urusi yaionya Marekani juu ya kuishambulia Syria

Urusi yaionya Marekani juu ya kuishambulia Syria

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Russia yaionya tena Marekani juu ya kufanya shambulizi dhidi ya Syria
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameelezea uwezekano wa Marekani na washirika wake kufanya shambulizi dhidi ya Syria hasa kwa kuzingatia hatua ya kusogezwa zana za kijeshi za nch hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati.
Maria Zakharova ameyasema hayo Alkhamisi ya leo ambapo ameashiria njama za muungano vamizi wa Magharibi unaoongozwa na Marekani kwa ajili ya kufanya mashambulizi mapya dhidi ya Syria na kuonya kuhusu hatma mbaya ya hujuma hiyo.
Amesema kuwa, hatua ya kusogezwa zana za kijeshi katika eneo hilo ina maana kwamba, Washington na washirika wake wanaweza kufanya shambulizi dhidi ya Syria ndani ya kipindi cha masaa 24 yajayo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia sambamba na kueleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa kukaririwa mchezo mchafu na wa kichochezi kwa kutumia madai bandia ya silaha za kemikali kama wenzo wa kuishambulia Syria, amesema kuwa, shambulizi kama hilo litakuwa pigo zito kwa juhudi za utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo na hata amani ya duniani. Maria Zakharova amesisitiza kuwa ni vigumu kutabiri hatma ya kuchezea moto.
Siku chache zilizopita pia, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilionya kwamba Marekani imeimarisha zana zake za kijeshi karibu na Syria na kwamba hatua hiyo inakusudia kufanya shambulizi dhidi ya jeshi la serikali ya Damascus kwa kisingizio cha shambulizi bandia la silaha za kemikali.
4bn06eb799e510uhko_800C450.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urusi wanajitahidi sana kuepusha vita mbaya lakini Marekani na washirika wake wanaonekana kuilazimisha vita hiyo!
 
Hawa wakubwa wanapigana kwenye ardhi za wengine halafu raia wao hawana muda kufuatilia ushabiki huu, wanachapa kazi na wana hela za kutosha.

Sisi huku walala ulimi nje tunafuatilia daily
 
Huyo mwanamke anamjua Trump vizuri?

Huyu ni Maria Zakharova (naweza kuwa nimekosea spelling hapa, )..ni mwanamke wa shoka..ndiye msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Russia...very intelligent woman....ni star wa Urusi..very famous...anakula sahani moja na mastaa wa Marekani..a beautiful woman and intelligent....anajua issues nyingi ..well informed...and knowlegeable
 
Upo sawa kbs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Russia, China, USA, na mataifa mengine yenye nguvu wanajua wanachokifanya, wanaigiza na kuleta maafa kwa mataifa dhaifu, hawatapigana vita wao kwa wao, huruma kwa watu wa SYRIA
 
Back
Top Bottom