Urusi yafunga bomba kuu la gesi kwenda Ulaya

Urusi yafunga bomba kuu la gesi kwenda Ulaya

Jamani ulaya waache kuwa tegemezi watafute alternative ata kutumia moto wa solar
 
Kampuni kubwa ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Urusi, Gazprom, imesema vikwazo katika bomba la Nord Stream 1 vitadumu kwa siku tatu zijazo.

Urusi tayari imepunguza mauzo ya gesi kwa kiasi kikubwa kupitia bomba hilo.

Lakini inakanusha shutuma za kutumia nishati kama njia ya kuadhibu mataifa ya Magharibi kwa kuiwekea vikwazo kutokana na uvamizi wa Ukraine.

Bomba la Nord Stream 1 lina urefu wa kilomita 1,200 (maili 745) chini ya Bahari ya Baltic kutoka pwani ya Urusi karibu na St Petersburg hadi kaskazini-mashariki mwa Ujerumani.

Ilifunguliwa mnamo 2011, na inaweza kutuma kiwango cha juu cha mita za ujazo 170 za gesi kwa siku kutoka Urusi hadi Ujerumani.

Bomba hilo lilifungwa kwa siku 10 mwezi Julai - tena kwa ajili ya kufanyiwa maboresho, kulingana na Urusi - na hivi karibuni limekuwa likifanya kazi kwa uwezo wa 20% tu kwa sababu ya kile Urusi inaelezea kama vifaa vibovu.

Rais wa mdhibiti wa mtandao wa Ujerumani amesema nchi hiyo itaweza kukabiliana na hali hiyo - ikiwa Urusi itarejelea utoaji katika siku zijazo.

‘’Nadhani tutaweza kukabiliana nayo’’, Klaus Mueller aliambia Reuters.

‘’Nina imani kuwa Urusi itarejea hadi 20% Jumamosi, lakini hakuna anayeweza kusema.’’

Viongozi wa Ulaya wanahofia kwamba Urusi inaweza kuongeza muda wa kukatiza usambazaji wa gesi hiyo katika jaribio la kuongeza bei ya gesi, ambayo tayari imeongezeka kwa kasi mwaka uliopita.

Kupanda kwa bei kunatishia kuongeza gharama ya maisha katika miezi ya msimu wa baridi, ambayo inaweza kulazimisha serikali kutumia mabilioni ili kupunguza mzigo kwa wananchi.

Siku ya Jumanne, Waziri wa Mpito wa Nishati wa Ufaransa Agnes Pannier-Runacher aliishutumu Urusi kwa ‘’kutumia gesi kama silaha ya vita’’.

Alikuwa akizungumza baada ya Gazprom kusema kuwa itasitisha utoaji wa gesi kwa kampuni ya nishati ya Ufaransa ya Engie.

Lakini msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin amekataa shutuma hizo - na kusisitiza kwamba vikwazo vya Magharibi vimesababisha usumbufu huo kwa kuharibu miundombinu ya Urusi.

Alisisitiza kwamba ‘’matatizo ya kiteknolojia’’ yanayosababishwa na vikwazo ndiyo kitu pekee kinachozuia Urusi kusambaza gesi kupitia bomba hilo, bila kutaja shida ni nini.

Mzozo wa hivi majuzi zaidi umekuwa juu ya magurudumu yaliyowasili Ujerumani baada ya kukarabatiwa huko Canada na ambayo Urusi ilikataa kuchukua tena, ikisema kuwa ilikuwa chini ya vikwazo vya Magharibi.

Ujerumani, hata hivyo, inakanusha hili.

Mapema mwezi huu, Waziri wa Uchumi Robert Habeck alisema bomba hilo lilikuwa likifanya kazi kikamilifu na kusema hakuna masuala ya kiufundi kama inavyodaiwa na Urusi.

Mapema wiki hii, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen aliahidi kuingilia kati katika masoko ya nishati, akiuambia mkutano huko Slovenia kwamba ‘’hawafai tena kwa malengo yaliyopo’’.

‘’Tunahitaji mfumo mpya wa soko la umeme ambao unafanya kazi kweli na kuturudisha katika usawa,’’ alisema.

Kabla ya mzozo huo, Ujerumani ilikuwa imeidhinisha bomba la €10bn (£8.4bn) la Nord Stream 2 - ambalo linakwenda sambamba na jingine lenye jina kama lake - lakini ilisimamisha shughuli zake baada ya Urusi kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine mwezi Februari.

Wiki iliyopita, BBC ilifichua kuwa Urusi imekuwa ikiteketeza gesi inayokadiriwa kufikia $10m (£8.4m) kila siku kwenye kiwanda karibu na mpaka wa Finland.

====
Kikubwa ni kwamba wote wataathirika
 
Putin anapeleka Moto hatari.
Wee mpelekee Moto ..peleka Moto, mpelekee Moto..
 
Jamani ulaya waache kuwa tegemezi watafute alternative ata kutumia moto wa solar
Mkuu, Ulaya wanajitahidi kutafuta nishati mbadala. Wameshaanza kutumia kuni.
 
Hii habari mbona imetoka BBC? Kwahiyo sio Propaganda?
 
Pedeshee Mangi
JamiiForums-1471852001.jpg


Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Former Ukrainian lawmaker Oleksiy Kovalyov, who joined the Russia-imposed Kherson regional government after Russian armed forces took over parts of Ukraine's southeast, has been found dead.

An adviser to the Kyiv-controlled regional administration, Serhiy Khlan, said on August 29 that Kovalyov was found dead a day earlier in his house in the town of Hola Prystan.

Ukrainian media reports said Kovalyov was found with a gunshot wound to his head and a Mossberg pump firearm that was officially registered to the former member of Ukraine's ruling Servant of the People party. The reports also said Kovalyov's girlfriend sustained a stabbing wound and was hospitalized.

Russia-imposed authorities did not comment on the reports, but pro-Russian Telegram channels confirmed them.
 
So what?!.... Wewe unanufaika na nn? Nyau wahed
Mbona kama unapanik na mitusi juu, kwani we ni mzungu 🤣🤣😂 maskini wa akili hala jirani m23 wanasumbua DRC na husikitiki, msumbiji wanasumbuliwa na magaidi hujawahi kulaani?

Ila kwa kuwa wazungu unajifanya unaumia saana ACHA UNAFKI!!!😡😡😡😡
 
Back
Top Bottom