Urusi:Watatu wauawa katika shambulio la ndege za kivita za Ukraine

Urusi:Watatu wauawa katika shambulio la ndege za kivita za Ukraine

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Watu watatu wameuawa na 35 kupelekwa hospitali kufuatia shambulio la Ukraine kwenye kiwanda kimoja katika mji wa Izhevsk - zaidi ya kilomita 1,000 kutoka mpakani, mamlaka ya Urusi inasema.
Kati ya wale waliojeruhiwa kumi wamepata majeraha mabaya, gavana wa Udmurtia Aleksandr Brechalov alisema, akiongeza kuwa alikuwa amemjulisha Rais Vladimir Putin juu ya shambulio hilo.
Ndege zisizo na rubani ziliripotiwa kulenga Kiwanda cha Kupol Electromechanical - kiwanda cha kijeshi ambacho kinasemekana kuzalisha mifumo ya makombora ya Tor kutoka ardhini hadi angani na vituo vya rada.
Kiwanda hicho pia kinajishughulisha na utengenezaji wa mifumo ya ulinzi wa anga ya Osa na kimetengeneza ndege zisizo na rubani, kulingana na vyombo vya habari vya Ukraine.
 
Wapimzike kwa amani Marehemu wote wana Russia,na wapate nafuu soon Majeruhi wote.
 
Back
Top Bottom