Urusi kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani

Urusi kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
  • _96886435_usarusleadersreut7jul.jpg

Urusi iko tayari kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani na kutwa mali ya Marekani kujibu vikwazo vya Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Urusi. Vitisho hivyo vinatolewa kutoka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Urusi na kunukuliwa na gazeti la daily Izvesta.

Mwezi Disemba utawala wa Obama uliwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi na kufunga makao mawili ya kijasusi. Hatua hizo ni jibu kwa madai ya kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani. Urusi tayari iko chini ya vikwazo vya Marekani.

Timu ya Trumo hayo iko chini ya uchunguzi kufuatia madai ya Urusi kuingia kati kampeni ya mwaka uliopita. Hata hivyo Urusi imekana madai hayo.


Chanzo: bbc swahili
 

_96886435_usarusleadersreut7jul.jpg
​

Urusi iko tayari kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani na kutwa mali ya Marekani kujibu vikwazo vya Marekani, kwa mujibu wa maafisa wa Urusi.

Vitisho hivyo vinatolewa kutoka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Urusi na kunukuliwa na gazeti la daily Izvesta.

Mwezi Disemba utawala wa Obama uliwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi na kufunga makao mawili ya kijasusi.

Hatua hizo ni jibu kwa madai ya kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.

Urusi tayarai iko chini ya vikwazo vya Marekani.

Timu ya Trumo hayo iko chini ya uchunguzi kufuatia madai ya Urusi kuingia kati kampeni ya mwaka uliopita. Hata hivyo Urusi imekana madai hayo.

Chanzo: BBC
 
Hii inaitwa mwaga mboga nimwage ugali.....

Ngoma droo.

maana huu mchezo alouanza ni USA mwenyewe so akifanyacho rusia ni kuendeleza gemu tu


Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app
 
Hii inaitwa mwaga mboga nimwage ugali.....

Ngoma droo.

maana huu mchezo alouanza ni USA mwenyewe so akifanyacho rusia ni kuendeleza gemu tu


Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app


Teh!, hawa wawili kama simba na yanga vile..
 
Hahahahaha..... Km nani na nani vile?

Hawa jamaa kila siku wanatunishiana misuli lkn cha kushangaza hawazichapi, sijui wanaogopana!!!?

Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app


Huh!, nimewaza hivyo, wanatunishiana misuli si kidogo lakini sidhani kama watakuja kuzichapa asee..
 
Kulikoni mkutano wa juzi wa Trump na Putin!, yamekuwa haya?
Unakumbuka nilishawah kukwambia kwamba Marekani hawana ONE MAN SHOW, yani hata kama Trump alielewana na Putin bila Congress kukubali kuondoa hvyo vikwazo ni kaz bure na pia kumbuka wajumbe wa Congress wanaichukia sana Urusi mfano hapa majuzi waliisingizia tena Urusi ilijaribu kudukua vinu vya nyuklia vya Marekani
 
Teh!, nimewaza hivyo, wanatunishiana misuli si kidogo lakini sidhani kama watakuja kuzichapa asee..
Acheni masihara kabisa huyu USA ni zaidi ya shetani yaan anaziburuza nchi zilizo against atakavyo.

Yaan km hujipendi bhasi mpinge USA , utapigwa vikwazo hadi unyooke.

Iran kachezea vikwazo hadi akili imemkaa sawa now.

Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app
 
Unakumbuka nilishawah kukwambia kwamba Marekani hawana ONE MAN SHOW, yani hata kama Trump alielewana na Putin bila Congress kukubali kuondoa hvyo vikwazo ni kaz bure na pia kumbuka wajumbe wa Congress wanaichukia sana Urusi mfano hapa majuzi waliisingizia tena Urusi ilijaribu kudukua vinu vya nyuklia vya Marekani


Yeah!, halafu hayo mazungumzo hayakufurahiwa na baadhi yao walioona kama Trump amekubaliana na Putin kiaina, na watambana kwenye floor ya Congress.

Kha!, walisema mpaka Mrusi kajaribu kudukua vinu vya nyuklia?!!..wow!
 
Acheni masihara kabisa huyu USA ni zaidi ya shetani yaan anaziburuza nchi zilizo against atakavyo.

Yaan km hujipendi bhasi mpinge USA , utapigwa vikwazo hadi unyooke.

Iran kachezea vikwazo hadi akili imemkaa sawa now.

Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app


Acha tu, inabidi wakubaliane lakini wamemkuta Putin sikio la kufa..
Sijui kama ataachia Cremea?
Halafu mfumo wa uongozi wa US ulivyo, Trump pamoja kutaka kwake kuwa karibu na Putin na kumuondolea vikwazo lakini bado anabanwa.
 
Yeah!, halafu hayo mazungumzo hayakufurahiwa na baadhi yao walioona kama Trump amekubaliana na Putin kiaina, na watambana kwenye floor ya Congress.

Kha!, walisema mpaka Mrusi kajaribu kudukua vinu vya nyuklia?!!..wow!
Yah.... Nakumbuka ni last week walisema kuna udukuzi kwenye vinu vya nyuklia vinavyozalisha umeme ambao wanahisi hacker ni Urusi maana eti njia iliyotumika kudukua inafanana na ile iliyotumika kuhack uchaguzi.
Yani sasa hv hata ndege ikianguka Marekani mtuhumiwa wa kwanza ni Russia.
 
Vikwazo vigumu sana hata ujifanye kidume siku wakiviondia ndio utaona mtu anavyopumua
Usicheze na vikwazo aseeee... Embu angalia Zimbabwe ilivyo mpaka wanatumia dollar kama fedha yao ya nchi.

Ukitaka kujua vikwazo vinaumiza angalia siku Iran na Cuba walivyoondolewa vikwazo jinsi wanamchi wake walivyokua wakishangilia mabarabarani.
 
Back
Top Bottom