Urusi: Kuna uwezekano Marekani ikaishambulia Kijeshi Venezuela

Urusi: Kuna uwezekano Marekani ikaishambulia Kijeshi Venezuela

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Kuna uwekezano Marekani ikaishambulia kijeshi Venezuela. Balozi wa Russia nchini Venezuela ameonyesha masikitiko yake kutokana na uwezekano wa Marekani kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo

Vladimir Zamsky, ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la Sputnik na kuongeza kuwa, kwa kuzingatia tajriba ya utendajikazi wake, Marekani imeendelea kusisitiza machaguo kadhaa, likiwemo chaguo la kijeshi dhidi ya Venezuela.

Mwanadiplomasia huyo wa Russia amebainisha kwamba, suala hilo ni hatari kubwa hususan kwamba Marekani imekuwa ikizungumzia stratijia ambayo inasisitiza kuyaacha wazi maeneo yote ya kusini mwa Marekani. Hayo yanajiri katika hali ambayo hivi karibuni Rais Nicolás Maduro wa Venezuela alilitaka jeshi la nchi hiyo kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na hujuma tarajiwa za Marekani dhidi ya nchi hiyo

Maduro alitoa indhari hiyo kwa jeshi la nchi yake kufuatia habari na ripoti zilizotolewa nchini Marekani kwamba, mwaka jana wa 2017 Rais Donald Trump wa nchi hiyo alikuwa na mpango wa kutaka kuishambulia kijeshi Venezuela.

Tarehe 11 Agosti mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika jimbo la New Jersey, alinukuliwa akisema kuwa kuna uwezekano wa Marekani kuishambulia kijeshi Venezuela, matamshi ambayo yaliwakasirisha mno viongozi wa Caracas.
 
Urusi imsaidie mshirika wake venezuela basi na ninafasi ya kumdhoofisha marekani the same us ilivyokua yatokee cuba.
 
Marekani visima vyake vya mafuta vitakuwa vinahitaji mafuta... ni lazma waivamie wakaibe wese pale
Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuzalisha mafuta duniani hivyo sidhani kama anahitaji kuiba mafuta Venezuela,
Ila anataka kuvamia kule kwasababu nyingine ambazo Lex Tillerson alizitoa kipindi kile katembelea America Kusini....
 
Urusi imsaidie mshirika wake venezuela basi na ninafasi ya kumdhoofisha marekani the same us ilivyokua yatokee cuba.
The Munroe Doctrine mzee; The Munroe Doctrine!
Ndicho kinafanya mataifa mengi yafikiri mara mbili kabla ya kwenda Amerika Kusini.
Hata hivyo siku hizi Urusi hana ushawishi mkubwa kule Latin America kama ambavyo Uchina anao.
 
Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuzalisha mafuta duniani hivyo sidhani kama anahitaji kuiba mafuta Venezuela,
Ila anataka kuvamia kule kwasababu nyingine ambazo Lex Tillerson alizitoa kipindi kile katembelea America Kusini....
Marekani anaenda kuiba mafuta, wacha watengeneze sababu za kuivamia..

Marekani siyo mzalishaji mkubwa wa mafuta, shehena ya mafuta aliyo nayo Marekani ni ya wizi

Hivi Marekani yupo OPEC kama ndiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta?
 
Dili la kuuza silaha hilo+kummaliza adui. Naamini iwapo vita ikipigwa basi marekani atakua na wakati mgumu sana tena na walivyo karibu mhhh. Uwepo wa china sidhani kama una madhara na iwapo akiisapoti venezuela basi lazima ashuke kiuchumi maana marekani kawekeza biashara kubwa sana china pamoja na makampuni binafsi kibao ya kimarekani kitu ambacho najua china hawezi kifanya.
 
Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuzalisha mafuta duniani hivyo sidhani kama anahitaji kuiba mafuta Venezuela,
Ila anataka kuvamia kule kwasababu nyingine ambazo Lex Tillerson alizitoa kipindi kile katembelea America Kusini....
Weee kule Libya anafanya nini na washirika wake?
 
Marekani anaenda kuiba mafuta, wacha watengeneze sababu za kuivamia..

Marekani siyo mzalishaji mkubwa wa mafuta, shehena ya mafuta aliyo nayo Marekani ni ya wizi

Hivi Marekani yupo OPEC kama ndiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta?
Usa ni mzalishaji mkubwa wa mafuta hata kama haongozi ila wanazalisha mafuta kuzidi Venezuela. Halafu kwanini waibe mafuta Venezuela wakati nchi zenye mafuta mengi karibu zote ni marafiki wa marekani. Qatar, saudia, canada. Kama wanashida ya mafuta wanaweza kuchukua kiurahisi tu.
 
Nicolas maduro ni juha mpumbavu
Kaitoa Venezuela toka nchi taji iliostawi Mpaka nchi maskini kuliko Colombia.
Ameua na kufunga wapinzani
Ameitisha uchaguz akagombea mwenyewe kama jiwe
Trump atakuwa kafanya jambo la msingi kumchapa maduro
 
US anapenda sana ubabe,duniani nasi tunaishi kama wanyama porini aidha uwinde au uwindwe
Nalog off
 
Nicolas maduro ni **** mpumbavu
Kaitoa Venezuela toka nchi taji iliostawi Mpaka nchi maskini kuliko Colombia.
Ameua na kufunga wapinzani
Ameitisha uchaguz akagombea mwenyewe kama jiwe
Trump atakuwa kafanya jambo la msingi kumchapa maduro
Kama ndiyo kafanya hivyo basi apigwe kama mbwakoko. Demokrasia ni moja ya kitu bora kabisa kuwahi kutokea kwa mwanadamu, yeyote anayeipinga na kuikandamiza ni adui wa ubinadamu. Braza Malcom Lumumba unamtetea mtu wa hivi?🙂
 
Usa ni mzalishaji mkubwa wa mafuta hata kama haongozi ila wanazalisha mafuta kuzidi Venezuela. Halafu kwanini waibe mafuta Venezuela wakati nchi zenye mafuta mengi karibu zote ni marafiki wa marekani. Qatar, saudia, canada. Kama wanashida ya mafuta wanaweza kuchukua kiurahisi tu.
venezuela ina mafuta mengi ardhini kuliko nchi yoyote duniani
 
Back
Top Bottom