Urusi imeunda Kombora jipya lisiloweza kutunguliwa na linafika popote Duniani

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.

Bw Putin amekuwa akieleza sera zake muhimu za muhula wa nne, taifa hilo linapokaribia kufanya uchaguzi katika siku 17.

Rais huyo anatarajiwa kushinda.

Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale. Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo."

Katika nusu ya kwanza ya hotuba hiyo yake kwa taifa, ameahidi kupunguza viwango vya umaskini nchini humo.

Kisha, ameonesha mkusanyiko wa silaha mpya, likiwemo kombora alilosema linaweza "kufika pahala popote duniani".

Hotuba hiyo ya Bw Putin imeendelea kwa saa mbili.

Uchaguzi utafanyika mnamo 18 Machi.

Kiongozi huyo anakabiliwa na wapinzani saba, lakini hakuna mmoja kati ya hao anayetarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwake.

Rais huyo hakushiriki katika mdahalo wa wagombea uliooneshwa moja kwa moja kwenye runinga Jumatano na kuwashirikisha wagombea hao wengine.

Kiongozi wa upinzani Alexei Navalny hajakuwa akifanya kampeni.

Amezuiwa kuwania na ametoa wito kwa wapiga kura wanaomuunga mkono kususia uchaguzi huo.

Rais Putin hajafanya kampeni sana na kufikia sasa alikuwa hajazungumzia sana mipamngo yake ya miaka sita ijayo.

Huku akitumia skrini kubwa, ameonyesha video za alichosema ni kombora jipya la Urusi.

Amesema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga ya makombora wa Marekani barani Ulaya na Asia.

Kadhalika, ameonesha video ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.

Kwenye hotuba hiyo yake kwa kikao cha pamoja cha mabunge mawili, amewahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha.

Ulinzi
Putin amesema uwezo wa kijeshi wa Urusi umepangwa na kustawishwa kwa lengo la kudumisha amani duniani.

Hata hivyo, amesema iwapo mtu yeyote yule atathubutu kurusha silaha za nyuklia dhidi ya Urusi, atajibiwa mara moja.

Operesheni ya kijeshi ya Urusi Syria, ambapo anasaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad dhidi ya waasi na amesema hiyo inadhihirisha kuimarika kwa uwezo wa Urusi katika kujilinda.

Amesema pia kwamba daraja la kuunganisha Urusi na rasi ya Crimea litafunguliwa miezi michache ijayo.

Urusi iliteka Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 wakati wa muhula wa sasa wa Bw Putin.

Kiongoiz huyo amesema Urusi inalinda maslahi yake katika eneo la Arctic kwa kuimarisha miundo mbinu yake ya kijeshi eneo hilo.

Chanzo: BBC
 
Putin aache tambo nyingi utafikiri mswahili, ajenge uchumi kwanza ndio wenzake walivyofanya.

Huwezi kwenda vitani kupigana na matajiri wakati wewe theluthi moja ya watu wako wanaishi chini ya dola tatu kwa siku na ndio maana wananchi wengi wanamshinikiza aondoe wanajeshi Syria.
 
skynews-vladimir-putin-russia_4243765.jpg

Rais Vladimir Putin amesema Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani.

"Halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale."- Putin.

=====

Russia is developing new nuclear weapons that are immune to enemy interception, Vladimir Putin has claimed.

In comments that are likely to ratchet up tensions with the US, the Russian President said this includes a nuclear-powered cruise missile and an underwater drone.

Speaking in a state-of-the-nation speech, Mr Putin warned that Moscow would regard a nuclear attack on its allies as an attack on Russia itself and would respond swiftly.

"We would consider any use of nuclear weapons against Russia or its allies to be a nuclear attack on our country. The response would be immediate," he told the audience of Russian politicians and senior officials.

Mr Putin said the weapons made NATO's US-led missile defence system "useless" and signalled the end to Western efforts to check Russia's nuclear ambitions.

"I want to tell all those who have fuelled the arms race over the last 15 years, sought to win unilateral advantages over Russia, introduced unlawful sanctions aimed to contain our country's development: all what you wanted to impede with your policies have already happened," Mr Putin said.

"You have failed to contain Russia."

He said the development of the new weapons was in response to the US withdrawing from a Cold War-era treaty that banned missile defences and Washington's moves to develop a missile defence system.

Source: SkyNews
 
Hawa jamaa wakorofi sana tena wakiongozwa na Rais wao, hawajaanza leo....ni tangu enzi za USSR wakati huo hata USA haifahamiki sana kidola.

Inashangaza tu kuwa huyu anachukia Ugaidi lakini ni dam dam na Waarabu na alishakiri kuwa Assad ni Rafiki yake wa karibu.
 
Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.

Bw Putin amekuwa akieleza sera zake muhimu za muhula wa nne, taifa hilo linapokaribia kufanya uchaguzi katika siku 17.

Rais huyo anatarajiwa kushinda.

Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale. Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo."

Katika nusu ya kwanza ya hotuba hiyo yake kwa taifa, ameahidi kupunguza viwango vya umaskini nchini humo.

Kisha, ameonesha mkusanyiko wa silaha mpya, likiwemo kombora alilosema linaweza "kufika pahala popote duniani".

Hotuba hiyo ya Bw Putin imeendelea kwa saa mbili.

Uchaguzi utafanyika mnamo 18 Machi.

Kiongozi huyo anakabiliwa na wapinzani saba, lakini hakuna mmoja kati ya hao anayetarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwake.

Rais huyo hakushiriki katika mdahalo wa wagombea uliooneshwa moja kwa moja kwenye runinga Jumatano na kuwashirikisha wagombea hao wengine.

Kiongozi wa upinzani Alexei Navalny hajakuwa akifanya kampeni.

Amezuiwa kuwania na ametoa wito kwa wapiga kura wanaomuunga mkono kususia uchaguzi huo.

Rais Putin hajafanya kampeni sana na kufikia sasa alikuwa hajazungumzia sana mipamngo yake ya miaka sita ijayo.

Huku akitumia skrini kubwa, ameonyesha video za alichosema ni kombora jipya la Urusi.

Amesema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga ya makombora wa Marekani barani Ulaya na Asia.

Kadhalika, ameonesha video ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.

Kwenye hotuba hiyo yake kwa kikao cha pamoja cha mabunge mawili, amewahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha.

Ulinzi
Putin amesema uwezo wa kijeshi wa Urusi umepangwa na kustawishwa kwa lengo la kudumisha amani duniani.

Hata hivyo, amesema iwapo mtu yeyote yule atathubutu kurusha silaha za nyuklia dhidi ya Urusi, atajibiwa mara moja.

Operesheni ya kijeshi ya Urusi Syria, ambapo anasaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad dhidi ya waasi na amesema hiyo inadhihirisha kuimarika kwa uwezo wa Urusi katika kujilinda.

Amesema pia kwamba daraja la kuunganisha Urusi na rasi ya Crimea litafunguliwa miezi michache ijayo.

Urusi iliteka Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 wakati wa muhula wa sasa wa Bw Putin.

Kiongoiz huyo amesema Urusi inalinda maslahi yake katika eneo la Arctic kwa kuimarisha miundo mbinu yake ya kijeshi eneo hilo.

Chanzo: BBC
Hawa viongozi wenye mawazo ya kikomonisti hawaeleweki, kama nafanya vizuri sana kwanini anafunga viongozi wa upinzani na kuwazuia kupiga kampeni? na kwanini bado wananchi wengi ni masikini na walevi wakupindukia?
 
Hakuna kombora ambalo haliwezi kudunguliwa Duniani bado halijatokea,je wenzake wakiliwahi pale punde linapotoka kwenye launcher na kudunguliwa si tayari linakua limedunguliwa
Mkuu umeona jinsi huyo mridhi wa Saturn alivyo na speed na anavyo badilika kwa kwa kugawanyika dah kweli wezetu wapo mbali sisi bado tupo tuna nunuwa nunuwa akina mtulia!!
 
Back
Top Bottom