urithi wa matatizo na matabaka yetu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

urithi wa matatizo na matabaka yetu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by opwa, Jul 18, 2011.

 1. opwa

  opwa Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikiikumbuka historia na siasa nilizosoma shule ya msingi zilinifunza kukarimia shida hata kama zinatesa, pia nilijifunza na kuaminishwa kuwa viongozi wa serikali ndo wakuheshimiwa, hivyo nikapelekwa barabarani kupunga mkono hata kama anaepita ni mbunge wa jimbo lingine, nimerisishwa woga wa kudai haki zangu za msingi kwa kunionesha polisi wanaozurura barabara na silaha zao. Hata nyumbani baba alinionyesha baiskeli (chang shung) kuwa ndo urithi wangu, sikuwaza kuwa itakuwa sio baskeli tena enzi nikiwa mkubwa.
  Leo nimekua nayoyashuhudia ni urithi wa matatizo tuliobebeshwa tangu utotoni. Watanzania leo tupo katika matabaka si ya kidini, ukwasi na makabila pekee bali hata utaifa nchi sasa inaongozwa na wahamiaji. Nchi ina
  1.wananchi na walanchi
  2.walala hai, walala hoi na walala heri
  3.watanganyika na wadanganyika.

  Haya yanatuweka hivi milele kwani mawazo ya viongoz wetu japo ni mgando bali ni ya kibinafsi tena.
   
Loading...