Urithi wa Karume Licha ya kuondoka fikra zake zinawaongoza Wazanzibari

Apr 4, 2020
16
7
1586408844005.png

IMETIMIA miaka 48 sasa tangu muasisi wa taifa la Zanzibar Abeid Amani Karume, kuuawa kikatili na wapinga maendeleo mnamo Aprili 7, 1972.

Wanaopinga maendeleo walimshambulia Karume na kumua akiwa kwenye makao makuu ya chama kilicholeta uhuru cha ASP ofisi ya Kisiwandui.

Tamko la Baraza la Mapinduzi mwaka 1972 liliweka bayana kwamba ''hayati Abeid Amani Karume, ameuawa na kuzikwa lakini kilichokufa ni kiwiliwili chake tu . Mawazo busara na mambo yote mema hasa ya kumuenzi Mzanzibari na kumletea maisha bora yataendelea kulindwa na kuenziwa kwa faida ya wananchi wote wa vizazi vilivyokuwepo na vijavyo.

Zanzibar itaendesha kisomo cha kumkumbuka Mzee Karume na kwamba hakitakuwa na watu wengi kama ilivyozoeleka katika miaka iliyopita kutokana na ugonjwa corona. Licha ya Karume kuondoka taifa limeendelea kushuhudia awamu mbali mbali za marais wakiongoza Zanzibar wakiendelea kufuata nyayo na kuyalinda yale mambo yote ya msingi yaliyoanzishwa na kiongozi huyo.

Zanzibar inatajwa kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo katika Bara la Afrika kutekeleza kwa vitendo maazimio na matamko ya jumuiya za kimataifa yanayohusu haki za binadamu na utawala bora mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964.

Hata, katika tamko lake la mwanzo mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964, lililotangazwa na Jemedari Karume aliuhakikishia umma kuwa Zanzibar itaongozwa kwa misingi ya kulinda utu wa binadamu na kuwajali wazee pamoja na watoto yatima.

Hatua, hiyo ilikwenda sambamba na kuundwa kwa wizara inayoshughulikia haki za wananchi pamoja na kujenga nyumba za kuhifadhi wazee na wasiojiweza ziliopo Sebuleni mjini Unguja.

Ndivyo anavyosema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, akitaja Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964, yaliyoongozwa na hayati Abeid Amani Karume, kuwa ndiyo yanayoweka sawa utekelezaji wa haki za binadamu ambapo makundi yote ya vijana,wazee na watoto yalitambuliwa rasmi na kupewa huduma na serikali.

Anasema wizara hiyo na taasisi wadau zinaendelea kutekeleza mambo yote ya msingi yaliyoasisiwa na Karume kwa vitendo. Anaeleza kuwa Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu wa Uchumi (Zaeca) kwa kiasi kikubwa imeweka misingi ya kupambana na ufisadi kwa viongozi waliokabidhiwa majukumu ikiwamo serikali na taasisi za umma.

Anaeleza kuwa rushwa ni adui wa haki na sehemu ambayo rushwa imetawala, watu wa kawaida na kusababisha wanyonge kunyimwa nafasi ya kupata mambo ya msingi wanayostahiki zikiwamo huduma za lazima.

KUBANA MAFISAD
I ''Tumepiga hatua kubwa katika kupambana na rushwa na uhujumu wa uchumi katika sehemu za utoaji wa huduma...tunawataka watu kutoa taarifa za rushwa ili tuwachukulie hatua za kisheria','anasema Suleiman. Anakumbusha kuwa hayati Karume alichukizwa na vitendo vya matajiri kuwakopesha fedha wananchi wanyonge na kuwatoza riba kubwa na hivyo kuwaweka katika maisha magumu. ''Mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12, Karume alipiga marufuku matajiri kuwatoza fedha wananchi wanyonge katika mfumo wa riba pamoja na rehani,'' anasema Suleiman.

Waziri huyu anakumbusha kuwa mara moja baada ya mapinduzi Karume alianzisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kumteua Mohamed Aboud, kuiongoza na baadaye, kiongozi huyo alikuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Tanzania Bara, akiwa ndiye mzalendo wa kwanza kufanya kazi hiyo baada ya kuondoka kwa mzungu.

Aidha, Suleiman anasema kwa upande wa watumishi wa umma,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haipo nyuma kutekeleza yale yote yaliyoasisiwa na rais wa kwanza katika kujali watumishi wake. Suleiman anasema Karume alikuwa akisema siku zote kwamba tumefanya mapinduzi kwa ajili ya wananchi walio wengi kushika hatamu ya kuongoza taifa lao.

''Sisi wazee tunampongeza kwa dhati Rais Shein kwa kuanzisha pensheni jamii na kuwapatia wazee Shilingi 20,000 kila mwezi bila ya ubaguzi. Hatua hiyo ni sawa na kufuata nyayo za Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Amani Karume za kuyalinda Mapinduzi na kuwaenzi wazee,''anaongeza Forouz.
 
Back
Top Bottom