Urithi wa Babu

Urithi wa Babu

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,367
Reaction score
55,054
Ilipofika mwezi pacha zenye Babu aliyaona mengi katika uso wa Dunia tena baadhi ya yale aliyoyaona yalimtoa sana Machozi ambayo kamwe hakuwahi kuyatoa Tangu aishi.

Babu aliiona damu ikivuja sana kwenye dirisha la nyumba kupitia mlango Mkuu ambao alizoea kila mara kuutumia kupita wakati akiwa katika nyumba ile, na kwa vile hakuna mgeni katika nyumba ile alijua kuwa kuna kitu kisicho kawaida katika nyumba ile na kupelekea roho moja wapo katika jumba lile inyofoke na kupotea kabisa, Damu hiyo ilikuwa ni damu nzito na alipoichunguza kwa makini aligundua kuwa ni damu ya Mtu mzima tena mwenye kujulikana hata nje ya ile nyumba ambayo Babu alikuwa akiishi zamani kabla kuhamia hii nyumba ndogo ambayo alijenga ili kujipumzisha akisubiri kifo chake.

Babu aliniambia Mambo sio mazuri pale mwezi Pacha utakapofika watu na watoto wa nyumba ile ambayo zamani babu alikuwepo watakuwa na huzuni kila watakapoona damu ile mlangoni pale.

Hadithi ya Zamani ambayo sitoweza kusahau.
 
"Babu aliniambia Mambo sio mazuri pale mwezi wenye namba mbili Pacha utakapofika na watu watoto wa nyumba ile ambayo zamani babu alikuwepo watakuwa na huzuni kila watakapoona damu ile mlangoni pale." Ahsante Mkuu
 
Back
Top Bottom