Usafi wa kucha na jinsi ya kuzitunza zisipate magonjwa

Namna Kucha Zinavyoweza Kutafsiri Afya ya Mwili Wako



Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa mwanamke. Mikono hutumika kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi. Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Pamoja na kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya mwanamke lakini pia ni vizuri kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za mwanamke kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini, vitamini na keratin na siyo rangi na vipodozi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha, inashauriwa kula mboga za majani, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Je! Unafahamu kuwa kucha zako zinaweza kukujulisha kuhusu afya yako? Zinaweza kukujulisha tatizo katika ini, mapafu na hata moyo wako. Tumekuwekea hapa maelezo ya kutosha ya namna muonekano wa kucha zako unavyoweza kukujulisha kuhusu afya yako.

1. Pale Nails

Pale Nail
Endapo rangi ya kucha zako ikiwa kama imefifia hivi basi kunawezekano mkubwa wa kuwa na tatizo la ukosefu wa damu, vile vile inaweza kuwa natitzo la kisukari au magonjwa ya Ini

2. White Nails



Ukiwa na kucha rangi nyeupe alafu zimezungukwa na weusi inasemekana utakuwa na tatizo la ugonjwa wa Ini (Hepatitis). Pia inaweza kuwa ni tatizo la figo au ukosefu wa virutubisho mwilini hasa Protini.

3. Yellow Nails



Endapo kucha zako zikiwa na muonekano wa rangi ya njano basi utakuwa unatatizo la fangasi kwani ndiyo chanjo kikuu cha kucha kuwa za njano. Lakini pia unaweza kuwa na tatizo la Tezi. Tafiti zinaonesha kuwa Tezi hili la shingoni husababisha kucha kutokuwa na afya zuri kwani thyroid homoni zinasababisha kucha kutengana na ukuta (mzizi wake) hivyo kupelekea kucha kushindwa kukua vizuri matokeo yake muonekano wa kucha unakuwa ni kama kwenye picha.

4. Bluish nails.


Ublue katika kucha nalo ni tatizo, hii inawezekana ukawa na tatizo katika mfumo wa hewa. Kuwa na kucha za rangi ya blue ni matokeo ya ukosefu wa oxygen katika kucha zako. Hii inasababishwa na kuwa na mzunguuko mdogo sana wa damu hasa katika maeneo ya baridi sana. Kuwa na mzunguuka mdogo wa damu kunasabosha damu isifike katika maeneo yote ya mwili kwa kiasi kinachohitajika.

5. Rippled nails.


Endapo utaona kucha zako ziko na vidoti vidoti kama inavyonekana kwenye picha na ngazi chini ya kucha inaonekana kama nyekundu basi wewe utakuwa na dalili za mwanzo za fangasi katika ngozi (Psoriasis). Hii inasababisha seli za ngozi ya juu kufa. Mara nyingi Psoriasis inatokea kwenye ngozi, kucha, viwiko (elbow) na magoti.

6. Dark lines beneath the nails.


Wataalamu wa afya wanasema kuwa endapo kucha zako zikionesha mstari mweusi kama ilivyokwenye picha, fanya haraka kutafuta hospitali kwa vipimo zaidi. Kuwepo kwa mstari huo mweusi ni dalili tosha za melanoma (Moja ya kansa mbaya sana za ngozi)
Inashauriwa kuwa ili tuweze kugundua rangi hii basi tusiwe tunapaka rangi za kucha kila mara. hii itatusaidia kutofautisha kati ya rangi za kucha na mstari huo. Vile vile kucha zikipata mwanga wa jua inakuwa rahisi kugundua rangi hizo na mwanga wa jua huwa haupiti kama kucha imepakwa rangi.

HITIMISHO.

Muonekano wa kucha ni njia rahisi kutambua afya yako lakini wakati mwingine si kila mwenye kucha nyeupe sana basi atakuwa na tatizo la ini. Pale unapohisi tu muonekano wa kucha zako umekuwa tofauti na ulivyouzoea basi fanya mpango wa kumuona daktari kwa ushauri na uangalizi zaidi.

Kwa afya njema ya kucha, mwanamke pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni. Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus) wanaoshambulia kucha.
Imeandaliwa na Muhsin Hero. Namna Kucha Zinavyoweza Kutafsiri Afya ya Mwili Wako | TANZANIA INVESTMENT ADVENTURERS
Nakukubali sana ndugu yangu Mzizi mkavu
 
yaani km vile vibibi vya kihindi


Mmh flat kama fundi cherehani eeh. basi nyota yako ishafifia hapa mjini. Unakosa vingi. Na si ajabu mguu nao ni kama waya wa gita.

Natoa consultation kwa wadada sampuli yako. Nitafute kwa muda wako.

-Kaveli-
 
Mmh flat kama fundi cherehani eeh. basi nyota yako ishafifia hapa mjini. Unakosa vingi. Na si ajabu mguu nao ni kama waya wa gita.

Natoa consultation kwa wadada sampuli yako. Nitafute kwa muda wako.

-Kaveli-
Ulijuajeee yani hivo viguu km kuni za nyongeza! nyuma bapaaaa....lkn nshukuru nmepata mume mzuri mwenye tabia nzuri na hekma! na watoto alhamdulillah....namshukuru Mungu!
 
ilikuwa ni nn dea? ya kwako ilitokeaje? na je ulienda hosp? hebu niambie ndugu yangu nao
Zilibadilika zikawa kama nimepaka hina hasa mkono wa kushoto,sikwenda hosptali lakini ile hali iliisha yenyewe
 
habari zenu ndugu zangu! ni mwanamke wa miaka 30 sasa! ndugu zangu jana usiku nmegundua kuwa kucha zangu zipo hivi! kamstari km ka rangi ya kahawia uliokaa km duara hv! hichi kidole kimoja kinaonyesha vizuri ila vingine vinaonyesha kwa mbaaali na vingine havina! je ni ugonjwa gani huu unaoninyemelea na ulionipata!?
790407d89dfb73739999ac6459c9ddd7.jpg
......nang'ata kucha jamani


Unajichamba vizuri lakini au?
 
Nilishajiwa, Na mgonjwa wa hivyo ila tulifanya vipimo vingi tu ili Ku study hiyo case; tuliomba FBP, biochemistry, urine test, HIV, kila tulichoomba ni negative hakikua na relevance zaidi zaidi tulikuta malaria tukaitibu, mgonjwa alendelea kuongezeka rangi mpaka ikawa kama hina kabsaa.

Mgonjwa yuko stable hana dalili yeyote ila kucha zimeshika rangi zote. Dermatology may wanaweza kusaidia. Consult huko .....
 
hazipo km ivo! sio yellow...angalia picha utaona kidole cha mwisho jinsi kilivyo
Ndio ni dalili za ugonjwa mwenywe nishapata hizo kucha nikiwa form six ila dactar alinipa dawa mistar ikatoweka
 
Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.

Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.

Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.



Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.

Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.

Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.

Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.

Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.

Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)



Chanzo: nakujuza255 blog
 

Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.

Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.

Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.

Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele. Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.

Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.

Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.

Usitoe hovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.

Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa. Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, baada ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembeau kitu chenye makali.



Ruhuwiko blog
 
KE hii inawahusu...mimi msela napata wapi muda wa kuanza kuremba kucha.. Nikishakata na wembe kwisha habari
 
Wakuu natanguliza salamu zangu na mniwie radhi kwa kuchanganya lugha katika uzi huu.

Urembo wa kucha ni utamaduni uliopo kwa muda mrefu sasa kwenye jamii yetu hasa katika kupaka rangi na kubandika kucha bandia (tips) na wengine kutengeneza kucha za unga (nail hardner)

Kwa sehemu kubwa MANICURE na PEDICURE (kukata na kuosha kucha za mikononi na miguuni bila kutumia kemikali) peke yake inatosha kwaajili ya matunzo na afya ya kucha lakini kumekuwa na hili la matumizi ya ;
NAIL POLISH
NAIL POLISH REMOVER
NAIL PRIMER
UNDERCOAT

Hivi vyote na vingine vinavyofanana na hivi hutokana na kemikali kadha wa kadha ambazo zinamadhara makubwa kwa watumiaji ambazo ni ;

PHTHALATES hizi ni kemikali zitumikazo kama plasticizers na kazi yake ni kuiwezesha rangi kusambaa vizuri kwenye uso wa kucha na kuzuia michubuko ya kucha .
Athari za kemikali hii ni katika mfumo wa hormone ambayo inapelekea endometriosis na wasichana kubalehe mapema (early puberty)

FORMALDEHYDES hizi zenyewe hutumika kama nails hardener na huongeza uwezekano wa magonjwa ya kansa kwa mtumiaji mwenye familia yenye historia ya magonjwa ya kansa .

METHACRYLATE na METHACRYLATE ACID hizi hutumika sana kwenye kutengeneza na kufitisha kucha bandia athari za kemikali hii ni huweza kumletea mtumiaji kansa .

PARABENS hapa kuna kemikali kama Methyl parabens na nyinginezo hizi hutumika kama preservatives chemical kuweza kutunza quality ya nail polish athari za kemikali hii ni huchangia kwa sehemu kubwa kuleta magonjwa ya kansa kwa mtumiaji.

Hizi ni baadhi ya kemikali chache nilizoweza kuwashirikisha zinazoweza kuleta athari kwa mtumiaji .

Ni hitimishe kwa kutumia msemo wa nguli wa toxicology Paracelsus aliyewahi kusema
“The dose makes the poison" ama kwa kigiriki “sola dosis facit venenum”

Asanteni.
 
Kweli Bora hinna tena ya majani, ya tube pia sio nzuri
Yeah in a chemical pia kuna mdada walimchora alikua anaharusi ebhanaeeh alivimba zle seem zote walizochora ngoz imejaa man as if kaungua moto harus ilkua chungu hahahaaa
 
Yeah in a chemical pia kuna mdada walimchora alikua anaharusi ebhanaeeh alivimba zle seem zote walizochora ngoz imejaa man as if kaungua moto harus ilkua chungu hahahaaa
Hahahhaaa, mimi kipaka kucha zinakatika kama gome la mti sina hamu nayo
 
Hata uwaambie hatari za kufa mtu, haitasaidia, wewe ushawahi kuweka kichwa kwenye yale ma microwave kichwani?! Au kuweka relaxer au Curl Kit?!
Sasa ndio uewelewe ujasiri wa hawa watu si wa mchezo mchezo, wanajilipuwa kuliko Al-Shabaab!
Acha kabisa aise...
 
Back
Top Bottom