korino
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 1,004
- 666
Habari zenu ndugu zangu! mimi ni mwanamke wa miaka 30 sasa! Ndugu zangu jana usiku nimegundua kuwa kucha zangu zipo hivi! Kamstari kama rangi ya kahawia uliokaa kama duara hivi!
Hiki kidole kimoja kinaonyesha vizuri ila vingine vinaonyesha kwa mbali na vingine havina!
Je, ni ugonjwa gani huu unaoninyemelea na ulionipataje?
=========
Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa binadamu. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.
Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma mtu katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.
Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, unaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zako kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe unaona unafaa kufanya hivyo hata ukiwa nyumbani.
Hii pia itakusaidia kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zako na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.
Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.
Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko.
Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha unashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha.
Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.
Kucha zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya mtu na familia yake hasa pale mtu anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.
Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.
Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.
Kwa afya njema ya kucha, pia unashauriwa usifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni. Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)
Usafi wa kucha
Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambavyo utavitumia unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu.
Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inayochangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya.
Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi.
Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, unapaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi.
Ni vyema kwa mtu anayejali afya ya kucha zake kuchukua muda mwingi kufuatilia kucha zake na kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha zinakuwa katika matunzo mazuri na kujitahidi kubuni mtindo ambao unaweza kuwa tofauti na wengine ambao wanapenda kuzifanya kawaida.
Hata hivyo katika kutunza kucha ziwe nzuri, vyakula ambavyo ni mlo kamili ni muhimu sana, vinginevyo utajikuta ukishauriwa na wataalamu kutumia vitamini mbalimbali kama vile vitamini A, vitamini C, Culcium, Folic Asidi, Protini na Vitamini B12.
Jinsi ya kusafisha kucha
1.Wekeza vifaa vizuri vya kisasa vya kutunzia kucha.
Tumia brush ya kucha kwa kusugua chini ya kucha na kuutoa uchafu na kufikia sehemu ngumu ambapo uchafu unajilundika. Unaweza tumia mswaki ukiwa huna vifaa vya kisasa.
2.Tumia maji moto na sabuni ya kunawia mikono. Anza kwa kusugua chini kabisa kwa kushikilia brush chini na sugua kuanzia nyuma kuja mbele pole pole, kisha juu ya kucha fanya hivyo kwa kuzunguka.
3.Toa rangi kwa kuloweka pamba kwenye polish remover.
Sugue kwa vidole vyenye hinna huna haja ya kuitoa. kwa vidole vya afya na nguvu vipumzishe kwa kutumia polish kila baada ya wiki kadhaa.
4.Loweka kucha na maji kwenye bakuli,au sinki,au kifaa cha uwezo wako hata dishi poa,kwa maji ya moto ya uvuguvugu na pitisha sabuni ya kunawia mikono.Na ni kucha tu usiloweke mkono mzima,kwa dakika tatu,sabuni kwenye maji hufanya mikono kuwa mikavu .
5.Suuza kwa maji safi ya uvuguvugu,au yaliyokua kwenye chombo yaani jimwagie,kisha zifute na taulo laini.
6.Tumia kikatio kucha kukata maana zitakua laini,au kifaa cha kuzipunguza kuweka sawa kama hauzikati.
Michango ya wadau

-----Namna Kucha Zinavyoweza Kutafsiri Afya ya Mwili Wako
Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa mwanamke. Mikono hutumika kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi. Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.
Pamoja na kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya mwanamke lakini pia ni vizuri kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za mwanamke kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini, vitamini na keratin na siyo rangi na vipodozi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha, inashauriwa kula mboga za majani, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.
Je! Unafahamu kuwa kucha zako zinaweza kukujulisha kuhusu afya yako? Zinaweza kukujulisha tatizo katika ini, mapafu na hata moyo wako. Tumekuwekea hapa maelezo ya kutosha ya namna muonekano wa kucha zako unavyoweza kukujulisha kuhusu afya yako.
1. Pale Nails
Pale Nail
Endapo rangi ya kucha zako ikiwa kama imefifia hivi basi kunawezekano mkubwa wa kuwa na tatizo la ukosefu wa damu, vile vile inaweza kuwa natitzo la kisukari au magonjwa ya Ini
2. White Nails
Ukiwa na kucha rangi nyeupe alafu zimezungukwa na weusi inasemekana utakuwa na tatizo la ugonjwa wa Ini (Hepatitis). Pia inaweza kuwa ni tatizo la figo au ukosefu wa virutubisho mwilini hasa Protini.
3. Yellow Nails
Endapo kucha zako zikiwa na muonekano wa rangi ya njano basi utakuwa unatatizo la fangasi kwani ndiyo chanjo kikuu cha kucha kuwa za njano. Lakini pia unaweza kuwa na tatizo la Tezi. Tafiti zinaonesha kuwa Tezi hili la shingoni husababisha kucha kutokuwa na afya zuri kwani thyroid homoni zinasababisha kucha kutengana na ukuta (mzizi wake) hivyo kupelekea kucha kushindwa kukua vizuri matokeo yake muonekano wa kucha unakuwa ni kama kwenye picha.
4. Bluish nails.
Ublue katika kucha nalo ni tatizo, hii inawezekana ukawa na tatizo katika mfumo wa hewa. Kuwa na kucha za rangi ya blue ni matokeo ya ukosefu wa oxygen katika kucha zako. Hii inasababishwa na kuwa na mzunguuko mdogo sana wa damu hasa katika maeneo ya baridi sana. Kuwa na mzunguuka mdogo wa damu kunasabosha damu isifike katika maeneo yote ya mwili kwa kiasi kinachohitajika.
5. Rippled nails.
Endapo utaona kucha zako ziko na vidoti vidoti kama inavyonekana kwenye picha na ngazi chini ya kucha inaonekana kama nyekundu basi wewe utakuwa na dalili za mwanzo za fangasi katika ngozi (Psoriasis). Hii inasababisha seli za ngozi ya juu kufa. Mara nyingi Psoriasis inatokea kwenye ngozi, kucha, viwiko (elbow) na magoti.
6. Dark lines beneath the nails.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa endapo kucha zako zikionesha mstari mweusi kama ilivyokwenye picha, fanya haraka kutafuta hospitali kwa vipimo zaidi. Kuwepo kwa mstari huo mweusi ni dalili tosha za melanoma (Moja ya kansa mbaya sana za ngozi)
Inashauriwa kuwa ili tuweze kugundua rangi hii basi tusiwe tunapaka rangi za kucha kila mara. hii itatusaidia kutofautisha kati ya rangi za kucha na mstari huo. Vile vile kucha zikipata mwanga wa jua inakuwa rahisi kugundua rangi hizo na mwanga wa jua huwa haupiti kama kucha imepakwa rangi.
HITIMISHO.
Muonekano wa kucha ni njia rahisi kutambua afya yako lakini wakati mwingine si kila mwenye kucha nyeupe sana basi atakuwa na tatizo la ini. Pale unapohisi tu muonekano wa kucha zako umekuwa tofauti na ulivyouzoea basi fanya mpango wa kumuona daktari kwa ushauri na uangalizi zaidi.
Kwa afya njema ya kucha, mwanamke pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni. Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus) wanaoshambulia kucha.
Imeandaliwa na Muhsin Hero. Namna Kucha Zinavyoweza Kutafsiri Afya ya Mwili Wako | TANZANIA INVESTMENT ADVENTURERS
----Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.
Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.
Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.
Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.
Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.
Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.
Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.
Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.
Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.
Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.
Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)
Chanzo: nakujuza255 blog
----Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.
Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.
Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.
Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele. Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.
Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.
Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.
Usitoe hovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.
Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa. Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, baada ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembeau kitu chenye makali.
Ruhuwiko blog
Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.