Urembo siyo zawadi bali ni mtihani wa asili kwa mwanamke

Nov 15, 2019
35
113
Habari za wakati huu wana JF, poleni sana na majukumu.

Wanawake wengi wamekuwa wakijivunia urembo wao kama zawadi ya uumbaji kutoka kwa Mungu na kusahau kuwa huo ni mtihani wa asili ambao wamepewa katika maagano ya uumbaji na wanapaswa kuufaulu ili waweze kujipatia heshima duniani.

Unakuta mwanamke ni mzuri kwa mwonekano lakini matendo yake ni meusi na hiyo chanzo chake huwa ni sifa ya urembo anayopatiwa na wenye hamu.
Mwanamke mzuri ni yule anayejiheshimu na kujua ni namna gani atakavyopambanua maisha yake kwa faida yake, familia yake na hata ndoa yake (kwa walioolewa).

Malezi kutoka kwenye familia zetu yamekuwa yakiathiri maisha yetu kwa kiasi kikubwa na hii ni kutokana na aina ya wazazi tulionao. Unakuta binti amezaliwa na kukua katika maisha ya madeko, yaani baba anakuambia "Ooh my daughter! You look so cute!" Halafu sifa hizo zinapokuja kuhamia kwenye akili ya binti matokeo yake ndipo tunapokuja kupata mabinti wasioeleweka mtaani, yaani unakuta ni Mrembo ila amezalishwa nyumbani. Wakati mwingine wazazi jitafakarini kabla hamjaanza lawama maana huenda mzazi ukawa ndo chanzo cha kuharibika kwa binti yako.

Dada zetu tunawapenda na tunawaombea mema, lakini iheshimuni miili yenu na muilinde heshima ya jamii zetu.
Urembo ni mtihani, unaposifiwa urembo jichunguze sana.

Wazazi ishini na watoto wa sasa kwa maisha ya kisasa lakini malezi yawe ya kizamani vinginevyo aibu itazidi kukiandama kizazi hiki.
Asanteni!​
 
Una akili nyingi sana mkuu. Heshima ya kipekee kwako.
 
Back
Top Bottom