Urasimu wa RITA

Urasimu wa RITA

Benno Bongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
621
Reaction score
716
Kumekuwa na tabia ukienda kujiandikisha kupata cheti cha kuzaliwa unapewa mlolongo mrefu usio na maana yeyote, mfano unaambiwa ulete kadi yako ya kliniki, uje na mzazi, vyeti vya ubatizo n.k pia kulazimisha mtu kujisajili mahali ulipozaliwa, Ina maana kwa mfano nimezaliwa kigoma lakini familia ikahama ikaenda kuishi mtwara nitatakiwa nisafiri mpaka Kigoma kufuata huduma ilihali ni nchi moja?

Tunaomba RITA, viongozi, na wote wanaohusika mliangalie hili kuepusha usumbufu usio na ulazima.
 
Wanafanya hivyo ili iwe rahisi ku prove kama hudanganyi.

Mfano ukisema ulizaliwa hospitali ya temeke tarehe flani, ni rahisi kwa Rita ya Temeke kwenda ku prove hapo hospital ya temeke... kuliko ukienda Rita ya Mwanza uwaambie umezaliwa hospital ya temeke.. watashindwa kuja temeke hospital maana ni mbali na gharama
 
Karne ya 21 mwaka 2022 yan kujua mtu kama alizaliwa kigoma mpaka uende kigoma ? mkuu upo serious au unatania ? kazi ya technology ni nini ?
 
Serikali haina technology hiyo unayoitaka, data base nyingi zipo kwenye manual files

Ndio maana wanakwambia nenda Rita ya wilaya uliyozaliwa
 
yan wanadatabase ya takwimu ya wananchi wote tanzania, database ya vitambulisho vya taifa hapa rita kipi kigumu mkuu ? they are just stupid....
 
Wanafanya hivyo ili iwe rahisi ku prove kama hudanganyi.

Mfano ukisema ulizaliwa hospitali ya temeke tarehe flani, ni rahisi kwa Rita ya Temeke kwenda ku prove hapo hospital ya temeke... kuliko ukienda Rita ya Mwanza uwaambie umezaliwa hospital ya temeke.. watashindwa kuja temeke hospital maana ni mbali na gharama
Vipi wale waliokua wanazaliwa nyumbani tu na sio hospitalini kama ilivyokua zamani?
 
Kumekuwa na tabia ukienda kujiandikisha kupata cheti cha kuzaliwa unapewa mlolongo mrefu usio na maana yeyote, mfano unaambiwa ulete kadi yako ya kliniki, uje na mzazi, vyeti vya ubatizo n.k pia kulazimisha mtu kujisajili mahali ulipozaliwa, Ina maana kwa mfano nimezaliwa kigoma lakini familia ikahama ikaenda kuishi mtwara nitatakiwa nisafiri mpaka Kigoma kufuata huduma ilihali ni nchi moja?

Tunaomba RITA, viongozi, na wote wanaohusika mliangalie hili kuepusha usumbufu usio na ulazima.
Unaweza kuomba online cheti kikatengenezwa kigoma na ukakichukulia hapo ulipo, kuhusu viambatisho sio lazima uwe navyo vyote. Unatakiwa uwe na ama kadi ya kliniki, au kadi ya NIDA, au kadi ya mpiga kura, au cheti cha ubatizo, au pasi ya kusafiria , au leaving certificate ya Sekondari nk. Kimsingi inahitajika document yenye kuthibitisha tarehe yako ya kuzaliwa na mahali ulipo zaliwa. Mzazi wako hahitajiki unless watilie mashaka uraia wako.

Lengo ni kuhakikisha wanaosajiliwa ni waliozaliwa Tanzania tu. Unataka walegeze masharti ili hadi wanyarwanda na wakongoman nao wasajiliwe?
 
yan wanadatabase ya takwimu ya wananchi wote tanzania, database ya vitambulisho vya taifa hapa rita kipi kigumu mkuu ? they are just stupid....
Sasa watakuaje na database ya kizazi kisichosajiliwa?? Cheti cha kuzaliwa huna, utakuwaje kwenye database ya RITA??

Hata hao NIDA wana database ya Raia waliosajiliwa tu
 
mkuu waza kwa upana, database iwepo, sasa mtu anakitambulisho cha taifa alafu rita haimtambui huoni kama huo ni ujinga ? kwanini mnatafuta excuse ya vitu ambavyo vipo obvious ? walijuaje yeye ni mtz ? sensa si inahesabu kila mtz ? na serikali inaamini , kwanini tusilink hiz db ? huoni kama tutapunguza data redundancy ? mkuu waza kwa upana, kumrudisha mtu tarime wakati alikuwa dar kisa kaja rita na unataka kujua kazaliwa wapi na sensa ilimpitia na alishawah kupiga kura kwakweli huo ni usengelema ambao haupo nchi nyingi sana duniani...mzee waza kwa upana njoo na challenge mpya, ulichosema hapa hakina logic yeyote mkuu...
 
Unaweza kuomba online cheti kikatengenezwa kigoma na ukakichukulia hapo ulipo, kuhusu viambatisho sio lazima uwe navyo vyote. Unatakiwa uwe na ama kadi ya kliniki, au kadi ya NIDA, au kadi ya mpiga kura, au cheti cha ubatizo, au pasi ya kusafiria , au leaving certificate ya Sekondari nk. Kimsingi inahitajika document yenye kuthibitisha tarehe yako ya kuzaliwa na mahali ulipo zaliwa. Mzazi wako hahitajiki unless watilie mashaka uraia wako.

Lengo ni kuhakikisha wanaosajiliwa ni waliozaliwa Tanzania tu. Unataka walegeze masharti ili hadi wanyarwanda na wakongoman nao wasajiliwe?
Wewe hapa umerahisisha sana, ila kiuhalisia haiko hivyo, kuna usumbufu mwingi
 
Unaweza kuomba online cheti kikatengenezwa kigoma na ukakichukulia hapo ulipo, kuhusu viambatisho sio lazima uwe navyo vyote. Unatakiwa uwe na ama kadi ya kliniki, au kadi ya NIDA, au kadi ya mpiga kura, au cheti cha ubatizo, au pasi ya kusafiria , au leaving certificate ya Sekondari nk. Kimsingi inahitajika document yenye kuthibitisha tarehe yako ya kuzaliwa na mahali ulipo zaliwa. Mzazi wako hahitajiki unless watilie mashaka uraia wako.

Lengo ni kuhakikisha wanaosajiliwa ni waliozaliwa Tanzania tu. Unataka walegeze masharti ili hadi wanyarwanda na wakongoman nao wasajiliwe?
Kuomba online ikoje hiyo
 
mkuu waza kwa upana, database iwepo, sasa mtu anakitambulisho cha taifa alafu rita haimtambui huoni kama huo ni ujinga ? kwanini mnatafuta excuse ya vitu ambavyo vipo obvious ? walijuaje yeye ni mtz ? sensa si inahesabu kila mtz ? na serikali inaamini , kwanini tusilink hiz db ? huoni kama tutapunguza data redundancy ? mkuu waza kwa upana, kumrudisha mtu tarime wakati alikuwa dar kisa kaja rita na unataka kujua kazaliwa wapi na sensa ilimpitia na alishawah kupiga kura kwakweli huo ni usengelema ambao haupo nchi nyingi sana duniani...mzee waza kwa upana njoo na challenge mpya, ulichosema hapa hakina logic yeyote mkuu...
Huyu bila shaka ni mfanyakazi wa RITA
 
Ivi wakuu mtu unaweza kubadili jina la mzazi katika cheti cha kuzaliwa
 
Back
Top Bottom