Wana jamvi,
Mamlaka ya iliyopewa dhamana ya kuratibu mchakato wa vitambilisho vya taifa imeonesha udhaifu mkubwa sana na urasimu wa hali ya juu.
Kwanza,utoaji wa ajira za muda mfupi kwa vijana wanaohusika na upigaji picha.NIDA wametoa ujira kwa usiri mkubwa sana na kwa taarifa za kuaminika ni kwamba ajira zimetolewa kwa kujuana wakati wapo vijana waliomaliza vyuo vikuu nchini hawana kazi ya kufanya.
Na wale waliopo hawakidhi vigezo kwani wanafanya kazi taratibu sana ivo kuweka foleni kubwa sana sehemu za kupigia picha.
Pili,kuna wananchi ambao majina yao hayapo kwenye mbao za matangazo mfano kata ya Kijichi wilaya ya Temeke majina ya watu hayaonekani na hakuna jibu lilotolewa la kuridhisha wananchi.
tatu,kuna wananchi wa jiji la Dar es Salaam ambao hawakuwepo kipindi cha kujiandikisha mwaka jana kwa minajili kuwa walisafiri na kwa muda huu wapo DSM lakini NIDA wameshindwa kutoa utaratibu kuhusu suala ili.
NINAOMBA NIDA NA WANABODI WOTE WENYE MAELEZO YA KUTOSHA KUHUSU SUALA HILI WAWEZE KULITOLEA UFAFANUZI.