Urasimu katika ofisi za RITA makao makuu Dsm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urasimu katika ofisi za RITA makao makuu Dsm

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by denoo49, May 10, 2012.

 1. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,658
  Likes Received: 5,249
  Trophy Points: 280
  Binafsi nimekerwa sana na utoaji huduma wa hizi ofisi za usajili wa vizazi na vifo. Kuna kila dalili ya harufu ya rushwa ili uweze kupata huduma. Kipindi ofisi hizi zinaanzishwa walikuwa watoa huduma na washauri wazuri kwa mteja ila mpaka kufikia sasa kama huna "kitu" ni utazungushwa mpaka.....! Nina mifano ya dhahiri na wazi nilikutana na mwenzangu takribani ni siku ya nane sasa katika hizi ofisi tukiwa na shida ya aina moja ila mwenzangu alihudumiwa ndani ya siku moja akamaliza tatizo lake ila mimi mpaka leo hii ni mwendo wa kupigwa tarehe na kupewa sababu zisiso kuwa na msingi... mara vitabu vya kumbukumbu havionekani, mara ndani kuna joto mpaka umeme urudi tuweze kutafuta vitabu, na nyinginezo kama hizo.
   
 2. Advicer

  Advicer JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  kaka sio dar tu!hata songea ni hivo hivo,kwanza vyeti unafwatilia zaidi ya mwezi.pia kiasi unachoandikiwa kwenye cheti na kile cha kwenye risiti ni tofauti.
   
 3. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,658
  Likes Received: 5,249
  Trophy Points: 280
  sipati jibu mpaka sasa kinacho wapa kiburi na jeuri katika kuhudumia watu ni nini hasa.? Hii inanipa picha ya kuwa hata uongozi wao wa juu utakuwa mbovu. Naomba taarifa hizi ziwafikie TAKUKURU popote walipo na ikiwezekana waanze kutembea kwenye ofisi zao, na wakati huo huo uongozi wa juu wachukue hatua ya kurekebisha "uozo" huu.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Sijuhi upo Mkoa gani ama wilaya gani, na wala siwezi kukupinga kwa sababu umeyaona, lakini kwa pale upanga, nyuma ya muhimbili naona wako poa sana na wala sijaona hizo dalili za kudai pesa
   
 5. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,658
  Likes Received: 5,249
  Trophy Points: 280
  nipo kwenye hizi hizi ofisi za upanga. Au we ndo'mwenzangu uliye hudumiwa fasta. Maana mwanzo nilisita kulalamika nikijua hii kero itakuwa imenikumba mimi peke yangu ila naona ni asilimia kubwa ya watu walo hapa inawakumba.
   
Loading...