Urais waumiza vichwa UKAWA, CHADEMA waja na mbinu ya Mwai Kibaki, CUF washtuka

GAZETI zuri sana hili kwa habari za uhakika, jiondoeni upofu kwa kung'ang'ania kusoma Tanzania Daima , mtaishia kusoma habari za CHADEMA peke, someni magazeti yanayo address masuala ya kitaifa na siyo ya SACCOSS ya CHADEMA.
Mwenye akili ya kutaka kuelewa yanayojili ndani na nje ya nchi, hawezi kusoma Tazama. Kwa Lumumba type sawa. Linauzwa sh. ngapi vile, maana hata sijui bei yake
 
Nimeelewa ni kwa nini hawa jamaa huwa wako shallow na unrealistic kwa mambo mengi kiasi kila wakiandika kitu hapa ni utumbo hadi wanaudhi.

Kumbe wanajisomea magazeti ya "TAZAMA"!.

Maskini ccm. Kwisha habari zao.

Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
 
Hata nani yangu hujamuokota kirahisi hivyo na kijarida chako cha tazama. CCM mtakuwa na mengi na mtulie tu sababu mtashinda kwa kishondo!!!
 
Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
umesema kweli tatizo mbinu za propaganda zimeisha
 
Hicho kigazeti bado kipo, kunawakati kilikomaa na Habari za Dr.Slaa naona sasa kimehamia ukawa.
 
GAZETI zuri sana hili kwa habari za uhakika, jiondoeni upofu kwa kung'ang'ania kusoma Tanzania Daima , mtaishia kusoma habari za CHADEMA peke, someni magazeti yanayo address masuala ya kitaifa na siyo ya SACCOSS ya CHADEMA.

Ndio mnalosoma Lumumba? maskini wa mawazo ndio maana mnatema sana pumba kumbe mnakiwanda
 
Ni kilaza pekee ndio hajui mgombea urais wa UKAWA atatoka CHADEMA.
CUF watamsimamisha Maalim Seif Zanzibar,na CHADEMA watatoa mgombea urais wa muungano.
CUF hawawezi kusimamisha mgombea urais pande zote za Muungano.
Hata hivyo CHADEMA wanaushawishi zaidi Tanganyika kuliko CUF.

UMELONGA SWAYIBA, WANAOMPIGIA CHAPUO LIPUMBA NI MACCM ATI YANAJARIBU KUDRO ATTENTION KWA KITU IMPOSSIBLE PIA KUTUGOMBANISHA, AAAAAAH WAIACHE UKAWA Yetu,
 
Ndoto ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi , maarufu kwa jina la UKAWA , ya kutaka kusimamisha mgombea mmoja wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , inaweza isifanikiwe kutokana na msuguano wa chini unaoendelea ndani ya vyama vikuu viwili vinavyounda umoja huo; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na chama cha Wananchi(CUF).Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika duru za siasa za vyama hivyo viwili zinaeleza kwamba wakati viongozi wakuu wa CHADEMA wanataka kutumia mbinu ya Mwai Kibaki wa Kenya , iliyomuwezesha kukiondoa madarakani chama kilichoipatia uhuru nchi hiyo cha KANU mwaka 2002 kwa kutumia muungano wa wanasiasa muhimu katika siasa za Kenya uliopewa jina la NARC , baadhi ya viongozi na wanachama wa CUF wameeleza kushtushwa na mbinu hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi wa na wanachama wa hao wa CUF, wameeleza mbinu hiyo ya viongozi wa CHadema kwamba inalenga kukidhoofisha chama chama chao kwa upande wa Bara, hali ambayo wanasema hawawezi kukubali kuona Mwenyekiti wao Profesa Ibrahimu Lipumba akishawishika kwa namna yoyote ile kuacha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupumbazwa na hicho kinachoitwa UKAWA.

Source: gazeti la TAZAMA Tanzania.

jukwaa la great thinker limegeuka kua jukwaa la great ignorant,linaloeneza ujinga wa kunakili,mwl nyerere aliwaisema mtu mjinga akikwambia jambo nawe ukakubali atakudharau'''binafsi siwez kua sehem ya watu wajinga wanaominishwa na mtu mjinga!!!hakuna jipya ni propaganda za kizandiki kuvuruga ukawa kwa hoja za kijinga mithili ya mtu mwenye elimu ya kaptula!!!!kama wewe ndo mpiga propaganda na magazeti uchwara ya ka.koo basi wahusika wanatakiwa kufanya mabadiliko haraka sana ili kunusuru kitengo....!!blinded mind appreciate even in darkness!!!!!
 
hii riwaya inamapungufu nenda uksitengeneze tena alafu uilete hapa ili tufurahi wote.sawa kijana!
 
Msema Kweli Ni Mpenzi Wa Mungu! Hili Gazeti Nilikua Silifahamu Vziri, Niliwahi Kulinunua Mwaka 2009 Baada Ya Kusoma Kichwa Cha Habari Yake. Mungu Wangu Nilichokutana Nacho Ndani! Nilijuta Kupoteza Jero Yangu. Ni Zaidi Ya Udaku.
 
Hiyo Ni Tabia Ya Fisi Kumfuata Mtu Nyuma Ili Mkono Ukidondoka Abebe.Mta TAZAMA Sana!
 
CUF na CHADEMA ni ndoto kusimamisha mgombe mmoja kwenye Urais!Sera, mbinu na mitazamo yao katika siasa ni tofauti mnoo, NCCR Mageuzi kinaweza kuungana na chama chochote kati ya hivyo!Tukiwa wakweli hapo kuna element kubwa ya Udini na Ung'ang'anizi wa madaraka!

Mkuu achana na sera, mbinu, mtazamo n.k.Muungano huo ni mzuri na CCM itabidi ijipange. Hata hivyo hapa uchu wa madaraka utafanya kazi yake. Ukichunguza kiukweli pale CDM kuna sura ya kumuachia Prof. Lipumba au yeyote kutoka CUF au NCCR Mageuzi aingie Ikulu hivihivi, patachimbika.
 
Hili ni gazeti la kufungia vitumbua halina tofauti la lile la ccm Uhuru mbona hawandiki ccm kufa wakati ccm unakaribia kufa muda wowote
 
Mkuu achana na sera, mbinu, mtazamo n.k.Muungano huo ni mzuri na CCM itabidi ijipange. Hata hivyo hapa uchu wa madaraka utafanya kazi yake. Ukichunguza kiukweli pale CDM kuna sura ya kumuachia Prof. Lipumba au yeyote kutoka CUF au NCCR Mageuzi aingie Ikulu hivihivi, patachimbika.

Muungano ni mzuri lakini hauwezekani kati ya CUF na CHADEMA!Wakilivuka hili wataiondoa CCM madarakani 2015, lakini sioni hilo likitokea!Nitarejea na maelezo yangu haya siku mambo yakiwashinda. Take it from me Lipumba Hawezi acha kugombea urais wala kuwaacha/kuwasaidia chadema waongoze dola, ni bora wakose wote.Na vivyo hivyo chadema hawawezi kukubali CUF isimamishe wagombe wa urais Tanzania na Zanzibar, na wakiwa chama kikuu cha upinzani hawawezi kuachia chama kingine kisimamishe mgombea wa TZ
 
GAZETI zuri sana hili kwa habari za uhakika, jiondoeni upofu kwa kung'ang'ania kusoma Tanzania Daima , mtaishia kusoma habari za CHADEMA peke, someni magazeti yanayo address masuala ya kitaifa na siyo ya SACCOSS ya CHADEMA.

Yeye kakuambia soma Tanzania daima? Mbona unajishuku? Hivi huko kwenu hakuna watu wenye weledi wa kuwaambia kuwa kutumia kazeti kama TAZAMA kufanya propaganda ni kujivunjia heshima? Ni sawa na kumtumia mwendawazimu apite mtaani kukunadi kugombea Uenyekiti wa Mtaa. Watu watakuona nawe ni mwehu tuu.
Hilo halina sifa ya kuitwa gazeti hata kama kuna habari kuwa Mhariri wake (ambaye anafahamika tabia zake) analipwa na ofisi yenu ndogo ile mliyobomoa kuharibu historia.
 
Back
Top Bottom