Urais waumiza vichwa UKAWA, CHADEMA waja na mbinu ya Mwai Kibaki, CUF washtuka

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Ndoto ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi , maarufu kwa jina la UKAWA , ya kutaka kusimamisha mgombea mmoja wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , inaweza isifanikiwe kutokana na msuguano wa chini unaoendelea ndani ya vyama vikuu viwili vinavyounda umoja huo; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na chama cha Wananchi(CUF).Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika duru za siasa za vyama hivyo viwili zinaeleza kwamba wakati viongozi wakuu wa CHADEMA wanataka kutumia mbinu ya Mwai Kibaki wa Kenya , iliyomuwezesha kukiondoa madarakani chama kilichoipatia uhuru nchi hiyo cha KANU mwaka 2002 kwa kutumia muungano wa wanasiasa muhimu katika siasa za Kenya uliopewa jina la NARC , baadhi ya viongozi na wanachama wa CUF wameeleza kushtushwa na mbinu hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi wa na wanachama wa hao wa CUF, wameeleza mbinu hiyo ya viongozi wa CHadema kwamba inalenga kukidhoofisha chama chama chao kwa upande wa Bara, hali ambayo wanasema hawawezi kukubali kuona Mwenyekiti wao Profesa Ibrahimu Lipumba akishawishika kwa namna yoyote ile kuacha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupumbazwa na hicho kinachoitwa UKAWA.

Source: gazeti la TAZAMA Tanzania.
 
Attachments

  • cuf5.jpg
    cuf5.jpg
    30.1 KB · Views: 1,079

View attachment 223889
"MAFASHISTI",

Yanahangaika,Yanatetemeka, Tazama, Mwaka wenu huu Mtaimba kila aina ya Nyimbo.
 
Last edited by a moderator:
Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
 
Raha yako tuandike udaku wa TANZANIA DAIMA?
 
TAZAMA linatoka nchi gani hivi?Maana sijawahi kuona Watanzania wakilinunua!
GAZETI zuri sana hili kwa habari za uhakika, jiondoeni upofu kwa kung'ang'ania kusoma Tanzania Daima , mtaishia kusoma habari za CHADEMA peke, someni magazeti yanayo address masuala ya kitaifa na siyo ya SACCOSS ya CHADEMA.
 
Binafsi siamini kama lipumba atakubali kutogombea urais mwaka huu kamwe. Maana amegombea toka mwaka 1995, sijui kama atakubali kuacha. Pia sioni uwezekano wa dr. Slaa kukubali kumwachia lipumba.
 
CHADEMA walikuwa wanawachukulia poa CUF, mwaka huu ndiyo watajua nini maana ya NGUNGURI ya CUF.
 
Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
Wewe ndani ya CHADEMA ni sawa na karai la zege tu, likishatumika hutupiliwa mbali, hujui hili wala lile wanaojua kinachoendelea ndani ya UKAWA watakubaliana tu na kilichoandikwa humu.
 
Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
Mkuu umerudi? Ulipotea kama mzizi wa jiwe baada ya kuwa umevurugwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama chetu. Jipe moyo mkuu nafasi yako bado ipo.
 
Sasa haya magazeti ya kijinga mkuu unayaletaje huku?

Ukigeuza page ya pili na tatu utakuta Elimu ya unajimu kisha 4&5 utakutana na Hadithi za Illuminati na jinsi ya kujiunga Freemanson kisha page ya 6 habari za michezo mashindano ya kombe la mbuzi na pia taarifa za kutanda kwa hali ya wasiwasi juu ya Ushirikina kwenye kambi za timu zinazocheza Robofainali za AFCON kule Guinea ya Ikweta

Please ! JF inahitaji heshima yake !
mkuu hili gazeti kila siku front page ni kusema ukawa inakufa wanakesha wakiomba ife
 
Kwani ukawa kunaviongozi jamani hebu tuache utani hakuna kiongozi pale hata mmoja kundi la wahuni na upotoshaji.
 
GAZETI zuri sana hili kwa habari za uhakika, jiondoeni upofu kwa kung'ang'ania kusoma Tanzania Daima , mtaishia kusoma habari za CHADEMA peke, someni magazeti yanayo address masuala ya kitaifa na siyo ya SACCOSS ya CHADEMA.
Naona umepewa kazi ya kuisambaza katika mitandao na blogs zote. Hongera
 
Back
Top Bottom