kwa hali inavyokwenda sasa ni heri kutafakari, haya mambo naona yanazidi nia ya kugombea uraisi ipo kitu kubwa wengi hatuijui. I am still studing the saga. Demokrasia at its highest level, scrumble at its highest level. Tuatafika na aumivu yetu wote.
Chonde chinde wapenzi na wale wasio wapenzi wa Kijana wetu ZZK wote tumieni busara. Dr kitila ameita hii hali uliberali mchwara, mimi naita demokrasia kwenye iliyokomaa kwa mtoto mchanga. Chadema bado inakuwa na haijakomaa bado kama chama chenyewe hakijaweza kufika mikoa yote huo uraisi tunaotaka kutoana nao macho ni kiini macho.
Sifa zote wanazopeana wakubwa zingesaidia kama wangekuwa wanajenga mtandao wa kushinda, siasa za ushindi zinafanywa leo sio jana. Nyerere alimwata Mkapa Mr Clean miaka kumi baadaye Mkapa aligeuka jina na kuitwa fisadi. Chenge alikuwa mfanyakazi asiyejua kuiba miaka kumi baadaye kawa mzee wa vijisenti.
Kinachotufanya Watanzania kuwa masikini ni viongozi wetu kupenda vyeo badala ya kazi na wananchi. Kizazi cha sasa tujifunze kuwapenda wananchi, nchi yetu na sehemu tunazoishi.
Chadema haiwezi kushinda Uraisi 2015 kama vijana mliopata fursa ya kutuongoza hamtaacha tamaa na kuwa kitu kimoja kumtoa adui CCM. Badala ya kuazna kuteteana leo miaka mitatu kabla ya uraisi wenyewe. Nia kila mtu atoae matamko kila mtu atamke halafu tunawahitaji site, huwezi kushinda uraisi maelezo na huwezi kushinda uraisi kwa kazi ya mwaka juzi. Ushindi ni leo na ni sasa kamanda ni alyeko site sasa sio jana.
Chief Mkwawa wa Kalenga
Anawatakia wote kwenye makundi ya Uraisi ndani ya CDM waende site waache kelele.