Urais wa Zitto 2015 ni kwa tiketi ya CHADEMA - Habib Mchange

Teh teh teh, hii ni 2012, sipati picha 2014 itakuaje! Ee Mungu, tunusuru waja wako, hatuna chochote zaidi ya pumzi tuliyonayo..!
 
Ni kwanini JK hakufanya kampeni jimboni kwa Zitto pekee?
Kwa nini mpaka sasa Zitto hataki kuongelea mauwji yanayofanywa na Polisi?
kwanini Zitto hashiriki M4C na vikao vingine vya Chama?
Kwanini zitto ajitangaze kabla ya kutangazwa?
Kwanini kila kukicha kuna thread mpya3 tofauti za ZK ndani ya JF, kila post anawalipa shg ngap?
 
Kuna watu huwa wanataka umaarufu usio na tija we katiba yenyewe hairuhusu sasa why disturb us na utakaji wa uraisi wakati bado miaka mitatu mbele?
Hivi huwa mnasoma shule gani nyie mbona hata ambao hatujasoma sana twawazidi kasomeni katiba na pia nahakika hatakuwa raisi huyo Zitto

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Kuna haja kujadili mantiki ya mada yenyewe, ZITTO anafaa au hafai kuwa Rais? mbona tunazunguka sana? kama anafaaa suala la katiba ni issue nyingine, tumkubali kwanza kijana ZITTO hayo mengine yatafuata. Suala la katiba liko chini ya uwezo wetu, ni kiasi tu cha kutoa maoni kwenye tume ya katiba mpya na umri utapunguzwa tu. Hii ni dunia ya vijana bwana. Nasisitiza, tuongelee uwezo wa ZITTO na siyo umri. Binfsi naona ZITTO ndiye anafaa kupeperusha bendera ya CDM 2015
 
Haya ni madhara ya lishe duni enzi ya utoto!Hv kati ya Dr na ZZK nani alitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa majimbo tajwa kwenye makala?Ati ni mbunge makini bungeni?anawazidi J Mnyika,na Tundu Lissu anayeogopwa hata na mkuu wa kaya aliyepita na aliyepo?Kama ni lazima Rais awe kijana aliyezaliwa baada ya uhuru kama alivyowahi kuropoka huyo Rais wa Facebook,basi CDM atakuwa Mnyika.Si kwamba Zito hana uwezo,ila ana busara fupi.
 
Mkuu hujui kuna mchakato wa kuandika katiba upya na vijana wanataka umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40? Hujui kwamba ahadi ya Rais JK ni kwamba katiba mpya itapatikana kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015? Ikiwa hivyo na bahati nzuri umri ukapunguzwa hadi miaka 40 basi Zitto atakuwa ndani ya wigo.

Wewe kweli Kimbunga!! Unaishi dunia ipi ambayo ahadi za Kikwete zinatimizwa; huyu watu wanamchukulia kama alivyo kuwa ni mzurulaji, kwani aliahidi maisha bora kwa wananchi imekuwa ni ndoto; pia akaahidi kutunga sheria ya kuwabana wanasiasa na wafanyabiashara nayo imeota mbawa!!! Sasa huyo Kikwete wa kukupa katiba kabla ya uchaguzi wa 2015 ni yupi huyo? Ni huyu huyu Kikwete wa Msoga au umemchonga mwingine?
 
Such a sounding descriptions,lets wait for Katiba Mpya probably Zitto could stand as Presidential candidate through CDM...
 
Mwambie katiba haimnruhusu kufanya hivyo amalize kukua,hatuweki wahuni ikulu nakuhakikishia it will take so long kwa zitto kuwa rais wa tz,huyu si atatujengea bilcana ndani ya ikulu lol
 
Such a sounding descriptions,lets wait for Katiba Mpya probably Zitto could stand as Presidential candidate through CDM...:lol:
 
Makundi ndani Chadema ndio kwanza yanaanza, Chadema Kaskazini povu linawatoka.
 
Mkuu Molemo huyu Mchange siyo Kamanda tena leo? Kweli siasa si hasa!

Kimbuga;Kumbuka siasa nazo zina zama zake,hakika Mchange alikuwa mzuri 2010 kulingana na mahitaji ya wakati ule lakini kwa sasa siasa zimemzidi upeo na ameishia kuondoa matumaini yake ya kisiasa na kuweka kwa mtu binafsi.
Nakumbuka uchaguzi mdogo uliopita wa diwani wa Kirumba-Mwanza nilikutana na Mchange na katika majadiliano alieleza jinsi inavyotakiwa kuendesha kampeni za kumchafua M/kiti wa CDM alipobanwa sana hakuwa na sababu ya msingi na hata nilimwambia mda huu na raslimali hizi ungezitumia kuimarisha chama na hasa Kibaha mjini ingesaidia chama na hata wafuasi wenu ila sio aina hii ya siasa haina msaada kwako.
Kifupi tu sio jembe tena.
 
Zitto celibate man tumweke ikulu ikulu sio ya wahuni, bado anahitaji kwenda club bado anatafuta mchumba. Afanye kwanza hayo na aacha undumila kuwili he will be considered not now!
By ze wei Lile hammer na Vogue kayatoa wapi vile?
Ebu wacha roho mbaya wewe Hammer na vogue ndio imekutoa roho, umeziona kwa Zitto tuu kwengine hukuziona?
 
kwa hali inavyokwenda sasa ni heri kutafakari, haya mambo naona yanazidi nia ya kugombea uraisi ipo kitu kubwa wengi hatuijui. I am still studing the saga. Demokrasia at its highest level, scrumble at its highest level. Tuatafika na aumivu yetu wote.

Chonde chinde wapenzi na wale wasio wapenzi wa Kijana wetu ZZK wote tumieni busara. Dr kitila ameita hii hali uliberali mchwara, mimi naita demokrasia kwenye iliyokomaa kwa mtoto mchanga. Chadema bado inakuwa na haijakomaa bado kama chama chenyewe hakijaweza kufika mikoa yote huo uraisi tunaotaka kutoana nao macho ni kiini macho.

Sifa zote wanazopeana wakubwa zingesaidia kama wangekuwa wanajenga mtandao wa kushinda, siasa za ushindi zinafanywa leo sio jana. Nyerere alimwata Mkapa Mr Clean miaka kumi baadaye Mkapa aligeuka jina na kuitwa fisadi. Chenge alikuwa mfanyakazi asiyejua kuiba miaka kumi baadaye kawa mzee wa vijisenti.

Kinachotufanya Watanzania kuwa masikini ni viongozi wetu kupenda vyeo badala ya kazi na wananchi. Kizazi cha sasa tujifunze kuwapenda wananchi, nchi yetu na sehemu tunazoishi.

Chadema haiwezi kushinda Uraisi 2015 kama vijana mliopata fursa ya kutuongoza hamtaacha tamaa na kuwa kitu kimoja kumtoa adui CCM. Badala ya kuazna kuteteana leo miaka mitatu kabla ya uraisi wenyewe. Nia kila mtu atoae matamko kila mtu atamke halafu tunawahitaji site, huwezi kushinda uraisi maelezo na huwezi kushinda uraisi kwa kazi ya mwaka juzi. Ushindi ni leo na ni sasa kamanda ni alyeko site sasa sio jana.

Chief Mkwawa wa Kalenga
Anawatakia wote kwenye makundi ya Uraisi ndani ya CDM waende site waache kelele.
 
Kimbuga;Kumbuka siasa nazo zina zama zake,hakika Mchange alikuwa mzuri 2010 kulingana na mahitaji ya wakati ule lakini kwa sasa siasa zimemzidi upeo na ameishia kuondoa matumaini yake ya kisiasa na kuweka kwa mtu binafsi.
Nakumbuka uchaguzi mdogo uliopita wa diwani wa Kirumba-Mwanza nilikutana na Mchange na katika majadiliano alieleza jinsi inavyotakiwa kuendesha kampeni za kumchafua M/kiti wa CDM alipobanwa sana hakuwa na sababu ya msingi na hata nilimwambia mda huu na raslimali hizi ungezitumia kuimarisha chama na hasa Kibaha mjini ingesaidia chama na hata wafuasi wenu ila sio aina hii ya siasa haina msaada kwako.
Kifupi tu sio jembe tena.

Mkuu nakushukuru kuweka wazi.Huyu jamaa matusi anayoporomosha Facebook akishirikiana na wengine dhidi ya Mbowe na Dr.Slaa ni aibu mpaka leo kujiita mwanachama wa CDM.
 
Nakubaliana na wanajamii walio na upeo wa kutosha. Kwamba rais wa 2015 atatoka chama gani au ana umri gani (kijana au mzee) si hoja. waTZ tunaomba Mungu atufumbue akili zetu ili tumchague mtu atakayekuwa mkombozi wetu hapahapa ili waTZ wote tuweze kufuta ujinga, maradhi na umaskini uliokithiri. Hali ilivyo kwa sasa inatisha viongozi hawawajui wala kuwathamini wanaowaongoza! Ni aibu kelele zote tunazopiga hata kustuka hawastuki! Kweli yataka moyo na safari bado ni ndefu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom