Urais wa Zitto 2015 ni kwa tiketi ya CHADEMA - Habib Mchange | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais wa Zitto 2015 ni kwa tiketi ya CHADEMA - Habib Mchange

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 12, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF

  ....Ifuatayo ni makala yaliyoandikwa katika gazeti la Raia Mwema na aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Kibaha Mjini-CHADEMA Habib Mchange na ambaye alikuja kugombea uenyekiti wa BAVICHA lakini akaenguliwa kwa madai ya Rushwa...Fuatilia.......  • Wengi tunampongeza kwa kusimamia vema mgawanyo wa majukumu
  • Ameweza kusimama kidete bungeni kutetea Watanzania bila kujali majimbo

  NIMESHAWISHIKA kuandika makala hii maalumu leo ili kuleta majibu fasaha kwa hoja zilizotokana na ama kutokuelewa au kuelewa dhana nzima ya ugombea urais 2015 kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

  Kwa mtazamo mwepesi, na hasa kwa mtu asiyeweza kunyambulisha mambo anaweza kushawishika na kuamini kuwa Zitto hana chama kitakachompa ridhaa ya kugombea urais mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa hoja za Mayege S. Mayage katika makala yake kwenye gazeti hili la Raia Mwema, toleo namba 262, ni kwamba tayari chama ambacho Zitto ni mwanachama mpaka sasa yupo mgombea urais.

  Yaani kwa lugha nyepesi, CHADEMA tayari wanaye mgombea wao na Watanzania wanajiandaa kumchagua huyo mgombea katika Uchaguzi Mkuu, 2015.

  Mayage hajaweka wazi ni mgombea gani huyo ambaye Watanzania wanamjua kupitia CHADEMA.

  Japo aliorodhesha sababu kadhaa za kwa nini Zitto hawezi kugombea na CHADEMA huku akijikanganya sehemu nyingi kwa kusema Kamati Kuu ya CHADEMA ndiyo itakayoamua nani agombee, lakini anajichanganya zaidi kwa kusema kila mwana CHADEMA ana haki ya kugombea kwa kuwa ni haki yake ya msingi.

  Pamoja na kutangaza maslahi yangu ya kisiasa kuwa mimi ni mwanachama hai na mtiifu wa CHADEMA, bila kuuma maneno nimsaidie kumjuza Mayega kuwa Zitto atagombea urais mwaka 2015 kupitia CHADEMA.

  Kupitia CHADEMA, Zitto atagombea urais na kupitia chama hicho hicho, ndipo naamini kuwa Watanzania tutaendelea kumuamini Zitto na kumuongezea majukumu kutoka ubunge hadi Rais wa tano wa Tanzania.

  Hoja ya kwamba Zitto hawezi kupitishwa kugombea urais kwa sababu hashiriki kwenye vuguvugu la mabadiliko, ni nyepesi na dhaifu mno.

  Zitto ndiye mwanachama pekee wa CHADEMA mwenye umri mdogo na kipato kidogo aliyeshiriki na anayeshiriki kukijenga chama chake, tofauti na umri na kipato chake.

  Niseme tu wazi kuwa CHADEMA ni zaidi ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), harakati za kukisambaza chama hiki kamwe hazikuanza na vuguvugu la mabadiliko na kamwe hazitaishia kwenye vuguvugu la mabadiliko, hata harakati za kukisimika chama hiki kwa wananchi hazikuanzishwa na walioanzisha vuguvugu la mabadiliko, M4C ni sehemu ndogo sana kati ya sehemu kubwa za uenezi na ujenzi wa CHADEMA.

  Chama imara cha upinzani huenezwa vema na mikakati yake ya kitendaji, kisera, kiutawala, usimamizi na utetezi wake kwa wananchi dhidi ya serikali na matukio yanayofanywa na chama tawala.

  Kazi hii mara nyingi hufanywa bungeni, hivyo basi wakati Mayege anamtaka Zitto akajisimike kwa wanaCHADEMA kupitia vuguvugu la mabadiliko, sisi wanaCHADEMA tunampongeza Zitto kwa kusimamia vema mgawanyo wa majukumu kwa kuendelea kusimama kidete bungeni kuwasemea na kuwatetea Watanzania bila kujali majimbo yao, kwenye hili sidhani kama Mayege anaweza kubisha.

  Ni Zitto huyu aliyetangaza kuutaka urais 2015 ndiye aliyerudisha matumaini ya Watanzania hasa vijana, kushiriki kwenye siasa, hususan siasa za upinzani.

  Baada ya Zitto kuingia bungeni mwaka 2005, vijana wengi walipata moyo na kujiona wanaweza na hawana sababu ya kusubiri kuzeeka ili wagombee ubunge.

  Sote tumeshuhudia na CHADEMA ambacho Zitto ni Naibu Katibu Mkuu wake kina wabunge vijana ambao baadhi wanaweza kukataa ukweli kwamba wao ni matunda na matokeo ya kazi nzuri ya Zitto ndani na nje ya Bunge.

  Kwa hili, kama Zitto aliweza kufungua njia ya ubunge kwa vijana, basi ana kila sababu ya ya kuwa rais kijana Tanzania.

  Ukweli una sifa ya kutokupendwa lakini ni lazima tuuseme tena mara kwa mara ili ueleweke na kumbukumbu ziwekwe sawa.

  Itakumbukwa mara baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime kuziba nafasi ya marehemu Chacha Wangwe, mwaka 2008, Zitto alikuwa kiongozi wa kampeni kuanzia mwanzo mpaka CHADEMA kikaibuka mshindi, CHADEMA kilianzisha harakati za ujenzi wa chama kwa wananchi kipindi hicho tuliita Operesheni Sangara.

  Yawezekana wengi hawajui, nitawaambia leo. Operesheni Sangara ilikuwa ni njia ya ujenzi wa chama na kukipeleka kwa wananchi kwa kutumia mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani kama unavyoona vuguvugu la mabadiliko hii leo.

  Operesheni Sangara, iliandaliwa, ilibuniwa na kusimamiwa kwa mara ya kwanza na Zitto Kabwe huyu huyu ambaye leo anautaka urais wa Tanzania.

  Zitto alianza Operesheni Sangara mikoa kadhaa ya Kanda ya Ziwa akiwa kiongozi na mbunifu wa operesheni hiyo. Operesheni hii ilianzia mkoani Mwanza ikaenda majimbo na kata zote za mkoa huo kisha kuelekea Mkoa wa Mara na kusambaa kata na majimbo yote ya mkoa huo.

  Kwa ustadi wa ajabu, operesheni hii ikachanja mbuga mpaka mkoani Mbeya na kuzunguka majimbo na kata zote za mkoa huo.

  Leo ukienda Mwanza utakuta wabunge watatu wa kuchaguliwa wa CHADEMA ambao ni Highnes Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje (Nyamagana) na Salvatory Machemli (Ukerewe), narudia haya ni matunda ya kazi, nguvu na akili za Ztto Kabwe na baadhi ya wanaCHADEMA.

  Na hata Mbeya walipokwenda hawakuishia hivi hivi maana kama si makosa ya kiutawala yaliyofanyika wakati wa uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini, mwaka 2008 na kusababisha Sambwee Shitambala aliyekuwa mgombea wa CHADEMA kuenguliwa, ama kwa hakika angeshinda.

  Na hata hivyo akili, nguvu na kazi ya Zitto leo imezalisha wabunge wawili wa kuchaguliwa mkoani Mbeya ambao ni Joseph Mbilinyi - sugu (Mbeya Mjini) na David Silinde (Mbozi Magharibi) nasisitiza haya ni matunda ya kuonekana ya Zitto Kabwe kwenye ujenzi wa CHADEMA, ambayo sina hakika kama Mayage anayajua ama ameamua tu kuyafumbia macho.

  Nje ya Operesheni Sangara na matunda yake, Zitto ndiye kiongozi pekee wa kitaifa wa CHADEMA ambaye katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu (ukiondoa Dk. Slaa ambaye alikuwa mgombea urais) alizunguka sehemu mbalimbali za nchi kuwanadi wagombea ubunge na udiwani.

  Nakumbuka nikiwa nagombea ubunge Kibaha Mjini, Zitto kwa gharama zake alikuja kuniunga mkono na kuninadi mbele ya wananchi wa Kibaha pale maeneo ya Mwendapole (kura zangu hazikutosha kutangazwa).

  Kesho yake Zitto akaenda kumnadi John Mnyika (leo Mbunge wa Ubungo), kisha Halima Mdee (leo Mbunge wa Kawe), mara nikawa namsoma magazetini kuwa yupo Mtwara, Musoma Shinyanga, Kahama, Geita, Mpanda mara Sumbawanga, kote huko kwa gharama zake na bila kujali naye alikuwa mgombea wa ubunge.

  Kwa lugha nyepesi, Zitto aligombea na kushinda ubunge kwa kampeni za wiki tatu tu na siku nyingine zote alishinda akizunguka kwenye majimbo ya wagombea wengine kuwaunga mkono na kuwaombea kura. Kwa kitendo hiki, ninaamini na nitaendelea kuamini kuwa kujenga chama ni zaidi ya M4C.

  Nasisitiza, vuguvugu la mabadiliko si kipimo cha ugombea wa urais kwa CHADEMA. CHADEMA ni zaidi ya M4C, na naomba nieleweke M4C haiwezi kuwa na mantiki yoyote kama chama hakitakuwa na wabunge wanaofanya vizuri bungeni kama anavyofanya Zitto.

  Hoja nyingine ya Mayege ni kuwa mgombea wa CHADEMA atapitishwa na Kamati Kuu. Hoja hii pia ni dhaifu tena dhaifu sana.

  Unawezaje kusema Zitto atagombea kwa chama gani kisha unasema atategemea kama atapitishwa na Kamati Kuu ya chama chake?

  Hoja yake hasa hapa ilikuwa ni nini? Anajuaje kama Kamati Kuu itampitisha Zitto awe mgombea?

  Mgombea urais wa 2015 wa CHADEMA ni lazima atokane na wananchi, CHADEMA ili kujitofautisha na CCM ni lazima impate mgombea ambaye hatokani na mawazo ya wajumbe wa Kamati Kuu, wasiozidi 30.

  Ni wanaCHADEMA wote kwa mikutano mikuu ya wilaya zao (convention) ndiyo wanaopaswa kumchagua mpeperusha bendera wao. Ni vema na muhimu mgombea wa CHADEMA akawa mali ya wananchi, hasa wanachama wa chini kabisa, na sio wajumbe wa Kamati Kuu pekee ambao ni wachache sana kuamua kwa maslahi ya wengi.

  Demokrasia bora na imara ni ile inayoruhusu ushindani na ushirikishi kwa walio wengi (nitaandika makala kuelezea namna bora ya kumpata mgombea bora wa vyama vya kidemokrasia kama CHADEMA).

  Kauli ya Mtei na umri wa Zitto

  Nikimnukuu Mzee wangu Edwin Mtei, mwasisi wa CHADEMA katika nukuu ya gazeti la Mwananchi anasema; "Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa (kugombea urais). Mimi nimemshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na si kukigawa wala kukivuruga.''

  "Dk. Slaa (Willbrod) anataka, Freeman anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua. Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.''

  Baada ya kumnukuu Mzee Mtei, kwa maoni yangu nadhani ni lazima sasa ifike kipindi wazee wetu watambue na kukubali kuwa wanapaswa kuwakabidhi vijana jukumu la ukombozi wa chama.

  Ni watu wavivu, waoga na wafitini pekee ndio wanaoweza kuamini kuwa kutangaza kugombea urais ni kukivuruga ama kuanzisha mgogoro kwenye chama.

  Lazima Mzee Mtei afahamu kuwa hizi si zama za wagombea kupita bila kupingwa, ni vema akaendelea kufahamu kuwa hizi si zama za wagombea wa urais kutumiwa timu ya kwenda kubembelezwa kugombea na mwishowe kuipa timu masharti ya kufanya ili agombee.

  Ni lazima sasa akubali na aelewe, demokrasia ni kushindana na demokrasia si kuachiana. Demokrasia ni kuchagua moja iliyo bora kati ya nyingi zinazoshindana. Demokrasia sio kupitisha moja iliyopo kati ya moja iliyojitokeza. Ni lazima sasa akubali kuwa chama kimekuwa.

  Unawezaje kusababisha mgogoro kwenye chama ambacho mpaka leo ni Zitto Kabwe peke yake ndiye ameshatangaza nia hadharani kuwa atawania urais?

  Kwa nini watu wanawasemea watu kuwa kuna watu wana haki ya kugombea urais na wengine hawana haki ya kugombea? Hatuhitaji mgombea urais anayesubiri kuombwa akagombee.

  Historia inaonyesha kuwa marais waliofanya vizuri ni wale walioonyesha nia, dhamira na uthubutu wa kuutaka urais mapema. Ni lazima mzee wetu akaelewa kwamba speed ya damu ya Zitto katika kufanya mambo ni tofauti sana na speed na uwezo wake.

  Nitamuunga mkono kijana yeyote anayeamini na atakayeshiriki kupigania kushushwa ama kuondolewa kwa kipengele cha umri kwenye Katiba. Ikitokea Zitto akasababisha kuondolewa kwa kipengele hicho, nitamuunga mkono ama yeyote yule akikisemea nitamuunga mkono pia.

  Kipengele cha umri hakina sababu ya kuwapo, hakisemi kwa nini mgombea urais awe na zaidi ya miaka 40, hakitoi hata uhusiano kati ya umri na uwezo wa kiongozi, inawezekana tumekirithi kutoka kwa wakoloni bila kujua sababu ya wao kukiweka.

  Kipengele cha kusema ili ugombee urais ni lazima uwe na miaka 40 na kuendelea ni sawa na kusema vijana wanaruhusiwa kupiga kura tu ya urais lakini hawaruhusiwi kugombea, ni sawa na kusema vijana wanaruhusiwa kuwa wapiga debe tu wa urais lakini hawaruhusiwi kugombea.

  Ni sawa na kusema wenye nchi hawaruhusiwi kujiongoza, hii ni kutokana na ukweli kwamba vijana Tanzania sasa wanavuka zaidi ya asilimia 60 ya idadi yetu. Hii ni kusema kwamba ikiwa vijana wote wakiamua kumpigia kura mtu mmoja basi huyo mtu atashinda kwa ushindi wa kimbunga.

  Kipengele hiki ni cha kibaguzi na kinawagawa Watanzania kwa rika lao, kwa umri wao na kinapaswa kiondolewe kwa sababu hizo. Ikitokea Zitto akapambana ili kiondolewe nitamwita mzalendo na mtetezi wa vijana na mpenda haki kwa watu wote.

  Urais si surprise

  Moja kati ya hoja dhaifu zinazompinga Zitto kugombea urais ni kwamba ametangaza mapema sana, bado wakati wake, eti sasa hivi mapema mno.

  Ndugu zangu, tunatakiwa sasa tuachane na urais wa kushitukiza, tuachane na marais wanaotangaza kugombea wiki tatu kabla ya kuanza kura za maoni ili kuficha maovu yao.

  Urais ni kazi inayotakiwa kufanywa na mtu anayeiweza. Na ili mtu aiweze ni lazima yeye mwenyewe ajione kama anaiweza hiyo kazi, na kama anajiona anaiweza hiyo kazi ni lazima awaambie mapema anaotaka kuwatumikia na wao wajithibitishie kuwa kweli anaiweza ama ataiweza.

  Mtu halazimishwi kuwa rais, mtu anatakiwa autake urais. Zitto amejipima na kuamini anauweza urais, hakufanya siri, akauambia umma Watanzania kuwa ukimtuma kuwa rais ataweza, ni jukumu letu sisi kumuandaa Zitto kuwa rais.

  Zitto hatakuwa aina ya mgombea wa kuzuia chama kisipite bila mgombea, atakuwa mgombea wa kuushinda urais na kuwa rais. Kwa sababu anaamini anauwezo. Naamini anaweza. Urais si suala la kumpima mtu kwa siku 76 za kampeni. Zitto ametangaza kuutaka urais, tumsaidie kumshauri tunapoona panafaa na tumuonyeshe njia inapofaa.

  Mwandishi wa makala haya, ameandika kumjibu mwandishi Mayage S. Mayage aliyeandika makala ya uchambuzi kuhusu uamuzi wa Zitto kutangaza kuwania urais 2015.  Chanzo: http://raiamwema.co.tz/urais-wa-zitto-2015-ni-kwa-tiketi-ya-chadema
   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mchange ndio nani?
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  katiba mpya kwa hali iliyopo na muda haiwezekani kukamilika kabla ya 2015,na katiba iliyopo mpaka sasa hairuhusu zitto kugombea.
  kwa nini tunatumia nguvu kubwa kupiga risasi wakati adui hatujamfikia je tukijamkuta si tutakuwa tumemaliza risasi.
  please ziito tulia tushughulikie katiba kwanza au unataka tuamini kuwa unatumika.
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,297
  Likes Received: 13,007
  Trophy Points: 280
  Kuna watu huwa wanataka umaarufu usio na tija we katiba yenyewe hairuhusu sasa why disturb us na utakaji wa uraisi wakati bado miaka mitatu mbele?
  Hivi huwa mnasoma shule gani nyie mbona hata ambao hatujasoma sana twawazidi kasomeni katiba na pia nahakika hatakuwa raisi huyo Zitto

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Huyu si yule KAMANDA wa Kibaha aliyepambana na Kweka na watu wakasema Kweka alichakachua?

  Makundi ndani ya vyama vya siasa ndio chakula cha ubongo wa kisiasa.
   
 6. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  We subiri utaona vilaza wasio na hoja wataanza kufanya personal attack kwa mtoa maoni badala ya kuangalia uzito/ wepesi wa hoja zake.
  Binafsi nakubaliana na maoni aloyatoa Mchange.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hujui kuna mchakato wa kuandika katiba upya na vijana wanataka umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40? Hujui kwamba ahadi ya Rais JK ni kwamba katiba mpya itapatikana kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015? Ikiwa hivyo na bahati nzuri umri ukapunguzwa hadi miaka 40 basi Zitto atakuwa ndani ya wigo.
   
 8. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Zitto celibate man tumweke ikulu ikulu sio ya wahuni, bado anahitaji kwenda club bado anatafuta mchumba. Afanye kwanza hayo na aacha undumila kuwili he will be considered not now!
  By ze wei Lile hammer na Vogue kayatoa wapi vile?
   
 9. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hii sichangii, naogopa kupigwa Ban!
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mungu atuepushe na udini na makundi ndani ya chadema....................................
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna hoja ya tani moja japokuwa si Zitto peke yake anayefanya vizuri bungeni kupitia CDM lakini kama wabunge wote watafanya vizuri bungeni basi huo ni mtaji wa kisiasa tosha kwa CDM. Nadhani jamaa huenda alikuwa anataka kukumbusha jinsi ambavyo wabunge wa CDM walivyomtupa mkono Zitto kwenye hoja yake ya kupinga posho za vikao!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mungi huwezi kuepuka makundi ndani ya Chama ama kusanyiko lolote lile. Chama cha siasa ama chama cha aina yoyote ile ni mkusanyiko wa vikundi vidogo vidogo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyu Mchange jina lake liliondolewa kugombea uenyekiti Bavicha alipokamatwa akigawa rushwa kama njugu kupitia mtandao.
  Pia huyu ndiye mara nyingi kwa kutumia facebook akishirikiana na mtu anayejiita Said Kulwa na Juliana Shonza wamekuwa wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi wakuu wa chama Dr Slaa,Freeman Mbowe na John Heche.Matusi wanayotukana hayandikiku
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo unataka kutuharibia thread.
   
 15. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  fmpiganaji Katiba itakamilika mapema 2 na itamruhusu ZITTO kugombea. Hata kama itakuwa bado na kama ambavyo tumesikia hata lile jukwaa la CHADEMA linavyolumbana na kamati ya maoni ya Katiba mpya , lazima tu uchaguzi wa 2015 utaongozwa na sheria mpya aidha kutokana na Katiba mpya au kwa kufanyia marekebisho baadhi ya vipengele na nadhana kipengele cha umri kitakuwa kimojawapo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Watanzania tutaelimika lini? Zitto kabwe umri haumruhusu kugombea urais kwa katiba iliyopo,kwa nini mawazo yenu yanatekwa na mtu anayetafuta kutengeneza historia isiyokuwa na maana.After hata kama katiba itabadilishwa,ni akili gani inayowashawishika kirahis kiasi hicho kwamba nchi hii ni ya kukabidhi mtu ambaye haeleweki? Hamjajifunza kutokana na makosa mliyofanya kwa kikwete rais dhaifu kupata kutokea katika nchi yetu! Watanzania lazma tujue kwamba jk ametufundisha kuwa urais si mrahisi kiasi kwamba yoyote anauweza.Mjifunze basi nyie mnaoshabikia bila kufikiria
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Molemo huyu Mchange siyo Kamanda tena leo? Kweli siasa si hasa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mkuu hao ndo wale wanaoamini CDM ni MBOWE na SLAA.
   
 19. S

  SEBM JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakati mwingine nasemaga huwa kuna watu hawana hekima na busara kabisa. Hivi huyu Mchange anaamini katika hicho anachokisema au ni propaganda tu?

  Inamuingia akilini mtu kuamini kuwa Zito ndo mwana CHADEMA pekee mwenye umri mdogo kuliko wote aliyeshiriki katika kukiimarisha chama chake. Joshua Nassari na wengineo watakuwa na umri gani? Wanachama wengine wa kawaida ambao kuchakutwa wako kwenye harakati za chama, wanakitetea chama, wanashiriki M4C, hao hawakuzi chama?

  Ni kweli kuwa Zitto ana kipato kidogo kuliko wote CHADEMA? Akiwa mchumi kwa taaluma, amefanya ulinganifu kwa kujifananisha na nani? MH. Zitto vs Mh Natse (anayesafiri kutoka Karatu kwa Dar Express yenye nauli ya Tsh 34, 000?). Au ni Mh Zitto vs John Mnyika (yeye ana magari ya kifahari, mwenzake anatembelea VITZ)?

  Ukweli ni kwamba, Habib Mchange na wengineo wengi wanaojaribu kuleta chokochoto katika CHADEMA, kamwe hawatofanikiwa. CHADEMA ni zaidi ya Zitto, Mbowe, Slaa, Mchange, Shonza, Nyakarungu n.k
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,528
  Likes Received: 5,674
  Trophy Points: 280
  Wanaodhani wengine tunaipenda tu Chadema (kama makada wa CCM walivyo) wanakosea sana,akina Habib Mchange ni mmojawapo wa watu wanaodhani Chadema imefika hapo pa kupendwa tu.

  Sina muda wa kujadili hoja zake dhaifu lakini namtahadharisha kuwa Watanzania tunataka mabadiliko kwa namna yeyote,Watanzania watampa nafasi yule waliyenae mtaani kila siku akiwatetea kwa moyo mmoja bila hila,Watanzania wanataka mtu safi na kiongozi aliyekomaa kwelikweli na amedhihirisha hivyo kwa vitendo na si kwa simulizi zake kutuambia aliyofanya kama vile sisi ni vipofu!

  Hawa akina Mchange wasameheni tu ni vijana wadogo wanaodhani wameshakomaa kisiasa na sifa zinawaharibu sana.Someni makala hiyo muone kama kuna kijana aliyeiva hapo!!!
   
Loading...