GE2025 Urais wa Tanzania ni mpango wa Mungu, kubalini tu Samia amepewa tiki

GE2025 Urais wa Tanzania ni mpango wa Mungu, kubalini tu Samia amepewa tiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Yawezekana kweli hatutapata kama huyu, lakini atabakia kwenye historia kama Rais aliyepiga kazi sana. Muangalie kwenye miundombinu, mahospitali kwenye sekta ya afya na utalii.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
downloadfile-39.png
 
Naunga mkono hoja, Thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

P
Mpango wa Mungu ulikuwa ni kipindi anachokiangalia sasa hivi kuhesabu tangu kifo cha Magufuli. Baada ya muda huo hawana kwani kuna vitu vingi kalazimisha sana, mazabe yamekuwa mengi tena yenye gharama zisizo lipika.
 
Jamaa una roho ngumu wewe.

Hivi Magufuli ulikuwa ukimchukia kwa sababu gani ?
Magufuli ndiye mwanzilishi wa uozo wote tunaopambana nao sasa hivi kuanzia kukandamiza demokrasia, kuingilia Mhimili wa Mahakama, kumiliki WASIOJULIKANA kwa ajili ya kuteka na kuua, kuweka bunge butu lenye COVID-19, kuharibu chaguzi za 2019 na 2020.

Kama asingeanzisha haya Tanzania ilikuwa inaelekea kuzuri kwenye demokrasia iliyokamaa na utawala bora
 
Alikatiwa maslahi huyu jinga siunawaona wakina zitto kabwe, Fatuma karume, Bashe na mafala wengine kama kina Lusungo yapo kimya kama hamna kinachoendela Tanzania wakati enzi ya Magu yalikuwa Frontline.
Na wewe umekatiwa masilahi yako na Samia kwa sasa? Ndiyo maana unabweka??
 
Ncha ya Mkuki haipigwi kwenzi! Kuna watu walifikiri Samia ni dhaifu, wangemwendesha kama mwanasesere. Wakajidanganya kwamba hakustahili kuwa Rais. Samia ni Rais kwa Matakwa ya Mungu na atabaki hapo kwa muda mpaka Mungu akipenda na siyo akina Polepole na wahuni wenzie walivyotaka!

Kila jambo ni mpango wa Mungu kwenye haya maisha. Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo na inakuwa.

Kuna watu walikuwa maarufu sana (Lyatonga, Membe, Lowassa, Mtikila, Maalim Seif) kuliko hawa akina Januari, Lissu, Majaliwa, Mwigulu, Gwajima. Lakini wamekufa hawakupata uRais wa Tz

Kuna matakwa ya tume na matakwa ya Mungu
Usimchanganye Mungu kwenye mambo ya ajabu
 
Magufuli ndiye mwanzilishi wa uozo wote tunaopambana nao sasa hivi kuanzia kukandamiza demokrasia, kuingilia Mhimili wa Mahakama, kumiliki WASIOJULIKANA kwa ajili ya kuteka na kuua, kuweka bunge butu lenye COVID-19, kuharibu chaguzi za 2019 na 2020.

Kama asingeanzisha haya Tanzania ilikuwa inaelekea kuzuri kwenye demokrasia iliyokamaa na utawala bora
Hapa nakubaliana na ww, he is the source, the blue print,
Chama kinafuata script ile ile
 
Magufuli ndiye mwanzilishi wa uozo wote tunaopambana nao sasa hivi kuanzia kukandamiza demokrasia, kuingilia Mhimili wa Mahakama, kumiliki WASIOJULIKANA kwa ajili ya kuteka na kuua, kuweka bunge butu lenye COVID-19, kuharibu chaguzi za 2019 na 2020.

Kama asingeanzisha haya Tanzania ilikuwa inaelekea kuzuri kwenye demokrasia iliyokamaa na utawala bora
Kwa hiyo Samia unamuunga mkono na haya maovu yake ? Wewe jamaa una roho ngumu kwako damu za watu si kitu kabisa aiseeh sijapata kuona
 
Kuna matakwa ya tume na matakwa ya Mungu
Usimchanganye Mungu kwenye mambo ya ajabu
Kwani Rais wa sasa nani? Nyie kuna wakati mmezusha kuwa uchaguzi hautafanyika, mara Samia atajiuzulu, mara Samia kakimbilia Uganda, mara Samia atakufa kabla ya uchaguzi. Kikowapi sasa??
 
Kwa hiyo Samia unamuunga mkono na haya maovu yake ? Wewe jamaa una roho ngumu kwako damu za watu si kitu kabisa aiseeh sijapata kuona
Sijaunga mkono uuaji na utekaji unaofanyika, sijaunga mkono pia ukandamizaji wa haki za kikatiba. Bali nimeunga mkono kazi kubwa aliyofanya kututoa kwenye uhayawani ulioanzishwa na Magufuli, japo hajaweza kuumaliza
 
Kwani Rais wa sasa nani? Nyie kuna wakati mmezusha kuwa uchaguzi hautafanyika, mara Samia atajiuzulu, mara Samia kakimbilia Uganda, mara Samia atakufa kabla ya uchaguzi. Kikowapi sasa??
Nyie akina nani?
si kila anaekosoa yupo group fulani

Kwa taarifa yako hata ww leo gov ikiamua wanakuweka kuwa rais unakuwa. Does that mean ni kipango ya Mungu?

Hell no
 
Nyie akina nani?
si kila anaekosoa yupo group fulani

Kwa taarifa yako hata ww leo gov ikiamua wanakuweka kuwa rais unakuwa. Does that mean ni kipango ya Mungu?

Hell no
Soma Warumi 13: 1-6
 
Back
Top Bottom