GE2025 Urais wa Tanzania ni mpango wa Mungu, kubalini tu Samia amepewa tiki

GE2025 Urais wa Tanzania ni mpango wa Mungu, kubalini tu Samia amepewa tiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tunajua Samia ni mtu mzuri sana.
Lakini nani anamshauri kuwa utekaji ni jambo jema na litaendelea miaka yote?

Ni
Suala la utekaji amelikuta kuanzia akina Ulimboka 2012, Mwangosi 2015, Ben Saanane 2016 etc

Pengine ni culture ya CCM
 
Huyu Bosi wako amekosa kibali Mbinguni na Duniani! Na ushahidi mdogo tu ni haya matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya wakosoaji/wapinzani wake, na pia rushwa isiyo na kificho.

Na akiendelea kulazimisha, basi matokeo atayaona siku si nyingi. Asome historia ya watu waliojivika ukaidi kama huu wa kwake, na aone matokeo yake yalikuwaje!
Mkuu hizi sentensi zako za maapizo nimekuwa nazisoma kuanzia mwaka 2022. The more unamuombea mabaya, the more Mungu anam imarisha
 
Hili jamaa wakati wa magufuli lilipokuwa linalalamika utafikiri linaakili timamu kumbe ni jitu binafsi linalopigania masilahi yake na genge lake ,Sasa hivi linasifia ujinga na kulazimisha watu waunge mkono hata mambo ya kijinga
Usiishi kwa kukariri. Magufuli nilimpiga vita kwa vile ndiye chanzo cha uozo huu wa kutekana na kuua na kuharibu demokrasia.
 
Yaani mkuu ulivyokuwa unamnanga jiwe na sasa kindakindaki kwenye kutetea uovu wa uongozi wa sasa.... Duh!
 
Samia ni Rais kwa Matakwa ya Mungu na atabaki hapo kwa muda mpaka Mungu akipenda na siyo akina Polepole na wahuni wenzie walivyotaka!
Huyo n "Mungu" uliye naye mfukoni kwako; sis sote hatuwezi kukubaliana na mungu wa kishetani kiasi hiki cha kuleta mtu kama Samia kuongoza nchi hii.
 
Usiishi kwa kukariri. Magufuli nilimpiga vita kwa vile ndiye chanzo cha uozo huu wa kutekana na kuua na kuharibu demokrasia.
Kwa hiyo sasa hivi unaunga mkono uozo alioanzisha jiwe?
 
Kuna watu walifikiri Samia ni dhaifu, wangemwendesha kama mwanasesere. Wakajidanganya kwamba hakustahili kuwa Rais. Samia ni Rais kwa Matakwa ya Mungu na atabaki hapo kwa muda mpaka Mungu akipenda

Kila jambo ni mpango wa Mungu kwenye haya maisha. Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo na inakuwa.
Naunga mkono hoja, Thread 'Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!' Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

P
 
Yaani mkuu ulivyokuwa unamnanga jiwe na sasa kindakindaki kwenye kutetea uovu wa uongozi wa sasa.... Duh!
Nilikuwa namnanga kwa sababu ndiye ailyeleta huu uovu wa kuteka na kukanyaga demokrasia. Ila Samia alikuja na 4R akawarudisha akina Lissu na Lema toka ukimbizini, akafungulia mikutano ya siasa, akawapa ruzuku na kufuta kesi zote za kubambikiza.

Kinyume chake akina Lissu wakadhani ni mnyonge wakaanza kumbeza nankumpeleka puta. Waache wacheze muziki wa mama. Goddammit
 
Huyo n "Mungu" uliye naye mfukoni kwako; sis sote hatuwezi kukubaliana na mungu wa kishetani kiasi hiki cha kuleta mtu kama Samia kuongoza nchi hii.
Huna namna, kuwa mpole mpaka 2030
 
Kwa hiyo sasa hivi unaunga mkono uozo alioanzisha jiwe?
Siungi mkono mtu kutekwa na kuuawa, ila naunga mkono namna Samia alivyopambana na waliokuwa wanambeza.

Mbona akina Polepole wasifanye haya wakati wa Magufuli???
 
Ncha ya Mkuki haipigwi kwenzi! Kuna watu walifikiri Samia ni dhaifu, wangemwendesha kama mwanasesere. Wakajidanganya kwamba hakustahili kuwa Rais. Samia ni Rais kwa Matakwa ya Mungu na atabaki hapo kwa muda mpaka Mungu akipenda na siyo akina Polepole na wahuni wenzie walivyotaka!


Kila jambo ni mpango wa Mungu kwenye haya maisha. Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo na inakuwa.

Kuna watu walikuwa maarufu sana (Lyatonga, Membe, Lowassa, Mtikila, Maalim Seif) kuliko hawa akina Januari, Lissu, Majaliwa, Mwigulu, Gwajima. Lakini wamekufa hawakupata uRais wa Tz


Sasa unajuaje kama pia Mungu hajampangia kuondoka hiyo tarehe 29...!!?
 
Back
Top Bottom