Urais wa Dkt. John Pombe Magufuli kuendeleza Wilaya ya Chato unatufundisha nini?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Unatufundisha mtu kwao,

Kwa muziki huo Marais waliopita walishindwa kuendeleza makwao kiuchumi na hata kimiundo mbinu, Leo Chato imepaa, kuanzia Mwinyi hadi Kikwete kama wangekuwa kama huyu, tungelishakuwa na miji iliyonawiri kama mikoa mitatu na huu wa nne.

Nawasihi viongozi mliobaki mfuate nyayo za Rais Magufuli, Mawaziri na wengine mkae mkijua kuwa mtu kwao,sio mnanunua mashamba na viwanja kwa ajili ya matumbo yenu,tunahitaji kuona mnayafanya kwa ajili ya miji yenu.

Ukiangalia watu wenye furaha leo ni kutoka Chato na wanatembea kifua mbele,angalia anakotoka makamo wa Raisi angalia anakotoka Waziri Mkuu na hata mawaziri wengine kama wa afya hakikisha unakotoka unajenga Hospital nzuri ya mkoa au japo iwepo wilayani kwako au wilaya yenye umeme wa uhakika.

Hongera sana Mheshimiwa Magufuli unaonyesha uongozi ulio na dira.
 
Chato oyeeee!!!

Oyeeee!!

Chato safiiiiiiii!!

Safiiiiiii!!!

Nawashukuruni sana ndugu zangu kwa kunisikiliza .Naunga mkono hoja kwa 100%
 
Kinachoshangaza hata baadhi ya Viongozi wakongwe wakipata fursa ya kuongea wanaishia kusifia tu awamu hii wala hizi kasoro hawazioni.

Hakuna anayekataa kwamba kuna maeneo yanatia moyo lakini tusisahau kuhoji yale yanayokwenda hobela hobela....na yapo.
 
Mawazo ya kimasikini sana haya, toka kwa watu masikini. Huwezi kusikia mawazo (au kuona mambo) kama haya kule duniani upepo wa neema unakotoka.
 
Chato inasemwa sana kwa sababu tu anatoka Mkuu wa Nchi. Lakini kuuhalisia Mikoa na Walaya mpya zilizopandishwa hadhi. Miradi ya miundo mbinu inayoendana na mabadiliko hayo inaendelea. Mf. Mkoa mpya wa Njombe una miradi ya Hospital ya Rufaa, Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wilaya Njombe Mjini na Wanging'ombe, Ujenzi wa Soko kuu, Ujenzi wa Barabara za lami kuunganisha wilaya na Upembuzi yakinifu Ujenzi wa Uwanja wa Ndege umeanza.

Geita kama Mkoa Mpya na Chato kama Wilaya Mpya lazima kuwe na miundo mbinu kama hiyo.
 
Hii hoja yako sijapendezwa nayo, Tanzania ni ya watanzania wote na sehemu zote zinatakiwa kuwe na maendeleo
 
Koma wewe. MARA ndo kila kitu mpaka leo mijitu na akili zao inaenda kuhiji Butiama kijijini. Wenyewe mnaiita wilaya ajii ya kipato.

Nyerere aliendeleza Mkoa muzima na majirani zake wa level ya kimkoa. Kifupi kanda ya Ziwa ilistawi sana including Chato!
Akawajaza mawazo mliobaki mpaendeleze bila nyie kujijua.

Na bado Dunia yote inaenda na itaenda hija Butiama sababu panafikika kirahisi na yeyote utokeee popote Duniani..

Asa huyu anaangalia kasehemu kamoja tuu ka kijiji kamoja tuuuuu! Tena kadooogo! Eti chato? Eti anaweka kakiwanja ka ndege! Mnamuona mujanjaaaa!

Kachato kaleee! Kabafikika kwa shida sana. siyo sifa! Nisawa na kujenga mghorofa uswahilini pasi barabara kwenye majirani shida wakabaji nana atapanga???.

Raha ya mghorofa jenga bwana! Uweke masaki.kariakoo. Sinza upangank. Yaani utakufa unatabasamu!

Siyo eti ujenge, kwamfuga mbwa. maji matitu???? Apange nani huko??? Kwanza kufika huko tyuu!

Hako ka Chato katasahaulika soon!!! wee subiri tu! Atoke! Hao wazee walio mshauri hawana akili

Angekuwa mwamba kamili km angepiga kwa umaridadi kanda nzima yote ile! Burigi aiunganishe na serengeti kiaina yaani watalii wakipitapita wanajikuta burigi Zamani za mkoloni kanda yooote! ilikuwa wilaya moja tu!

Ili atembee kifua mbeleeee! Chato iwe katikati ya ufahari. akitoka na ndinga km kadhaa watu waone utukufu wake.

Anayo fanya huyu rais Ni sawa na baba mwenye nyumba mbinafsi Punguani eti analala pazuri na anakulia chakula kizuri chumbani kwake anajiona mjanja then anakatiza sebureni kwa maringo! Kwenda kazini.

Vitoto vyake vinamuangalia huku vikiwa na njaa! Na vichache vinamshangilia baba huyoooo! Huku vina njaa! Siyo akili nzuri hiyo!
Raha ya nyumba kubwa na nzuri yenye matunzo jibu ni
watoto.
Mke.baaaasi.
Hao wageni watafuata bidaye. Lkn familia yangu kwanza iwe na furaha. Na familia ya jiwe ni kanda nzima ile.

Siyo ka kijiji ka chato tu yaani hata dege lolote km la Abiria.la mizigo hata la Rais likikosea tu kutua Bahati mbaya bado liwe nasehemu salama mlemle maeneo ya kidharula kwenye eneo maalum la kwao linatua kwingine.

Na hii ingefanya kanda ya ziwa iwe njia salama ya anga kutoka kaskazini na kusini mwa Dunia.hela tungepiga ndefu mpaka wazungu wangetuonea wivu!

Rais lazima afikirie kwa mapana na marefu siyo hii akili km ya Mleta mada upo?
 
Inatufundisha ukiwa waziri wa fedha, una waambia mawaziri wa ki secta, waweke miradi ya kimaendeleo kwenye jimbo lako, na mashirika ya ki sector, unachagua wajumbe wa bodi, unaofahamiana nao, una peleka trainning watu wa jimbo lako, na kuwapa kazi katika mashirika hayo, hata mtu akiwa mwalimu, anaweza kuwa afisa utumishi/ trainning officer, na kuwa ana kupa taarifa za ndani na watu wasio wa jimbo lako
 
Sisi wa Kilimanjaro tuna furaha wakati wote!

Hata wanasiasa wanatuheshimu.
Ukisikiaga watu wana sifa za kijinga wapo kilimanjaro. wilaya za mkoa wa kilimanjaro zina maendeleo gani? Hakuna wilaya hata moja ina hadhi ya mji. wilaya ya Rombo imedoda pale, wilaya za Hai na Siha bado ni miji midogo hata havijajengeka bado. Wilaya ya Mwanga mji ni bora hata makao makuu ya Tarafa na Same mpaka leo ina benki moja NMB, mji umedoda hakuna maendeleo ya maana. kwa watanzania msioufahamu huu mkoa mtadanganywa sana. Tatizo lao wana midomo sana na sifa za kijinda.
 
Haya mambo si yakushabikia,katika karne hii tulitegemea kuwa na kiongozi atakaye itazama zaidi Tanzania kwa mapana na marefu.

Tanzania kama taifa siku hizi tumeanza kuzungumzia ukabila,ukanda na pengine udini. Hili jambo halina afya katika mustakabli wa taifa letu wote kuanzia kusini,kaskazini,mashariki,magharibi na kati. Ni bahati mbaya sana katika siku hizi za karibuni Chato imekuwa ikitajwa ungefikiri labda ni Mkoa au makao makuu ya nchi. Chato ni sehemu ya Tanzania ambayo inastahili kupatia maendeleo kama sehemu nyingine za nchi.Tatizo ni hiyo kasi iliyopitiliza ukilinganisha na sehemu nyingine za JMT.

Upendeleo wa maendeleo kwa sehemu wanakotoka viongozi kutaweka precedence mbaya kwa viongozi watakao fuata baadae.Matokeo yake sehemu ambazo hazitabahatika kutoa viongozi zinaweza kubaki nyuma.
 
Back
Top Bottom