2mbaku
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 316
- 67
HARAKATI za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimeingia katika hatua mpya baada ya kuvuja kwa taarifa za kuwapo mkakati wa kuwapa nafasi wanasiasa wanawake na kuwatosa wanaume kwa kile kinachodaiwa kuvunja makundi yenye uhasama.Habari za ndani ya makundi makuu ya wataka urais ndani ya CCM, zimethibitisha kuwapo taharuki kubwa miongoni mwao baada ya taarifa za wanawake kupewa nafasi kubwa kuzidi kushika kasi siku zinavyozidi kwenda.
Wataka urais wanaolengwa kuzimwa ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wanawake wanaotajwa kufanikisha mpango huu ni Dk. Mary Nagu, Prof. Anna Tibaijuka na Dk. Asha Migiro ambao wote watasukumwa na makundi yenye fedha nyingi ili angalao wawili kati yao waingie hatua ya mwisho.
Kutokana na nguvu ya CHADEMA na kile kinachoonekana kwa wana CCM wenye ushawishi mkubwa kuogopana kwa sababu mbalimbali, kuna mkakati wa kuwa na 'plan B' ya kusimamisha wanawake, mkakati kama uliotumika kumzima aliyekuwa Spika wa Bunge, Samwel Sitta.
Source: Tanzania Daima
Kazi kwelikweli! Je hii plan B itafaulu?