Uraibu wa ngono

Uraibu wa ngono

Nafarijika sana kuona kuwa, kuna ambao walikuwa huwa na uraibu wa picha na video za ngono lakini wanaamua kutoka ingawa mara zote kuna vishawishi vya kuwarudisha huko. Kama zilivyo nyingi SITES za Pornography, hali kadhalika zipo pia nyingi SITES za kusaidia kuacha mambo hayo, hivyo mara zote kinachobaki ni kimoja tu.. MAAMUZI YA KIPI UNASOMA AU KUANGALIA!!

Lakini hivi karibuni kuna jambo ambalo nimeligundua. Mimi ni mdau mkubwa sana wa HADITHI na SIMULIZI ZA SAUTI!! Huko awali, hakukuwa na wimbi kubwa la simulizi zenye maudhui makubwa ya NGONO NGUMU!!

Lakini sasa hali sio ya kawaida!! Kuna utitiri wa SIMULIZI ZA SAUTI pamoja na tungo nyingine za maandishi ambazo ni NGONO TUPU!!! Hizi zinapatikana kwa wingi mitandaoni hasa Youtube na pia katika majarida mbalimbali.

Napenda sana kushauri kuwa, Ikiwa ulikuwa na uraibu wa picha na video za NGONO, na umeamua kuanza "Kujitibu", ni busara sana kuzikwepa simulizi hizi chafu. Uwepo wake hasa kwa lugha ya kawaida kabisa ambayo inatumika kila siku katika mazingira yetu unaamsha hisia zaidi ya mara mbili kuliko zile za kizungu tulizozoea na matokeo yake nadhani tunayafahamu..
Kweli kabsa yan ukisoma izo adith unaamsha popo kabisa
 
Back
Top Bottom