URAIA wa waikulu mbona utata mtupu?

Status
Not open for further replies.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Sijui ni tanuru lipi hupitia kuchekecha uraia halisia wa viongozi wetu na matokeo yake utata na minong'ono haiishi.

Mzee kifimbo wako wanaamini hakuwa raia pia Mzee wa zama za uwazi na ukweli ni msumbiji na sasa hapa kazi tu wanadai ni mrundi.

Sijui mbichi na mbivu zikoje lakini ni utaratibu upi huwa tunautumia kuhakiki uraia wa wanaikuku?

Isije kuwa raia wasio na hatia ndiyo wanatumbuliwa na mamluki.

Isije kuwa wanatumbuliwa vyeti feki na raia feki kwa maana si raia wa kuzaliwa kulingana na sheria za nchi hii na tunawalamba miguu na kuwatetemekea wazamiaji.

Isije kuwa nchi haijawahi kuongozwa na mtanzania mzawa ila wazamiaji ndiyo wanatutesa.

Katika wanaikulu wote sijasikia Mzee rukhsa au Mzee wa ari mpya na kasi mpya uraia wao ukitiliwa mashaka kwa sababu hauna utata.

Wakati wa ukapa wako raia walifutiwa uraia na kuagizwa wakajiandikishe upya na utawala uliokuwa ukiongozwa na muikulu mwenye uraia tata.

Au ilikuwa kombe mfukuzie mwanaharamu ili shetani apite.

Unapoona kiongozi anazungumzia baba lakini ndugu wa baba au hata kijiji alichokuwa akiishi hakijulikani basi hapo hoja za kuwa baba yake alikuwa mkimbizi kutoka Burundi zinapoanza kushika kasi na kuwa na mashiko machoni pa jamii.

Hivi swali langu bado liko pale pale hivi huyu ni mwenzetu kweli au ni raia feki?

Mwenye majibu ya ukweli ni vyema akatuelimisha
 
Mmhhh kama kuna kitu unataka kusema lkn unasita. Hebu funguka zaid. Huyo babamtu tuelezee zaid
 
Eti wanadai Tanzania imewahi kuwa na rais mmoja tu raia wa Tanzania ambaye ni Jakaya Mrisho Kikwete, eti kumbe hata awamu ya pili uraia wake una mashaka.
 
Mmhhh kama kuna kitu unataka kusema lkn unasita. Hebu funguka zaid. Huyo babamtu tuelezee zaid
Babamtu alikuwa akiishi kijiji gani kule Bukoba? Labda tuanzie hapo na ndipo majibu ya uhakika yatapatikana. Kudai alifia na alizikwa bukoba mjini siyo uthibitisho wa uraia ila inaongeza kasi ya kuhisi kwanini hakuzikwa kijijini kwake?

Na Bukoba mjini alizikwa na nani kama siyo na halmashauri ya Bukoba mjini?
 
wew
Sijui ni tanuru lipi hupitia kuchekecha uraia halisia wa viongozi wetu na matokeo yake utata na minong'ono haiishi.

Mzee kifimbo wako wanaamini hakuwa raia pia Mzee wa zama za uwazi na ukweli ni msumbiji na sasa hapa kazi tu wanadai ni mrundi.

Sijui mbichi na mbivu zikoje lakini ni utaratibu upi huwa tunautumia kuhakiki uraia wa wanaikuku?

Isije kuwa raia wasio na hatia ndiyo wanatumbuliwa na mamluki.

Isije kuwa wanatumbuliwa vyeti feki na raia feki kwa maana si raia wa kuzaliwa kulingana na sheria za nchi hii na tunawalamba miguu na kuwatetemekea wazamiaji.

Isije kuwa nchi haijawahi kuongozwa na mtanzania mzawa ila wazamiaji ndiyo wanatutesa.

Katika wanaikulu wote sijasikia Mzee rukhsa au Mzee wa ari mpya na kasi mpya uraia wao ukitiliwa mashaka kwa sababu hauna utata.

Wakati wa ukapa wako raia walifutiwa uraia na kuagizwa wakajiandikishe upya na utawala uliokuwa ukiongozwa na muikulu mwenye uraia tata.

Au ilikuwa kombe mfukuzie mwanaharamu ili shetani apite.

Unapoona kiongozi anazungumzia baba lakini ndugu wa baba au hata kijiji alichokuwa akiishi hakijulikani basi hapo hoja za kuwa baba yake alikuwa mkimbizi kutoka Burundi zinapoanza kushika kasi na kuwa na mashiko machoni pa jamii.

Hivi swali langu bado liko pale pale hivi huyu ni mwenzetu kweli au ni raia feki?

Mwenye majibu ya ukweli ni vyema akatuelimisha
mmh we! unaongea nini unajipenda au hujipendi acha kuongea makubwa hayo utapotea shauri yako. usichokoze nyuki kwenye mzinga utang`twa
e
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom