Uraia pacha hauna ubaya wowote.
Hakuna Hasara ya uraia wa nchi mbili. Watu tunaowaongelea wengi ni raia wa Tanzania kwa sasa wengi wamezaliwa Tanzania na watoto wao. Watanzania wengi sana wazawa wapo nje kutafuta maisha na wakati mwingine ni muhimu kuchukua uraia wa nchi wanaoishi kwasababu ya familia na mafao yao ambayo mengi yanaenda Tanzania. Mfano hapa USA sijaona tofauti ya uzalendo kwa watu wenye Dual na wasionao na sijaweza kujua kwasababu wote wana mapenzi sawa kwa nchi kwa mtazamo wangu. Ghana na Nigeria wanao Dual na Ghana hasa imewasaidia sana kwasababu watu wanajua hawatachukuliwa mali zao wanatuma pesa Ghana sana.
Watu wametega mingo, Come on Membe ruhusu hii kitu bana watu warudi home kuwekeza.
Hii kitu ina madhara sana kwa nchi kama TZ kwa kuwa wengi wanaotaka kukimbilia huku ni kutoka India, china, Somalia, na Uarabuni .. ni kwa sababu hali ni mbaya kule kwao.
Mfano Wasomali ndiyo wanaofanya kule kwao kusitawalike. wakuja huku itakuwaje?
Note: kuna Kiongozi kasha kula pesa za watu na anashabikia kinoma hili swala na yeye anao uraia wa Nchi mbili... Kuna mwingine Kapewa Uraia na anataka kuja Kuwa Rais wa Nchi hii na wote wako serikalini, Majina na details tunazo tunawakaushia tu.
Mfano Anold Schwarzenegger (USA) alikuwa Gavana wa Jimbo la Carfonia na huku akishikilia uraia wake wa Australia. Lkn kwa sababu USA iko makini waliangalia uwezo wake wakaona anafaa kupewa nafasi hiyo. Multiple citizenship inafaa sana ktk mambo ya biashara na uwekezaji. Hapo tunaweza kunufaika nayo sana.
Ni hofu miongoni mwa watawala tu lakini uraia wa kuzaliwa wa mtu haufi kwani hata huko wanapopewa urai pacha wanaweka bayana uraia asilia.
Wengine hata cha kuwekeza hatuna. Ila hatuoni sababu yoyote ile kwa nini tunyang'anywe uraia wetu endapo tukiamua kuchukua uraia wa kwingine.