Uraia pacha: Maslahi binafsi dhidi ya masilahi ya Taifa

hivi kwanini wanatulazimisha turuhusu uraia pacha? hawa maforeigner waeleze uraia pacha utaleta faida gani kwa Tanzania. kwa akili zao wanafikiri Tanzaniat unatafuta wawekezaji wa level yao? yaani nchi kubwa kama hii itafute wawekezaji wanaotegemea kupata hela toka kwenye kutunza vizee na kuosha vyombo vya wazungu? NJOONI BASI muwekeze migodini, njoni mchimbe visima vya gesi, njoni muwekeze hata kilimo tu kama hata iyo ardhi mtaweza kununua, umeosha masaburi unafikiri watz tunakutegemea utangaze utalii au uje uwekeze? nyie hamna faida kwa watz na wala msitusumbue, hatutaki uraia pacha period!
 
Watanzania wanaopinga uraia pacha hawana hoja zaidi ya wengi wanafuata mkumbo tu na kuwa na roho mbaya, kuna sababu gani umkataze mzaliwa na mtanzania aliye raia wa nchi nyengine asipate uraiya wa nchi yake ya asili. Wengi wenu hamjapata fursa za kusafiri na kuishi nje ya nchi na mkipewa fursa hiyo mtafanya lolote ili muipate fursa hiyo, mkifikiri wote wanaoishi nje wanaishi kama wafalme.Wengi wao wanafanya kazi, wanasoma na wengine wameenda na wameamua kuishi baada ya kupata fursa ya matibabu na kati ya hao kuna wanaotaka wanataka kurudi nyumbani kuwekeze hata hicho kidogo wanachopata na wengine kuja fanya kazi kama raia baada ya kumaliza masomo. Dunia imekua kama mji mmoja siku hizi muwache roho mbaya pale penye ushindani ndipo panapatikana mafanikio siyo mtu anakataa kwa jazba tu bila nguvu za hoja.


1. vipi unaweza kutusaidia ni kitu gani unakikosa wewe Mtanznaia mwenye urai w ahuko na kama ukipata huu wahuku ukawa na mbili Utapata huku Tanzania na kitakuwa cha maana na faida kwako kuliko unachokipata huko ulipo?(Maana naamini kama umefikia kuukana huu umeona huo w ahuko ni wa maaan zaidi.

2. Hizo dharau zenu za kuwafanya wengine wajinga wakati nyinyi mnafanaya shughuli za ajabu na kuishi maisha ya ajabu kuliko tunayoayaishi uku bongo ndipo mnapofeli.
 
Tungekuwa na vijana kama kumi wenye kuchambua mambo kwa dimensional ya Pole Pole tungekuwa si mbali tu bali tofauti na tulipo!
 
Sasa mbona rais aliyechaguliwa na Watanzania haishi kuja kuomba Diaspora warudi kuwekeza nyumbani?

Kwa nini asiusugue tu huko au kuacha kukutana na Wabongo kiwanja?


Mwambieni awakome, asiwafatefate na asijipendekeze kwenu. Sie wenyewe tunamshangaa
 
Si ndio huu ubinafsi unaozungumziwa????!!!?

Sio suala la kipaumbele kwa sasa, acheni watu wajadili mambo ya muhimu kwa manufaa ya wengi, umiliki wa ardhi, madaraka ya rais,separation of power,rasilimali na kama hayo

Sasa hicho nilichokisema si ni moja ya hivyo vipaumbele unavyovisema?

Mimi mara nyingi nilipokuwa nikifika hapo JNIA wale rafiki zangu wa Uhamiaji huwa walikuwa wananishauri sana kuwachukulia pasi watoto wangu kwasababu wanaona wanazo zile za nchi nyingine ihali baba yao anayo na ile pasi ya Tanzania.

Tena kuna mmoja ananiambia utaratibu mzima wa kuzipata pasi hizo na kwamba nisiwaache watoto waje kupotea, je unafahamu alikuwa akimaanisha nini?

Haya mambo yote ya rasilimali kama ardhi, nyumba na biashara vyote mimi ninavyo na si kwamba ni tatizo, ila kwa sabab twakazania hilo jammbo.

Huyu jamaa amekosea kwenye "heading" ya hoja yake.

Tusiendekeze uvivu wa kufikiri hata kwa mambo madogo.
 
Binafsi bado natetea uraia pacha na nimjibu mleta mada kwa hoja ndogo tu: Kuwa kama hofu ni kuwa ukimpa mtu uraia pacha na akaishi hapa nchini atakosa uzalendo, basi ajue hata ukimpa uraia wa kuandikishwa pia hatakuwa mzalendo. Yani sawa na alivyosema mtanzania aliyepewa uraia huko nje hapa tz atapewa hadhi maalumu, basi hata mtu wa nje akipewa uraia wa kuandikishwa hapa bongo huko kwao atapewa hadhi maalumu (kama alivyosema kwa India na Ethiopia) na huyu mtu ukiwa nae jeshini au kwingineko ujue kama ana lake jambo bado atalitekeleza tu, iwe alikana kwao au hakukana.

Cha muhimu tuwe tu makini na wale waliopewa uraia pacha hapa tz lakini originally sio wa hapa...
 
Binafsi bado natetea uraia pacha na nimjibu mleta mada kwa hoja ndogo tu: Kuwa kama hofu ni kuwa ukimpa mtu uraia pacha na akaishi hapa nchini atakosa uzalendo, basi ajue hata ukimpa uraia wa kuandikishwa pia hatakuwa mzalendo. Yani sawa na alivyosema mtanzania aliyepewa uraia huko nje hapa tz atapewa hadhi maalumu, basi hata mtu wa nje akipewa uraia wa kuandikishwa hapa bongo huko kwao atapewa hadhi maalumu (kama alivyosema kwa India na Ethiopia) na huyu mtu ukiwa nae jeshini au kwingineko ujue kama ana lake jambo bado atalitekeleza tu, iwe alikana kwao au hakukana.

Cha muhimu tuwe tu makini na wale waliopewa uraia pacha hapa tz lakini originally sio wa hapa...


Unazijua haki za Raia w aKuandikishwa?
 
Wajinga wa dizaini yako mpo wengi ndio mnaonedelea kumuweka kwa ahadi kuwa tawaleteea Uraia Pacha,

kwa taarifa yako Uraia pacha ni zaidi ya Ushoga.

Unajichanganya.

Mara unasema.kawekwa na tume, mara wajinga wengi.

Unataka kuniambia Tanzania ni nchi ya wajinga?
 
Tungekuwa na vijana kama kumi wenye kuchambua mambo kwa dimensional ya Pole Pole tungekuwa si mbali tu bali tofauti na tulipo!

Ndugu Horseshoe Arch ni kweli unayoyasema.Bandiko la Ndg Kashishi limejaa mambo mengi ya maana ambayo inapaswa kuyajadili kwa kina kwa mustakhabali wa Taifa letu na si kutupa kashfa na kubezana kama ilivyo kawaida yetu kwa sasa.Ieleweke wazi kwamba Ndugu zetu waliopo Diaspora si kwamba ni wasaliti.Wapo waliokwenda huko kwa ajili ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masomo,na kukawafanya watokomee huko kutokana na fursa za kiuchumi walizozipata.Lakini walio wengi bado wana Utashi mkubwa na mambo ya nyumbani (Tanzania).Hapa namnukuu Waziri wa sheria wa Nchi ya Denmark alipokuwa anatoa Hotuba baada ya Bunge la Nchi hiyo kupitisha sheria ya Uraia pacha, Mwanzoni mwa summer ya 2014."Katika Dunia ya leo watu wengi wanachagua kuishi katika Mataifa ya Nje kwa sababu mbalimbali, lakini bado kuishi huko Nje hakuwaondolei Uzalendo na Mapenzi katika Nchi zao Asilia!" Mwisho wa kunukuu.

Kutokana na Takwimu zilizopo, Leo hii kuna Waafrika karibu 190milioni wanaoishi Nje ya Bara la Afrika.Kuwepo kwao Nje kwa sababu mbalimbali hakupaswi kupuuzwa.Kwani kwa kipindi cha Mwaka 2012 Remittance kutoka kwa watu hao imekuwa kubwa kuliko misaada ya Nchi na Mashirika ya Kimataifa kwa Africa.Remittance ilikuwa Dola la kimarekani 60 Billion. Na kwa Waafrika wanaoishi kusini kwa Jangwa la sahara Remittances ilikuwa 2010 - US$ 22m, 2011 - US$ 29m, 2012 - US$ 31m na 2013 - US$ 33m. Kumbuka katika Nchi hizo za kusini mwa Sahara Tanzania nasi tupo.Kwa kuanisha hivyo si kupuuza suala zima la Diaspora kwa kiwango fulani watu hawa wanachangia uchumi wa Nchi.

Hapo awali Ndugu Kashishi kazungumzia Nchi Ya India kukataa suala zima la Uraia Pacha.Ni kweli Nchi hiyo hawalitaki suala hili haswa kwa sababu za kiusalama na Utamaduni wao.Lakini pia kumekuwa na Shinikizo kubwa kwa miaka ya karibu kujaribu kubadili sheria hiyo.India Citizenship Act ya mwaka 1924 imefanyiwa ammendment mara 5 kujaribu kutoa mwanya kwa kilio cha Wahindi kuhusu Uraia pacha lakini bado hawajafanikiwa,ammendments za miaka ya karibuni ni za 1992,2003 na 2005.India inawatambua Raia kwa makundi mawili tu 1);Citizen by right of blood ( Jus Sanguinis) na 2); Citizen by right of Birth or Territory (Jus Soli). Bado makundi ya watu wa Haki za binadamu na wanasiasa wanaamini kuwa ipo siku India kama ilivyokuwa kwa Sweden na Denmark itakuwa na Uraia pacha.India na China ndio Nchi zinazoongoza kwa Remittances kutokana na Wananchi wake kuwa Dispora.

Tujibishane hapa kwa Hoja lakini tugundue kuwa wimbi hili zito la Uraia pacha linakuja kwetu kwa nguvu kubwa tu,Halikwepeki, tuangalie mianya yote tuizibe ili tuweze kuunda sheria itakayokuwa na manufaa kwa Taifa kuhusu suala hili la Uraia pacha.Kwa mawazo yangu,ikiwa sheria hii itapita,wote wenye Uraia pacha wasipewe nafasi ya kufanya kazi ktk vyombo vya usalama au kuwa na uwezo wa kugombea nafasi ya Uongozi wa Umma.Waziri Mkuu wa Zamani wa Sweden Mh.Olof Palme aliwahi kuikataa Hoja hii ya Uraia pacha,na ni kitu ambacho Wasweden wengi wazee hawakubaliani nacho,Lakini Bunge la Nchi hiyo ilipitisha sheria ya Uraia Pacha na imeanza kutumika toka 2002.
 
Tulisha ongea hili miaka mingi iliyopita mwandikaji amekwepa ukweli

1. Kwanini tunajifananisha na India ambayo haifanani na sisi hata kitu kimoja badala ya kujilinganisha na ndugu zetu wa Kenya na Uganda. Kama ni mifano ya nchi basi Kenya ni mfano mzuri kuanzia kwenye utamaduni mpaka uchumi.
2. Mwandishi anaongelea diaspora wa sasa watafadika je kunaanaejua miaka kumi ijayo nani atakuwa diaspora badala ya kuongelea watu binafsi tungeweka nchi mbele. Je uraia wa nchi mbili una faida kwa Tanzania sio kuhusu ubinafsi.
3. Uzalendo haununuliwi! unaweza kuwa mzalendo au kutokua mzalendo huwezi kusema mtu ni mzalendo leo kwasababu tu ya passport na kesho si mzalendo kwasababu kachukua uraia wa nchi nyingine. Uzalendo uko kwenye moyo wa mtu sio swala la kisiasa au la kujionyesha kwa passport. Huwezi kulazimisha watu wawe wazalendo hivyo kama mtu si mzalendo leo haita badilisha lolote kama ana passport moja au mbili. Mfano Kuna Mtanzania professor ana passport ya USA miaka michache iliyopita alileta madiwani kutoka kanda ya ziwa bure kujifunza kazi za miji kwenye University pale Mississippi, wameleta Engineers zaidi ya ishirini kwa miaka kumi iliyopita kutoka chuo kikuu kusoma bure pale Florida A & M sasa ni VP wa university huko North Carolina. Je huyu si mzalendo kwasababu ya kuchua passport ya USA. Wale walarusha wafanyakazi wa serikali wengine ni wabunge je ni wa zalendo kwasababu tu ya passport zao za Tanzania? jiulize haya badala ya kutafuta mifano ya India ambayo huelewi vizuri hiyo nchi.
4. Faida binafsi kwa watanzania wa diaspora zinasaidia vipi Tanzania? Mimi mfano hapa namsomesha mtoto wa kaka Tanzania hii ni faida binafsi na faida ya nchi, natuma pesa kwa mama ni faida binafsi na ni faida kwa Tanzania, najaribu kujenga ni faida binafsi na faida kwa Tanzania (viwanda vya cement, vigaya, mbao, mafundi, rangi, engineers, mafuta) , natoa michango ya kijamii misiba, harusi, ujenzi wa makanisa, matengenezo ya shule yetu ya sekondari hii ni faida binafsi na faida ya Tanzania. Nimepeleka kundi la marafiki kupanda Kilimanjaro hii ni faida binafsi na faida ya Tanzania. Kuitwa Mtanzania USA ni faida ya nchi tunaitangaza nchi yetu tunasaidi jamii kimawazo.
5. Vilevile ni lazima ujue watu unao waongelea badala ya kutoa mifano bubu mfano tofauti na wahindi Watanzania wa diapora hawajahama kimoja wengi wao wanaenda likizo kusalimia labda kama wanamatatizo ya makaratasi hawawezi kusafiri. Matatizo haya ya makaratasi na vibali mengi yanatokana na hili swala la uraia. Wahindi wa Tanzania mfano waliletwa na waingereza 1950's kujenga railways Watanzania wa diapora wengi wameenda miaka ya 1990's kwa elimu na kutafuta maisha!. Hivyo issue hazifanani kabisa
6. Watanzania wa diapora wanatuma pesa nyingi kuliko wanayochukua Tanzania.
7. Watanzania wa diaspora wamejisomesha wenyewe na kufanya kazi ngumu kwa miaka mingi kujimudu
8. Watanzania wa diaspora si wafisadi na hawajakimbia Tanzania kwasababu zozote za kihalifu
9. Watanzania wengi wa diaspora ni watanzania sasa hivyo kama ni wabaya au si wazalendo basi hata sasa hivi si wazalendo kama nilivyosema. Watanzania wa dispora wanaishi nje sasa hivi na hakuna kitu ambacho sasa wanashidwa kufanya kama wangekuwa na nia mbaya
10. Hivi kama una ndugu yuko kwenye nchi nyingine akajisomesha kwa miaka kumi na kuwa engineer halafu kamaliza shule kampuni ya Boeing wakataka kumpa kazi ya kutengeneza ndege za kivita lakini sharti au raia. Mtu huyu asikopata kazi anarudi Tanzania kwasababu ya vibali. Kazi ni ya $90,000 na huyu kijana anategemewa na familia nyumbani. Anaweza kubahatisha kazi nyumbani lakini vilevile anaweza asipate kazi na uzoefu. Je wewe utamwambia achukue au aache kazi kwasababu ya uzalendo? Je unapenda huyu jamaa akae USA bila kazi au afanye kazi za chini ya kiwango? sasa kunafaida gani ya kuwa nchi za wenzetu kama huwezi kusaidia nyumbani? mnataka Watanzania wawe second class kwasababu ya uzalendo feki?

Vilevile kuchukua passport nyingine kunakupunguzia nini Mtanzania wa kawaida, mimi na makaburi ya babu zangu yanakuuma nini, mimi kuja kwa wazazi wangu kuna kuuma nini, mimi kuwa na urithi wa mababu ambao wameishi kabla ya nchi kuitwa Tanzania inakuuma nini. Uzawa, Utanzania si kibali au wanasiasa wa dodoma kuamua hivyo mwandishi hajua anachokiongea ameweka kuangalia watu zaidi ya nchi
 
diaspora wawekeze nchini? yaani mkafue nepi za vizee na kutawaza vizee mpate hela ya kuwekeza nchini? labda uwekezaji wenu iwe ni kufungua vibanda vya barbershops, ila uwekezaji wa tz utakaotusaidia ni uwekezaji mkubwa wenye mitaji mikubwa sio huo wa wauza bangi na unga ulaya. kama ni kwa hela yenu hiyo mbona wabongo wengi wanayo, waliobaki tz watawekeza wenyewe ninyi wekezeni hukohuko ulaya. mtu unakuja na ka milioni hamsini kako au mia unajifanya wewe ni diaspora mwekezaji na "you know w'r i'm saying" nyingiiiii utafikiri kichwani kuna kitu kumbe mzibua mitaro tu. uwezo ninyi wa kuwekeza tz hamna, uwezo wenu umeishia kwenye kutuma pesa kwa ndugu zenu walioko hapa tu na kuwajengea vibanda vya kuishi, ila kuwekeza tz hamna uwezo huo. na wala ninyi sio tegemeo la taifa kwa uwekezaji; mtawekeza kwenye gas ninyi? mtawekeza kwenye madini ninyi? mkashindane na masukuma ya kahama na geita huko hayajasoma na hayajui ulaya ni nini lakini yana vitalu kibao na wala hela yake wewe mfua nepi humfikiii, si bora tuwasapoti hawahawa walioko hapa? au mnalialia uraia pacha baada ya kuona mtakosa kufaidi gas ya mtwara? ndo mshaikosa ivo.

Utakuwa na matatozo yako binafisi na wapigabox nje. Tafakari kunawatu hawakupata nafasi kupata elimu ya juu hapa tanzania na wakaamua kwenda nje kujisomesha wakwati hilo lilikuwa jukumu la Tanzania kuwasomesha. Ho watu wameenda nchi kama Poland ambapo sio pazuri sana lakini kwasababu iliwabidi wakae miaka mingi kujisomesha wameoa na kuwa na familia poland. urahia ni haki ya mtu kwenda nchini kwake bila kupingwa kwa kunyimwa visa. sasa ukimwambia huyu mtu asiwe na uraiya wa nchi mbili unamaana inabidi achague haki ya kunyimwa kwenda poland kuwaona watoto wake au haki ya kuja tanzania kuangalia wazazi wake kwasababu usipokuwa rahia unaweza kunyimwa visa wakati wowote. Watanzania tujifunze kuwa na empathy. pia aliyosema polepole sio mabaya ila hayafikii kuwanyima watu uraia. tungewapa uraiya ila tukawazuia kuwa viongozi serekalini au kujiunga na jeshi. Ila ukumbukwe raia yeyote wa tanzania ambae hajawai kwenda nje anaweza kuihujumu nchi na kukimbilia nchi nyingine na akapewa urai maana pesa ndio huongea. na kunawanaoiba na kubaki bongo bila kufanywa lolote
 
hivi kwanini wanatulazimisha turuhusu uraia pacha? hawa maforeigner waeleze uraia pacha utaleta faida gani kwa Tanzania. kwa akili zao wanafikiri Tanzaniat unatafuta wawekezaji wa level yao? yaani nchi kubwa kama hii itafute wawekezaji wanaotegemea kupata hela toka kwenye kutunza vizee na kuosha vyombo vya wazungu? NJOONI BASI muwekeze migodini, njoni mchimbe visima vya gesi, njoni muwekeze hata kilimo tu kama hata iyo ardhi mtaweza kununua, umeosha masaburi unafikiri watz tunakutegemea utangaze utalii au uje uwekeze? nyie hamna faida kwa watz na wala msitusumbue, hatutaki uraia pacha period!
Hute nawashangaa sana Watanzania wanaopiga madongo wenzao kwa kujitegemea! kama kazi ni ya halali hata kama kuoasha nepi ni poa tu ni kazi. Mimi nilivyokuja kama mwanafunzi mwisho wa 1997 nilikuwa na miaka 20 tu na niliafanya kazi ngumu iliwa ni pamoja na kufanya kwenye viwanda kwa matofali, vifaa vya hospitali na kufanya kazi za utengenezaji wa Computer. Nimejitahidi imenichukua miaka 9 kumaliza degree ya kwanza ambayo ni ndefu kidogo ya USA nilipata na green card. Nkajiendeleza nikapata kazi kabla ya kumaliza shule ya Excel kwenye kiwanda cha simu hivyo nilijiendeleza. Kwa miaka yangu ya mwanzo nilikuwa nalipwa $7 kwa saa. Lakini sijuti maana Tanzania nisingweza kusoma masomo niliyokuwa nataka wakati huu vyuo vya shida. Miaka imeenda mingi tumefanya kazi ngumu lakini sasa tunaona matunda. Watanzania wengi sana wanafanya vizuri na wana kazi nzuri lakini imechukua muda na jitihada za hali ya juu. Mimi nilikuwa naingiza $14,500 kwa mwaka, nikaja $35,000, nilivyo maliza shule ya degree $50,000 , nikaja $55,000 sasa naingiza zaidi ya $80,000 kwa mwaka. Sasa tusemeni tu kwamba tumefua chupi za wazee sisi hatutawasema mungu ndiyo anajua unafanya nini kwa sababu gani. Usiko kuwa mwangalifu unaweza ukawa unajisema mwenyewe bila kujua. Sijaiba, sijaomba pesa y mtu, sijatoa rushwa yeyote n nilikuwa sina kitu lakini sasa mambo mazuri zaidi mungu kasaidia. Lakini watu wengi wameanzia chini. Hawa wazee unaowaona sasa hivi kwenye bunge wengi wametokea vijijini walienda shule bila hata viatu, walichaguliwa kibahati tu kwenye kwenye shule za serilaki, walipewa marejesho kurudi likizo nyumbani, walipewa pesa za kusoma na kazi kwenye serikali. Hivyo hata hao wazee na wengine mafisadi walianzia chini sana. Kitu ambacho watu wengi hamjui ni kwamba sisi wengi wa diaspora bado ni vijana sasa kama tumetoka kwetu bila kitu sasa tuko hapa je unafikiri tunaenda wapi? ndiyo maana wanasiasa wana punic si bure! sis tuta take over anyway tuwe na passport au tusiwe nazo muda umepita kuzuia hawa vijana waliopikwa miaka chini ya miaka 40 lakini uzoefu wa miaka 55!. Hata mkitunyima wana diaspora kuwaona ndugu zetu, kutembelea makaburi ya mababu zetu na kutupiga madongo tutaenda mbele na hakuna mtu ataweza kutuzuia sasa its too late
 
hivi kwanini wanatulazimisha turuhusu uraia pacha? hawa maforeigner waeleze uraia pacha utaleta faida gani kwa Tanzania. kwa akili zao wanafikiri Tanzaniat unatafuta wawekezaji wa level yao? yaani nchi kubwa kama hii itafute wawekezaji wanaotegemea kupata hela toka kwenye kutunza vizee na kuosha vyombo vya wazungu? NJOONI BASI muwekeze migodini, njoni mchimbe visima vya gesi, njoni muwekeze hata kilimo tu kama hata iyo ardhi mtaweza kununua, umeosha masaburi unafikiri watz tunakutegemea utangaze utalii au uje uwekeze? nyie hamna faida kwa watz na wala msitusumbue, hatutaki uraia pacha period!

Duuuu jamaa umetapika pumba sio mchezo kweli safari bado ni ndefu mpaka watu kama wewe kuelewa.
 
inasikitisha sana kuona kuna watz wengi waliisaliti nchi yao mbele ya mzungu. lengo lao walijua tz hakutakuja kuwa na fursa, nakuambieni hata mkipata hela nyingi huko nje, ile kutokuwa watz ni hasara kubwa sana na hii inadhihirishwa na jinsi mnavyolialia hapa. ninapenda niwape moyo, ninaamini kwamba kuna siku Tanzania itakuja kukubaliana na uraia pacha, LAKINI HIYO SIO LEO WALA KESHO, inaweza kuchukua muda sana na si chini ya miaka 30 ijayo. hivyo kama mnapambana kupata uraia pacha, pambaneni tu ila itakuwa kwaajili ya watoto wenu baadaye sana ninyi mkishazeeka.

fursa hizi tunazozipata bongo ninyi hamna haki nazo. ile mimi ninapoamka asubuhi naenda tanga kununua shamba ekari nyingi za machungwa, au ninaponunua shamba kuubwa la kulima mananasi na mihogo yangu bagamoyo au kisarawe, ninyi haki hiyo mmeiuza.

kitu cha ajabu ninachowashangaa ninyi maforeigner ni kwamba, wengi wenu bado mna kasumba kujiona mna uelewa na akili nyingi kuliko wabongo waliobaki tz. ni ile kasumba ya wazungu kujiona wako bora. unaenda ulaya unajifanya una hela kama wenzio wa huko na kuwadharau waliobaki, "you know marekani ninaishi vizuri, nina appartment nzuri, nina gari zuri...etc" mwenzio aliyebaki bongo anakwambia "nimejibana nimejenga nyumba arusha, nyingine nimeanza kimara, nina viwanja kadhaa kibaha na mbeya na mashamba ekari 50 kwaajili ya mananasi. we unabaki mdomo wazi. utahangaika sana lakini umeacha fursa kubwa sana tz ambazo hamtakuwa na haki nazo. huwa nawashangaa mnavyojidai utafikiri mna kitu, kaeni tu hukohuko mkisubiria huruma zetu, siku tukiamka vizuri tunaweza kuwafikiria, ila kama mnaendelea kutukana nakuhakikishia mnazidi kuharibu.jf unaweza kuidharau lakini bunge zima liko humu hadi rais wenu anapitia humu na mkiwa mnaleta dharau na matusi wakati mnategemea huruma zetu mtakesha sana.
 
Duuuu jamaa umetapika pumba sio mchezo kweli safari bado ni ndefu mpaka watu kama wewe kuelewa.
hata mimi kipindi bado limbukeni wa diaspora nilikuwa na fikra kama zako, lakini nilivyorudi bongo nikamkuta msukuma mmoja kahama hajafika hata uganda tu hajawahi toka nje lakini ana vitalu vya kuchimba dhabahu geita na musoma huko anaingiza billions, niliishiwa pumzi nikaona kumbe ulimbukeni si hela bal ushamba....nikaacha ucivilization wangu pembeni nikajifanya mjinga na mshamba matokeo yake sasa nimejua nini maana ya kuwa na uelewa mkubwa na mdogo kimaisha ni nini. ukiwa diaspora kuna kasumba kwamba unatamani sana maisha yale ya wazungu, maendeleo yao yale yawe Tanzania, na unakuwa na hasira sana kwamba kwanini viongozi wa tz hawafanyi kazi hata tukaendelea kama ulaya? matokeo yake unafika kipindi kila aliyeko tz unamuona mjinga hana uelewa mzuri kama wewe hajaona dunia kama wewe na mshamba tu....umesahau kusoma vitabu vitu gani viliifanya ulaya ikawa hivyo na lini ilibadika kuwa hivyo. ninaye jamaa yangu mmoja yeye amejibana sana akanunua condominium nchi fulani, na ana gari yake nzuri ya kuendesha, alikuwa anajiona yuko juu, siku tukamtembelea ndugu yangu mwingine hapa bongo akashangaa sio tu kuwa ana gari bali ana malori kama 20 ya mizigo, ana hotel na lodge na ana biashara kubwa sana, achilia nyumba za kuishi arusha na dsm. hivyo ninyi endeleeni kujifanya mnajua sana kuliko wabongo, na bakini na ukweli palepale kuwa ninyi ni maforeigner mliouza haki zenu na mnapambana kuzipata tena bila mafanikio.
 
Ndugu Mwawado sina roho ya kwanini kiatika hili ila kuna changamoto nyingi sana kwenye suala zima la uraia pacha mojawapo ikiwa ni ya kiusalama! Sina hakika kama tumejiandaa vya kutosha kukabiliana na changamoto hizo kwa sasa! What if mwanya huu utatumika vibaya na wenye malengo yao kwa kupandikiza watu ambao watakuwa vibaraka?

Sheria italindaje maslahi ya taifa dhidi ya maslahi binafsi mfano pale itakapotokea mfanyakazi wa idara fulani ya serikali atakapopata sabbatical leave kwenda kuongeza ujuzi na kisha kuamua kutokomea kwa kisingizio cha uraia pacha! Huoni wasioitakia mema nchi wanaweza kumtumia mwana diaspora huyo kwa manufaa yao?

Ni haya na mengine mengi yananifanya niwaze kwamba sheria zetu na mifumo yetu ya kuzisimamia kuna namna haijakomaa kuweza kustahimili changamoto zitakazojitokeza kwenye suala zima la uraia Pacha. Kama nidhanivyo ndivyo basi ijulikane wazi kwamba ili uweze kuwa na nguvu za kiutawala ni lazima utawale watu ndani ya mipaka yako kisheria,sasa inapotokea mtu huyo huyo yuko ndani ya territory mbili sina hakika kama una nguvu kumbana pale inapotokea kaenda kinyume na taratibu alizotakiwa kuzitii. Tunarudi kwenye concept ya popo! Ni kukubali kuachia mbawa zake ili arudi kwenye kundi la wanyama ama abadilishwe features za mammal awe ndege!
 
Wordy wackness full of medieval mincing.

Hivi hawa watu wanajua kwamba Tanzania penda isipende itabidi kukubali uraia pacha kama ilivyokubali vyama vingi? That they can't fight against the tide of time?

Aand that, the earlier they do this, the better for the country?

Nchi zinazoruhusu uraia wa nchi mbili au zaidi zikikupa uraia wake maana yake ni kuwa unaweza kuwa na uraia wa nchi husika na uraia wa Tanzania,kinyume chake ni kuwa Tanzania hairuhusu utaratibu huo!.kama umepeta uraia mfano wa America,na unaamua kuishi marekani basi huna sababu ya kuukana uraia wako wa Tanzania na huna haja ya kurudisha passport ya Tanzania!,Badala yake mtu akipata tu uraia wa nchi nyingine basi mwenyewe anaamua tena kwa nyodo kuponda passporti ya Tz na kuirudisha bila hata kutaka maelezo ya kisheria.Kama ukiwa na passport za nchi mbili na unataka kurudi nyumbani unaweza kurudi na passport ya Tanzania na kufanya shughuli zako zote kama mtanzania.Kwa hiyo hakuna haja ya kuwaiga Kenya wala uganda etc. huwezi kutumikia nchi mbili kwa wakati mmoja na ukizingatia maisha yasiyozidi miaka !00.
 
Back
Top Bottom