Uraia pacha: Maslahi binafsi dhidi ya masilahi ya Taifa

Kashishi

JF-Expert Member
Apr 11, 2010
1,131
611
Uraia pacha, masilahi binafsi dhidi ya masilahi ya Taifa

polepole.jpg

Humphrey Polepole

KWA UFUPI

Ikumbukwe katika suala la uraia, nchi (State), inatafsiriwa kama Mamlaka Kuu (Sovereign Authority), yenye mamlaka kamili ya kutawala watu katika eneo lake linalotambulika.

Wanaoendelea kudai uraia pacha, ama hawajasoma Rasimu au wana lao jambo.
Salamu zangu kwenu wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, naendelea kuwapa moyo kwamba kazi mnayoifanya ni yetu na ninyi miongoni mwetu mmeonekana wenye sifa na vigezo vya kuitenda kazi hiyo ipasavyo.

Simamieni masilahi ya umma na masilahi ya nchi yetu kwanza. Kwa hakika, masilahi ya wananchi na nchi yakiwekwa vizuri, maslahi yetu binafsi na ya makundi yetu, yatapatikana kwa kuzingatia usawa, sifa, vigezo, uzalendo na uamuzi tukiwa sisi wananchi.

Leo nitazungumzia hoja inayovuma mjini juu ya uraia pacha. Nilitembelea mji wa Dodoma nikagundua hata Kamati za Bunge Maalumu zina kazi katika hili. Nianze kukiri kwamba katika hoja hii nina masilahi. Nina ndugu, jamaa na marafiki ambao wameondoka hapa nchini miaka nenda rudi na baadhi yao wameamua kuchukua uraia wa huko waliko ughaibuni.

Zaidi ya wale ndugu, jamaa na marafiki ambao wamehamia ughaibuni, nimepata bahati ya kuwa na ndugu wa damu, ambao ni raia wa nchi nyingine na baadhi yao wako hapa nchi jirani katika Afrika Mashariki.

Nianze na mtazamo wa kawaida kabisa, ndugu hawa, jamaa na marafiki zangu na hasa nizungumzie wale walioacha kuwa raia wa Tanzania kwa kile kigezo cha kuchukua uraia wa nchi nyingine hakujawaondolea ukweli kwamba wao bado ni Watanzania kwa asili na nasaba. Uhusiano, mawasiliano na uhalisia wa udugu, ujamaa na urafiki wetu haujabadilika hata kidogo. Nimeshuhudia hata pale ambapo kuna shida au furaha hapa nyumbani, ama wameshiriki moja kwa moja au kwa michango yao ya hali na mali.

Ni ukweli ulio dhahiri kabisa kwamba, hawakufanya uamuzi wa kulazimishwa bali kwa namna moja au nyingine mazingira yaliwafanya wajitafakari kubaki na uraia wa Tanzania na kukubali kubaki na changamoto fulani wakiwa ughaibuni au wachukue uraia wa huko waliko, ili kuweka wepesi wa hali lakini pia kupanua wigo wa fursa wanazoweza kupata huko waliko kama raia.

Tafsiri ya uraia kwa ufupi

Kitabu cha taarifa na chenye kumbukumbu (Insaiklopidia) cha Chuo Kikuu cha Stanford, kinatafsiri uraia (citizenship) kama uanachama katika jamii ya kisiasa na unaonufaika na haki, pamoja kuwa na wajibu katika uanachama huo. Dhana ya uraia inajumuisha mambo matatu.

Moja, kwamba uraia ni hadhi ya kisheria inayotafsirika kwa haki za kiraia, kisiasa na kijamii. Hapa, raia ni mtu anayekwenda kwa mujibu wa sheria na ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria.

Mbili, ni raia kama mawakala wa kisiasa wanaoshiriki kikamilifu katika taasisi za kijamii na kisiasa.

Tatu, ni raia kama wanachama wa jamii ya kisiasa inayoakisi aina fulani ya utambulisho. Utambulisho katika dhana ya uraia ni jambo muhimu sana. Utambulisho huakisi uhusiano alionao mtu au raia moja kwa moja ama kiasili au kinasaba na jamii fulani ya kisiasa.

Ikumbukwe katika suala la uraia, nchi (State), inatafsiriwa kama Mamlaka Kuu (Sovereign Authority), yenye mamlaka kamili ya kutawala watu katika eneo lake linalotambulika. Kama ilivyo mipaka ya kisheria ya nchi inayoonyesha ukomo wa eneo lake, ndivyo dhana ya uraia (citizenship) inavyoonyesha na kutambulisha watu walio chini ya Mamlaka ya nchi fulani.

Leo hii nchi siyo tu ni nguvu za dola na taasisi zake mbalimbali, bali pia ni jumuia ya wananchi kama wanachama. Uraia kwa maana hiyo, ndiyo uanachama katika nchi. Kama ilivyo katika vilabu vya mpira wa miguu, mfano Yanga au Simba, mtu unaweza kuwa mwanachama wa Yanga au Simba, lakini siyo vilabu vyote viwili kwa pamoja.

Ubaya wa uraia pacha

Uraia pacha unaondoa ile dhana ya uaminifu usiogawika (indivisible loyalty) kwa nchi na Mamlaka Kuu ya nchi. Kama ambavyo mtu hawezi kutumikia wakuu wawili kwa wakati mmoja, vivyo hivyo mtu hawezi kutumikia (kwa maana ya uaminifu na utii) nchi zaidi ya moja. Uraia pacha unadhoofisha usalama wa taifa. Nieleze kwa mifano tu, miezi kadhaa iliyopita kulitokea uvumi kwamba ofisa wetu wa Jeshi la Wananchi, tena mwenye dhamana ya kutunza au kushughulika na taarifa nyeti za kimawasiliano ametoweka.

Sote tu mashahidi kihoro tulichokipata kipindi kile na zaidi uvumi ulipozidi kuwa huenda amekimbilia nchi fulani ya jirani. Tukiwa na uraia pacha, hofu hii itaongezeka maradufu, hasa pale wenye uraia pacha watakapopewa dhamana ya madaraka makubwa na nyeti.

Kuna mifano ya jamaa zetu, ambao tuliwafahamu kama Watanzania, tukawasomesha kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania, wakahitimu na tukawapa dhamana na madaraka makubwa na nyeti. Leo hii angalau wale ambao mimi nawajua hawako nasi tena. Wamekwenda kwenye ile nchi ambayo ni kama ilizaliwa upya na inasemekana inapiga hatua kubwa kimaendeleo.

Kama uraia pacha ukiwapo, itakuwa vigumu kusema hii ni siri na ni kwa masilahi ya taifa tena huenda dhidi ya mataifa jirani kwa sababu hao wenzetu ambao pia watakuwa raia wa nchi jirani tutakuwa nao tukitengeneza mambo hayo.

Tuchukue mfano mwingine, sasa tuna sera ya kuhudumu katika jeshi kisheria kwa vijana wetu kama sehemu ya kujenga ushupavu na kuimarisha uzalendo wao, tukiwa na uraia pacha tujiandae kuwa na Warundi, Wakongo, Wamarekani, Wakenya na Wasomali JKT tukiwafundisha uaminifu, utii na namna ya kuipenda Tanzania kwa moyo wote hata na ikibidi mpaka tone la mwisho la damu yao.

Zaidi ya yote, uraia pacha unavunja msingi wa haki ya usawa kwa sababu katika taifa moja, raia wanawekwa katika mafungu, wale wenye uraia wa zaidi ya nchi moja, ambao wanakuwa na haki zote nchini na haki zaidi kwingineko dhidi ya wale wenye uraia mmoja, ambao wana haki zote za hapa nchini pekee, lakini wote wako sawa nchini.

Suluhisho ndani ya Rasimu ya Katiba Toleo la Pili

Rasimu inapendekeza bila kupepesa macho kwamba uraia wa Jamhuri ya Muungano ni mmoja na utapatikana kwa njia mbili kuzaliwa na kuandikishwa.

Ibara ya 59 ya Rasimu ya Katiba na kama inavyofafanuliwa na Randama, inawatambua na kuwapa hadhi maalumu watu wenye asili au nasaba ya Tanzania na ambao wameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata uraia wa nchi nyingine wanapokuja Tanzania kwa masharti yatakayoainishwa na sheria za nchi.
Lengo la Ibara hii ni kuwapa hadhi maalumu watu walioacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano, tofauti na raia wa nchi nyingine ambao hawana asili au nasaba ya Tanzania.

Sababu ya mapendekezo haya ni kuwawezesha watu waliokuwa raia wa Tanzania waliopoteza uraia kwa namna yoyote ile kuwa na hadhi maalumu wanapokuwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hadhi hiyo itawaondolea usumbufu wanaporejea Tanzania na kuwapa fursa mbalimbali za kushiriki katika maendeleo ya nchi, jamii na familia zao zilizobaki Tanzania.

Mapendekezo haya yalizingatia kuwa nchi itakapotambua uraia wa nchi mbili, haitakuwa na msingi wa kikatiba na kisheria wa kuwazuia raia wa nchi nyingine kubaki na uraia wao wanapokuwa raia wa kuandikishwa wa Tanzania kwa kuzingatia kuwa Jamhuri ya Muungano inapakana na nchi nane na italeta changamoto ya usalama na ulinzi.

Uzoefu wa nchi nyingine

Uzoefu wa nchi ya India na Ethiopia ambazo hazina na zimesita kutoa uraia wa nchi mbili kwa sababu za kiulinzi na usalama, lakini zimetoa hadhi maalumu kwa watu wenye asili na nasaba ya nchi hizo, ambao wameacha kuwa raia wa nchi hizo.

Katika Katiba ya India, watu hao wanaitwa ‘Persons of Indian Origin' na wana hadhi maalumu. Kwa mujibu wa sheria za India, mtu mwenye asili au nasaba ya India hadi kizazi cha nne, atapata hadhi ya ‘Person of Indian Origin (PIO)', isipokuwa kwa raia wa nchi za Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, China, Iran, Nepal, Pakistan na Sri-Lanka.

Watu wenye hadhi ya PIO wanaweza kupata fursa zifuatazo: Kupata kadi ya kitambulisho cha PIO. Hahitaji viza ya kuingia na kutoka India. Anaweza kukaa miezi sita nchini India mfululizo bila kulazimika kujiandikisha uhamiaji. Wana haki sawa ya kupata huduma za kiuchumi, kifedha na elimu kama ilivyo kwa raia wengine.

Wana haki ya kununua, kumiliki, kuhamisha, kuuza mali isiyohamishika isipokuwa kwa mashamba makubwa ya kilimo. Watoto wao wana haki ya kudahiliwa katika vyuo vya elimu ya juu nchini India. Wana haki ya kupata makazi katika utaratibu unaosimamiwa na Serikali au wakala wake.

Hata hivyo, watu wenye hadhi ya PIO hawana haki zifuatazo: Hawaruhusiwi kupiga kura na hawaruhusiwi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa wala kushika madaraka ya utawala.

Wito wangu kwa wajumbe wa BMK na wananchi wenzangu

Tuisome Rasimu ya Katiba Mpya Toleo la Pili kwa jicho chanya, tuyaelewe maudhui yake, tuone ni namna gani yanalenga kuimarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tulifuatilie Bunge Maalumu kwa ukaribu na tuendelee kujadiliana kwa uwazi kwa maana ya kujenga. Nchi yetu bado ni changa sana kuanza kuugawa uaminifu (loyalty) na utii (allegiance) wetu kwake
.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Nachefuka nikishakiaona hiko kijamaa (pichani) akilinachojifanya kinajua kumbe ni zero kinaleta vurugu tu.
 
Safi Sana kuna watu wanamasilai chanya na nchi yetu kutetea hili lakin wanaaindwa kua recognized kwa ushabiki wa wapuuzi wachache na maslai yao binafsi

Echo werema jaji kwa kulisimamia hili bila woga
 
Kimsingi hatuwazuii kuja kusalimia nduguzao,hatujawahi kuwazuia na hatutawazuia kwa kuwa hata sasa wanakuja, Mtimti yeye mpaka sasa ana passport mbili na ana mpango wa kuongezea nyingine kama anavyokiri,idara ya uhamiaji iwe na utaratibu wa kuwasiliana na idara za nchi nyingine ili hawa watu wakamatwe,tanzania hatuna asili ya uhuni kwa kutoa passport ovyoovyo kama alivyopewa huyu jamaa Mtimti na akawa anatamba kwenye mitandao, wapewe vikaratasi tu kama alivyosema polepole vya kuonyesha kuwa wao ni second class tanzanians
 
Last edited by a moderator:
Nachefuka nikishakiaona hiko kijamaa (pichani) akilinachojifanya kinajua kumbe ni zero kinaleta vurugu tu.

Huyo dogo ni hazina ya taifa kama ilivyo gesi na dhahabu, tatizo hazina aliyonayo bwana polepole hamuwezi kuifanyia kama mnavyozifanyia hazina nyingine za ma prof wa mlimani wanaotumika na magamba
 
Swala la Uraia wa nchi mbili halipingiki ni Km watu walivyokuwa wanakataa vyama vingi. Nchi nyingi zilizoendelea zinaruhusu raia wake kuwa na uraia pacha. Hili watanzania lazima tulikubali.
 
Nachefuka nikishakiaona hiko kijamaa (pichani) akilinachojifanya kinajua kumbe ni zero kinaleta vurugu tu.

uko kama mimi jamaa kajinga sana hakajui kitu halafu kanajifanya kanajua mambo mengi kumbe ulimbukeni tu.
 
Swala la Uraia wa nchi mbili halipingiki ni Km watu walivyokuwa wanakataa vyama vingi. Nchi nyingi zilizoendelea zinaruhusu raia wake kuwa na uraia pacha. Hili watanzania lazima tulikubali.

Umepewa mifano hai ya mataifa makubwa kama india yameukataa kwa sababu nzuri tu,nawashauri hao diaspora wakishaolewa na vibibi na vibabu vya kizungu na kubadili uraia,wao si watanzania, hata wale wanaofanya kazi ya kuviosha na kuvivisha nepi vikongwe visivyojiweza katika vituo maalum, either ubaki mtz au sepa
 
uko kama mimi jamaa kajinga sana hakajui kitu halafu kanajifanya kanajua mambo mengi kumbe ulimbukeni tu.

Jadili mada critically,unamchukia mtu au una uwezo wa kupinga hoja zake? Jamaa anajua sana na katika ukoo wenu itabidi mzaane sana ndio mpate mtu mwenye talent kama ya bw polepole
 
Swala la Uraia wa nchi mbili halipingiki ni Km watu walivyokuwa wanakataa vyama vingi. Nchi nyingi zilizoendelea zinaruhusu raia wake kuwa na uraia pacha. Hili watanzania lazima tulikubali.
Ila uelewe pia hizo nchi zilizoendelea mazingira yao ni tofauti sana na nchi kama zetu, wao walishajenga misingi imara sana ya kimaisha na kimaendeleo ndani ya nchi zao, uzalendo ulishajengwa kwa nchi zao karne na karne; ni vigumu sana kumkuta mtu wa Ulaya au Marekani akaisaliti nchi yake, labda kwa mtu kama Snowden alivyofanya japo inawezekana hakufanya usaliti kama inavyodaiwa, si ajabu ni System ya USA ipo kazini. Lakini hebu angalia jinsi watu wa nchi masikini wanavyosalitiana wao kwa wao, leo hii ni jambo la kawaida kumkuta mwanachama wa chama fulani anakisaliti chama chake kwasababu ya njaa ya fedha au madaraka, je umeshawahi kusikia mwanachama/kiongozi muandamizi wa chama fulani cha siasa kwa nchi za Ulaya/USA amekisaliti chama au hata kukihama kwasababu yakukosa nafasi yakugombea nafasi za juu za chama hicho? ( mfano kutoka Democtrat kwenda Republican). Nimekupa mfano huo ili tu ujue kuwa sisi ni bado sana, Tunatakiwa kwanza kujenga misingi imara ya kimaisha na kimaendeleo kwa watu wetu na nchi na wakati huohuo kuwajenga uzalendo wanachi wetu hasa wakiwa bado na umri mdogo kwasababu uzalendo ni sawa na IMANI na kuithamini imani hiyo kwa dhati ya moyo na hatimaye itakuwa ni suala lakurithishana vizazi na vizazi. Nikupe mfano mwingine mdogo: Hebu fanya utafiti wa wa Tz wanaoishi nje ya nchi, utakuta wengi hata kama mambo yamewanyookea huko lakini hawakumbuki ndugu zao waliowaacha nyumbani hasa WAZAZI wao, wengine wanakwenda kipindi cha misiba tu huku wamevalia miwani nakulia kwakupiga vifua tu eti My My My My Rest In Peace. Ipo mifano mingi hai, ni 5% tu ya wa tz waliopo ughaibuni wanakumbuka kwao. Hivyo sio busara kuilinganisha tz na nchi zilizoendelea ktk suala la uraia wa nchi mbili ni sawa na Babu na Kitukuu. Huu sio wakati wake. why not India, China, France, Italy, Rusia/ also these are developed country. Also why not Israel etc. Hawajaruhusu kwasababu ya changamoto za kiusalama. MARA NYINGI MASIKINI ANAKOSA UZALENDO SABABU YA UMASIKINI WAKE
 
Urai pacha kwa hawa watz mbona mta koma pia mbona rasimu ilishajibu yote haya,fuateni rasimu muache ujinga
 
Wenzetu wa Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi wote wanao uraia pacha. lakini sio sisi Tz. tuache ushamba ndugu zangu wabongo.
 
Ndugu yangu kibanga kampiga mkoloni, hata kama bado sijausoma huo wa india. mbona hizo nchi 4 za afrika mashariki wameupitisha huo uraia wa nchi 2?. au wewe unadhania hao jirani zetu hawana uchungu na nchi zao?. wenzenu tuko huku nje ya nchi tunatafuta maisha ili tujenge nyumbani, tusomeshe ndugu na jamaa zetu. na wala sio kwamba sisi ni wahaini.
 
Wenzetu wa Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi wote wanao uraia pacha. lakini sio sisi Tz. tuache ushamba ndugu zangu wabongo.
uraia pacha ni adui mkubwa wa nchi ya Tanzania. hakuna mtu anaweza kutumikia mabwana wawili. nashukuru kwa mtoa mada, nashukuru sana. nilikuwa sijajua huo mbadala ambao rasimu imeweka, kwa mfano wa india, naona kwakweli hilo ndilo suluhisho tosha kwa hawa wasaliti wa nchi yetu, na kama watawekwa kwenye kundi hili maalum wataweza kuendelea kumiliki ardhi walizoachiwa na wazazi wao bongo, na wataweza kununua ardhi n.k. tofauti na hapo kwa sasa hawaruhusiwi hata kumiliki ardhi isipokuwa kwaajili ya uwekezaji kwa kupitia tanzania investment centre (sio kienyeji, lazima wapite pale). mtu anapoamua kuukana uraia wa nchi yake mbele ya mzungu (most of these betrayers have not sacrifice their tz citizenship for an african country isipokuwa S.africa, nchi nyingi wametusaliti nazo ni zile zilizoendelea). sasa anapoamua kuuuza utz wake mbele ya mzungu ili apate mkate, anakuwa ana uuza urithi wake na haki zake zote ambazo angepata kama mtz, ikiwemo haki ya kumiliki arhi n.k (achilia mbali hiyo ya kupiga kura kwasababu najua sio priority yao...hahaha).that means kwa sasa kwasababu hatuna uraia pacha na hawajawekwa kwenye kundi maalumu, watz tukiwagundua tu tunatakiwa kuchangamkia ardhi zao wanazomiliki bila kupitia TIC, tuwachongee kwa mamlaka za ardhi, revocation ifanyike (kila ardhi yenye hati imekuwa registered hivyo kama umeregista tutaona jina lako) au hata zile unregistered tuzitafute ili tuzitumie sisi watz watuuzie au zigawanywe kwa wengine kwasababu wenye nazo walikuwa tayari kuzikosa mbele ya mzungu ili wapate mkate. hili litakuwa fundisho kwa watz wanaosaliti uraia wao.

jamaa ameongea vizuri sana, sipati picha mtz akiwa na uraia wa tz na Rwanda pamoja, na kuna siku tz tukaamua kwenda kigali kuwachapa yeye kama mjeshi wa tz tunamuamini vipi? kuna mtu anaweza kushasaliti ndugu zake wa damu? vivyohivyo, akiiiba hela akakimbilia nchi ambayo haina ushirikiano na tz ktk mutual legal assistance na nchi hiyo ilimpa uraia, yeye atakua amekimbilia kwenye nchi yake na nchi yake itamlinda, how can we recover our properties.....kama kuna nchi nyingine zilidanganyika kuleta uraia pacha ni hizo tu, tz kamwe hakutakuwa na uraia pacha, hautusaidiii, hauna faida kwetu. wasalaam Mtimti.
 
Ndugu yangu kibanga kampiga mkoloni, hata kama bado sijausoma huo wa india. mbona hizo nchi 4 za afrika mashariki wameupitisha huo uraia wa nchi 2?. au wewe unadhania hao jirani zetu hawana uchungu na nchi zao?. wenzenu tuko huku nje ya nchi tunatafuta maisha ili tujenge nyumbani, tusomeshe ndugu na jamaa zetu. na wala sio kwamba sisi ni wahaini.
kwahiyo kama wenzio wakitoa harufu chafu mbele za watu na wewe unatoa, wakijisaidia haja kubwa na wewe unachojoa nguo unatita? wao ni wanyarwanda, waganda, warundi na wakenya, sisi ni watz.

ujifunze kwamba kama alivyosema uyo jamaa, kati ya nchi ambazo zilitakiwa kuwa na uraia wa nchi mbili ni india kwasababu wahindi wapo dunia nzima, angalia waliopo tz uhindini kila mkoa kuna uhindini, canada, marekani, asia huko ulaya n.k, wahindi nje ni wengi sana na india ilitakiwa kutoa uraia pacha kwa wahindi, lakini kwa kupima garama waliona hii ni hatari kwa nchi ya india hata kama wengi wa hilo kundi maalumu wengekuwa ni wahindi pure (kama kina manji, kina dewij etc), hivi dewij ambaye ni mbunge wa tz unafikiri wahindi wanamwamini kwamba ataisaliti tz kuliko india? hata kama wanaona ni mhindi mwenzao lakini hawawezi kumwamini asilimia mia, ndio maana wakawapa kundi maalumu na ndilo tutakalowapa ninyi. hamtakuwa na haki ya kupiga kura, kugombea uongozi etc, lakini kwasababu nyie ndi watoto wetu kaka zetu daa zetu wa damu basi mtapata kundi maalumu mnapoingia na kukaa tz na mtamiliki mali. unaelewa?
 
uraia pacha ni adui mkubwa wa nchi ya Tanzania. hakuna mtu anaweza kutumikia mabwana wawili. nashukuru kwa mtoa mada, nashukuru sana. nilikuwa sijajua huo mbadala ambao rasimu imeweka, kwa mfano wa india, naona kwakweli hilo ndilo suluhisho tosha kwa hawa wasaliti wa nchi yetu, na kama watawekwa kwenye kundi hili maalum wataweza kuendelea kumiliki ardhi walizoachiwa na wazazi wao bongo, na wataweza kununua ardhi n.k. tofauti na hapo kwa sasa hawaruhusiwi hata kumiliki ardhi isipokuwa kwaajili ya uwekezaji kwa kupitia tanzania investment centre (sio kienyeji, lazima wapite pale). mtu anapoamua kuukana uraia wa nchi yake mbele ya mzungu (most of these betrayers have not sacrifice their tz citizenship for an african country isipokuwa S.africa, nchi nyingi wametusaliti nazo ni zile zilizoendelea). sasa anapoamua kuuuza utz wake mbele ya mzungu ili apate mkate, anakuwa ana uuza urithi wake na haki zake zote ambazo angepata kama mtz, ikiwemo haki ya kumiliki arhi n.k (achilia mbali hiyo ya kupiga kura kwasababu najua sio priority yao...hahaha).that means kwa sasa kwasababu hatuna uraia pacha na hawajawekwa kwenye kundi maalumu, watz tukiwagundua tu tunatakiwa kuchangamkia ardhi zao wanazomiliki bila kupitia TIC, tuwachongee kwa mamlaka za ardhi, revocation ifanyike (kila ardhi yenye hati imekuwa registered hivyo kama umeregista tutaona jina lako) au hata zile unregistered tuzitafute ili tuzitumie sisi watz watuuzie au zigawanywe kwa wengine kwasababu wenye nazo walikuwa tayari kuzikosa mbele ya mzungu ili wapate mkate. hili litakuwa fundisho kwa watz wanaosaliti uraia wao.

jamaa ameongea vizuri sana, sipati picha mtz akiwa na uraia wa tz na Rwanda pamoja, na kuna siku tz tukaamua kwenda kigali kuwachapa yeye kama mjeshi wa tz tunamuamini vipi? kuna mtu anaweza kushasaliti ndugu zake wa damu? vivyohivyo, akiiiba hela akakimbilia nchi ambayo haina ushirikiano na tz ktk mutual legal assistance na nchi hiyo ilimpa uraia, yeye atakua amekimbilia kwenye nchi yake na nchi yake itamlinda, how can we recover our properties.....kama kuna nchi nyingine zilidanganyika kuleta uraia pacha ni hizo tu, tz kamwe hakutakuwa na uraia pacha, hautusaidiii, hauna faida kwetu. wasalaam Mtimti.

Mkuu Hute,

Mimi nimemwelewa sana huyu mheshimiwa Humphrey Polepole na asiemwelewa anasema nini itakuwa ni basi tu.

Mimi ni mmoja wa watanzania wanaoishi ughaibuni kwa miaka mingi sana na mpaka leo bado natumia pasi ya kusafiria ya Tanzania, na katika miaka hiyo yote nimekwishapewa nafasi ya kuziomba pasi za kusafiria za nchi zaidi ya tatu za Ulaya, lakini nimekuwa na wazo jingine au "second thought" kuhusu kuchukua pasi hizo.

Lakini inasemwa kwamba baadhi ya viongozi wa kitanzania ambao leo hii wanashikilia nafasi nyeti ndani ya serikali ya Tanzania, wanahodhi pasi za kusafiria za ama US au UK, Comoros au nchi zingine.

Sasa tukianza kupiga kelele kutaka watanzania wengine wasipewe haki ya kutambuliwa, kwamba wapo sehemu mbalimbali duniani lakini wanaishi ng'ambo hata kama kwa sababu mbalimbali walipewa pasi za kusafiria za nchi zingine, hiyo inakuwa si haki.

Huo mfano wa India ni mzuri sana na unaweza kutumika kwa Tanzania ila ni lazima nyumba isafishwe kwanza kabla ya kuangalia nje kama kunahitaji usafi.

Viongozi wote waliomo serikali wenye pasi za nchi zingine (kama inavyodaiwa) wajulikane na baada ya hapo, wale wote wenye pasi za kusafiria za nchi nyingine wajiorodheshe kule uhamiaji na ijulikane idadi yao.
 
Back
Top Bottom