Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Urafiki wa muda mrefu baina ya Godbless Lema na Mawazo Alphonce umefikia hatua ya kutishiana kumalizana kisiasa.Ikumbukwe Lema na Mawazo walikuwa wanachama wa TLP kabla ya kujiondoa na kujiunga na CHADEMA na CCM respectively.Lema kupitia radio 5 amekuwa akijigamba atahakikisha Mawazo anashindwa kutetea nafasi ya udiwani Sombetini kwasababu ni yeye aliempeleka CCM na kumpigania hadi kupata nafasi ya udiwani.
Mawazo Alphonce kwa upande wake amedai Lema alitapeli watu kiasi cha tsh 3,6000,000/ kama ada ya kiingilio cha wanachama kupitia taasisi PTN [Positive Thinker Network] na vifaa vya ujenzi vyenye thamani tsh 4,428,000/=.Lema aliweza kufanya utapeli huo kwa kumweka mke wake Bi Neema Lema mweka hazina wa PTN.kabla ya kutimuliwa yeye na mke wake.
Mawazo Alphonce pia amedai Lema hakumaliza elimu ya msingi huku kwako Nronga Machame.anashangazwa sana kusikia Lema ana shahada ya juu [Advance Diploma Human Resource Managemant].Bwana Alphonce Mawazo ametoa ahadi kupitia radio 5 kwamba siku Lema atakapoweza kuwasilisha vyeti vya kuhitimu shahada anayodai anayo yeye Mawazo ataondoa jina lake kutetea udiwa na kumpigia kampeni mgombea wa CHADEMA.
Nina hakika wapo waJF wengi hapa Arusha wamefuatilia malumbano haya lakini kwakuwa yanamdhalilisha mbunge wao mtarajiwa hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kuhabarisha wanajamvi.Pia nina hakika waraka wa kumkashifu Lema utakuwa umesomwa na watu wengi lakini kama ilivyo ada na mazoea watu wamepiga kimya.
Tayari waraka wa kumchafua Bwana Lema umeshatoa na kusambazwa kama pipi sehemu mbali mbali mkoani Arusha.
"JE UTAPENDA KUONGOZWA NA MBUNGE TAPELI"
Napata taabu kidogo kuattach bado nafanya juhudi ikiwezekana mtausoma waraka wenye kichwa cha habari hapo juu.
Maoni yangu.
Nadhani Lema ameingia kirahisi kwenye mtego wa malumbano yasiyokuwa na tija na pengine CCM wamekusudia kuendelea ili apoteze muda badala ya kujikita zaidi kwenye lala salama ya kampeni za ubunge.
Pia si sahihi Lema kugombana na mgombea udiwani na kumwacha mgombea nafasi ya ubunge akiendelea kupeta.Madhaifu mengi ya Lema yalikuwa hayafahamiki sawasawa kwa wapiga kura sasa yameanza kufahamika hasa suala la elimu.
Radio 5 inamilikiwa na Lowassa, Lema kukubali kuitumia ni ukosefu wa akili kupindukia.Hii radio iko pale kuwasaidia CCM na mtandao wa Lowasa sioni sababu za msingi mtu anayegombea ubunge ashindwe kujua hili.