Elections 2010 Urafiki wa Lema na Mawazo wafikia ukingoni

Chenge shule yake kali sana kama ya Obama na Baba yake - Wote wamesoma chuo kimoja.

Pamoja na Chenge kusoma shule nzuri sana na kuwa Mwanasheria mzuri, badala apiganie awe Rais wa nchi kama Obama, yeye anapigania KUIIBIA nchi yake. Kama shule zenyewe ndiyo hizi, sijui zinawasaidia vipi.................

Msuya niliambiwa kwa hesabu alikuwa mzuri sana, kaishia tu kuungza BoT zetu.

CCM wasomi kibao lakini ndani ni kama Maboga, vimbegumbegu tu, heheheeee ..................



attachment.php

Heshima kwako Sikonge,

Mkuu wangu nakuheshimu sana jaribu kuungani dot.

[1] Godbless Lema alitakiwa kusema kweli kuhusu elimu yake.Katiba ya JMT iko wazi kabisa,mgombea ubunge na udiwani [urais sina hakika]anatakiwa ajue kusoma na kuandika.Nina hakika G Lema ana vigezo hivyo hakuwa na sababu za msingi kujipachika elimu asiyokuwa nayo.

[2] Ni kosa la jinai kudangaya au kufoji elimu sidhani ninatakiwa kutoa maelezo marefu ili uelewe.

[3] Ikiwa Lema anadangaya mambo madogo kama haya tena bila sababu za maana je unadhani atakuwa mwakilishi mzuri ?.

[4] Suala la Lema halina uhusiana wowote na picha alizozibandika Kachanchabuseta.Hana hoja hakutegemea hii maneno ya Lema ingetia timu jamvini.

NB;Tayari vyama vya CCM,CUF,demokrasia makini na TLP vina andaa utaratibu wa kutoa mkanda wa mdahalo wa TBC1 ili watu wengi wajionee wenyewe Lema alivyosema uongo.Pia taratibu za kumburuza mahakani haziko mbali.
 
Mkuu Kachanchabuseta vipi mbona umetimua mbio nilikuwa nafurahia picha zako yaelekea wewe ni msanii mzuri endelea kuleta burudani lakini mwisho wa siku lazima ujibu hoja.Najua kumekuwa na juhudi mbali mbali tena wakati mwingine za kijinga za kuficha maovu kwasababu anayetenda ni mtu wetu ?.
 
Mbavu sina yaani wakati mwingine unaweza kumshangaa sana mwanadamu kosa la kudangaya angefanya mgombea wa CCM au chama kingine pangechimbika hapa lakini kosa hilo hilo akifanya mgombea wa CHADEMA watu wananuna hawataki lisemwe na likisemwa watafanya kila juhudi kupoteza maana.Post imefika #22 hakuna majibu bali viroja !!!!!!
 
Hizo kasfa dhidi ya Lema siyo za kweli vinfinevyo polisi wangekuwa wamemweka mkononi siku nyingi sana.

Tayari waraka wa kumchafua Bwana Lema umeshatoa na kusambazwa kama pipi sehemu mbali mbali mkoani Arusha.

"JE UTAPENDA KUONGOZWA NA MBUNGE TAPELI"

Napata taabu kidogo kuattach bado nafanya juhudi ikiwezekana mtausoma waraka wenye kichwa cha habari hapo juu.

Hivi utapeli wa CCM wanafikiri tutausahau na madhara yake kwa jamii?
 
Kale kaugonjwa ka chademaism kamewanasa wengi ebu tuwe wakweli kidogo Ruta wewe ni mkaazi wa Arusha nimesoma post zako kibao zimeenda shule haswaa.Polisi wanawezaje kumkamata Lema ?.Wenye uwezo wa kumshitaki ni wagombea wenzake,wapiga kura.ni kwanini Kihiyo,Mary Nagu,Dr Kamala na wengine kibao hakukamatwa na polisi?.
 
Wacha nikapige mvinyo kidogo naona hakuna wakujibu hapa wote wamelowa kisa kilaza wao kaanza kuumbuliwa.
 
Wakuu kabla sijaondoka labda nimsaidie Ruta,

[1] Naomba nielezwe kama Lema alianzisha Positive Thinker Network.Labda tuanzie hapa kama jibu ni ndiyo je hiyo taasisi bado iko kama iko je Lema bado ni mwanachama wake ?

[2] Lema ana Advance Diploma in Human Resources Management kama jibu ni ndiyo alisoma chuo gani ?mwaka gani ?.Lema huyu huyu alipokuwa akigombea ubunge mwaka 2005 alidai ana Diploma in Theology. Je ni kwanini mwaka huu anadai ana ADHRM wakati hana hata sifa za kujiunga na hiyo kozi.

[3] Wapo baadhi ya watu mashuhuri wametajwa kwenye waraka mfano Mzee Kagengere wa Case book shop,yupo Bwana Shoo wa sky tel kwanini ajakanusha au Lema asikimbilie kwenye vyombo vya dola na habari kama alivyokimbilia TAKUKURU ?.Great thinker wanakuja na majibu ya kimakamba makamba wengine wana copy & paste ! nasisitiza Lema na wapiga debe wake wmeashakutana na hii kitu wamepiga kimya na wapenzi wake kaani kimya msiwe wapambe wa mabo ya kijinga.
 
Mkuu Rutashubanyuma jibu hoja acha viroja.

Ngongo
Saa nyingine kunyamaza kimya ni jibu zuri sana.... kuepuka wote kuonekana mazuzu..... naona sasa unalazimisha watu wajadili upupu.... kaa subiria naona thread imejamba!!!! :hand::hand::hand::hand::hand:
 
Back
Top Bottom