Urafiki wa Kikwete na Lowassa

Urafiki wa Kikwete na Lowassa

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,804
Reaction score
24,434
Kama kweli Lowasa na Kikwete ni marafiki wazuri sana na wanategemea kurithishiana madaraka, basi wote wawili hawana akili. Iwapo Lowassa ndiye anayejitangaza kuwa ni rafiki wa karibu sana wa Kikwete na urafiki wao haukuanza jana, basi huenda atakauwa anajipendekeza kusudi Kikwete asimtose kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Iwapo Kikwete ndiye anayemshauri Lowasa kugombea kwa nia ya kumsaidia kulinda legacy yake, basi atakuwa amepotea sana kwa sababu Lowasa alishasema kuwa baada ya yeye kuondoka Uwaziri mkuu serikali ya Kikwete iliyumba sana; alisema hivyo kwa maana ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa serikali ya Kikwete.

Urafiki wao huu ama haupo au ni wa kinafiki, kwani sijasoma mahala popote ambapo Kikwete ama amemsaidia rafiki yake huyo kupata uteuzi hata kwa mawazo tu au kuuandaa umma kwa kuushawishi kumkubali Lowasa kuwa ndiye kiongozi bora.

Nyerere alishawishi sana watu kumkubali Mwinyi na vile vile kumkubali Mkapa.
 
Kumbuka tu in politic there are no permanent friends. Lowassa alibeba lawama za madhambi ambayo Kikwete alikuwa mhusika mkuu, aliahidiwa kurudishwa serikalini hapo baadaye, haikutokea. Sasa Kikwete anaogopa Lowassa anajua madudu yake, na huenda akamuumbuua kama vile Kikwete alivyomuumbua Mkapa kwa kunasa nyaraka zake za siri.
 
JK ni kiongozi wa chama hivi unadhani ni rahisi kumuuza mgombea wake wakati yeye ndio dira na kiongozi wa wagombea wote 42. huoni kufanya hivyo hadharani ni kukimega chama? Nyerere alifanya hivyo kwa mkapa kwa kuwa hakuwa kiongozi wa chama bali mstaafu.

jambo jingine ni kuweka kumbukumbu sahihi, kwamba wakati wa awamu ya pili mwinyi hakuwa chaguo la Nyerere bali dr Salim.

Urafiki wa viongozi tena katika siasa huendana na mazingira ya siasa yenyewe kwa wakati husika. you just wait and see on 12/07/2015. Lowassa is powerful over the powerless
 
Huyu mleta mada nahisi atakuwa ni shekhee ponda ni mchochozezi kweli kweli
 
Kumbuka tu in politic there are no permanent friends. Lowassa alibeba lawama za madhambi ambayo Kikwete alikuwa mhusika mkuu, aliahidiwa kurudishwa serikalini hapo baadaye, haikutokea. Sasa Kikwete anaogopa Lowassa anajua madudu yake, na huenda akamuumbuua kama vile Kikwete alivyomuumbua Mkapa kwa kunasa nyaraka zake za siri.

Kati ya vitu huwezi kumhusisha Kikwete ni wizi,anaweza akawa na madhaifu ya upole hapa na pale na kuwa na moyo wa huruma kuwachukulia hatua kali waliokosea lakin Kikwete is clean.Hana tamaa na pesa.Weka hiyo kwenye kumbukumbu zako.

Lowassa ni mfanyabiashara wenye hisa zake katika deal mbalimbali, hatufautiani sana na Chenge kama alivyokiri Chenge kuwa yeye ni nyoka mwenye makengeza,anayeangalia sana palipo na pesa.
 
Mbona pale stadium hamkuyasema haya.
Unaposema kikwete kamuumbua mkapa una maana gani mbona Mkapa anaendelea na shughuli zake na anaendelea kuheshimika.
 
He is powerless over the powerful!!
Subirini mzione muscles za mwenyekiti.
siasa raha sana..... kumbuka uwekezaji huu una zaidi ya miaka ishirini hivyo sayansi ya siasa itakupa matokeo yake tar 12/07
 
siasa raha sana..... kumbuka uwekezaji huu una zaidi ya miaka ishirini hivyo sayansi ya siasa itakupa matokeo yake tar 12/07

Miaka 20 ni ya kujivunia kwenye nchi kongwe kama hii??
 
Kumbuka tu in politic there are no permanent friends. Lowassa alibeba lawama za madhambi ambayo Kikwete alikuwa mhusika mkuu, aliahidiwa kurudishwa serikalini hapo baadaye, haikutokea. Sasa Kikwete anaogopa Lowassa anajua madudu yake, na huenda akamuumbuua kama vile Kikwete alivyomuumbua Mkapa kwa kunasa nyaraka zake za siri.

acha unafiki, kwanini unawagombanisha mkapa na kikwete,eleza sifa kiongozi wako sio kuleta mboyoyo hapa.
 
Huyu mleta mada nahisi atakuwa ni shekhee ponda ni mchochozezi kweli kweli

Mimi siyo Shehe Ponda, na wala sijui elimu ya uislamu kama alivyo shehe ponda; ila tuliambiwa kuwa ndege wa aina moja huruka pamoja.

ducks2.jpg
 
Naona kwenye Uzi huu wamejaa wachochezi na wapendwa kujua maisha binafsi za watu. Kwenye uchaguzi huu hakuna cha urafiki wala cha uwadui. Kilichopo ni mwenye nguvu na anayekubalika. Lowassa hakuna hata chembe ya Shaka kuwa ndiyo anayekubalika na mwenye nguvu ndani na nje ya CCM.

Tungeweza kupata combination ya Lowassa na Dr. Slaa hii ingekuwa safi Sana.
 
Mbona naona kama kikwete hanaga time na lowassa.
 
Kichuguu

Mwalimu Kichuguu,

Katika urafiki huu, mmoja aliubeba msalaba wa aibu na kuwajibika kwa niaba ya mwenzake. Aliyekingiwa kifua badala ya kurudisha fadhila, kageuka kuwa ndumilakuwili.

Hili lazima liwe somo kwa Wanasiasa wetu, waachane na ushirika wa kichawi. Ni heri watu waaminiwe na kupewa dhamana na majukumu kutokana na uzalendo na umahiri wa kuwajibika kwa ufanisi kwa kufuata maadili na si kuutaka Urais kama mashindano ya Urembo!
 
Last edited by a moderator:

Mchungaji Rev. Kishoka, katika siasa hakuna rafiki wa kudumu, ukiona rafiki yako anakuwa liability unamtosa, na haya ndio ya EL na JK
 
Last edited by a moderator:
urafiki wao uishie kwenye karata kulamba karanga na jembe si ktk rasilimali zetu kulamba madini na gesi!Mtanzania amka!!
 
He is powerless over the powerful!!
Subirini mzione muscles za mwenyekiti.

Mi nashauri huduma za afya ziboreshwe dodoma hasa kipindi hiki majeruhi watakuwa countless😀😀
 
Kati ya vitu huwezi kumhusisha Kikwete ni wizi,anaweza akawa na madhaifu ya upole hapa na pale na kuwa na moyo wa huruma kuwachukulia hatua kali waliokosea lakin Kikwete is clean.Hana tamaa na pesa.Weka hiyo kwenye kumbukumbu zako.

Lowassa ni mfanyabiashara wenye hisa zake katika deal mbalimbali, hatufautiani sana na Chenge kama alivyokiri Chenge kuwa yeye ni nyoka mwenye makengeza,anayeangalia sana palipo na pesa.
I beg to differ. Kikwete ni mwizi. Alianza enzi za IPTL akiwa waziri wa nishati na madini. Soma taarifa ya Brian Cocksley ndio utaelewa. Ametengeneza hela nyingi tu katika mikataba ya madini pamoja na kuhongwa na wazungu wanaochimba madini, hasa wale wa Nyamongo na ndiyo maana hawakuguswa licha ya kwamba ndugu zetu waliuawa huko kwa visingizio vya kuvamia eneo la machimbo ya mwekezaji. Kikwete is not clean at all.
 
Back
Top Bottom