Upvc vs alluminium windows

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
Wakuu napata tabu sana kwenye uchaguzi wa madirisha mazuri kwa ajili ya ujenzi wa makazi yangu,

Naombeni uchambuzi wa kitaalamu ni nini tofauti ya haya madirisha?? Je na kwa bei ipi ni bei zaidi ya

Nyenzake? Vipi kwenye ubora? Etc etc sehemu gani ni the best na affordable kupata hizi bidhaa...?

JF is the home for great thinkers i believe i'll get all the answers here.

Welcome!!
 
Wakuu napata tabu sana kwenye uchaguzi wa madirisha mazuri kwa ajili ya ujenzi wa makazi yangu,

naombeni uchambuzi wa kitaalamu ni nini tofauti ya haya madirisha?? Je na kwa bei ipi ni bei zaidi ya

nyenzake? Vipi kwenye ubora? Etc etc sehemu gani ni the best na affordable kupata hizi bidhaa...?

Jf is the home for great thinkers i believe i'll get all the answers here.

Welcome!!

mkuu uko wapi kwani!? Nipm namba yako sisi tunafunga hizo alluminium kwa affordable price!!
 
Ungetoa maelezo ya kutosha kuhusu alichokiulia ZionTZ mfano aina za madirisha,gharama zake,picha za madirisha ili uwasaidie na wengine gwankaja
 
Last edited by a moderator:
Wakuu napata tabu sana kwenye uchaguzi wa madirisha mazuri kwa ajili ya ujenzi wa makazi yangu,

naombeni uchambuzi wa kitaalamu ni nini tofauti ya haya madirisha?? Je na kwa bei ipi ni bei zaidi ya

nyenzake? Vipi kwenye ubora? Etc etc sehemu gani ni the best na affordable kupata hizi bidhaa...?

Jf is the home for great thinkers i believe i'll get all the answers here.

Welcome!!
 1. Advantage kubwa ya PVC dhidi ya Aluminium ni kupenyesha ubaridi kidogo au joto kidogo, Aluminium ni good conductor of heat, PVC ni bad conductor of heat, hivyo kwa nchi za wenzetu, zenye winter, madirisha ya PVC kwao ni bora zaidi kuliko madirisha ya aluminium.
 2. PVC inapitisha unyevu kwa shida, kuliko aluminium, hivyo kwa nyumba za beach houses, chunvi inakula alumium, chuma ndio balaa kabisa, hivyo pvc hailiwi na chumvi na unyevu!.
 3. Monekano wa PVC ni mzuri zaidi kuliko muonekano wa Aluminium.
 4. PVC in a more choice of colours kuliko aluminium ambayo in a limited choice of colors unless owe ni ya kupaka ambapo after a certain period of time, rangi inababuka!. PVC in atengenezwa na hiyo rangi hivyo haibabuki.
 5. PVC inapindishika kwa urahisi, malleable, kwa sababu ni plastiki na ni laini, hivyo unaweza kutengeneza madirisha ya shape mbali mbali kwa urahisi haswa arch windows, aluminium inapindishika kwa mbinde!.
 6. Aluminiun ni imara zaidi, na nzito zaidi, PVC sio imara sana na ni nyepesi, hivyo madirisha ya aluminium over a long period of time, ile funga fungua, inalika kidogo kidogo hivyo inakuwa a bit loose!.
 7. Kana utachagua sliding windows, aluminium in a slide kwa sauti ya scratching, hivyo ni kelele, PVC in a slide kwa kuteleza bila kelele.
 8. Wear and tear ya PVC ni muda mfupi zaidi kuliko alminium, na tena kama PVC ya China ndio balaa, kama ulichagua white profile, ndani ya miaka 5, inageuka cream, afadhali uchague PVC ya Uturuki, aluminium haibadiliki rangi kwa muda mrefu!.
 9. Aluminium ni fire resistance, hivyo nyumba ikishika moto, haukolezwi, PVC ni mkolezo ikishika moto imeshika hutaambulia hata jivu!.
 10. Wabunifu wa PVC waliidhamiria kwa nchi za ulaya, hili joto la hali ya juu sana la bongo sio rafiki kwa PVC.
 11. Bei ya PVC ya ukweli, iko juu kuliko bei ya alumium ya ukweli!, ujio wa Mchina kwenye soko, umepelekea kupata very cheap pvc na very cheap aluminium, ushauri wangu, usikimbilie cheap just to save money, cheap is expensive, better go for a best quality hata kama zitakutoka!.
 12. Aluminium na PVC ni kwa nchi za wenzetu wenye limited natural resources, madirisha ya mbao, mninga, ndio mpango mzima, kwa sababu wenzetu hawana!, nenda masaka ukaone jinsi wazungu wanavyokimbilia nyumba za mbao!, ila pia kuna watu wanapenda PVC au Aluminium kwa ulimbukeni tuu wa muonekano, na kuna nyumba nilikuta hadi artificial grass kwenye garden ya jamaa mmoja ili kuonyesha jeuri ya pesa!, kumbe ni ulimbukeni tuu, Dubai hawana mvua, artificial grass kwao sawa, hapa tuna mvua why usitengeneze live garden yenye uhai?!.
Kwa mjadala mpana, tembelea hapa pvc vs aluminium Windows - JamiiForums

Pasco.
 
 1. Wear and tear ya PVC ni muda mfupi zaidi kuliko alminium, na tena kama PVC ya China ndio balaa, kama ulichagua white profile, ndani ya miaka 5, inageuka cream, afadhali uchague PVC ya Uturuki, aluminium haibadiliki rangi kwa muda mrefu!
 2. Bei ya PVC ya ukweli, iko juu kuliko bei ya alumium ya ukweli!, ujio wa Mchina kwenye soko, umepelekea kupata very cheap pvc na very cheap aluminium, ushauri wangu, usikimbilie cheap just to save money, cheap is expensive, better go for a best quality hata kama zitakutoka

Pasco.

Hakika mkuu Pasco uchambuzi wako ni mujaarabu sana na uko sahihi kwa 100%

kuna siku nilipita duka/show room moja iko makumbusho mkono wa kulia kama unaenda victoria, pale niligundua duka lile ni la waturuki wenyewe na alikuwepo mzungu pale, basi yule mhudumu wa pale akanipa maelezo ya kina sana, ila bei yao sasa ni balaa, tofauti ya kama laki moja na ushee kwa mita moja ya mraba ukilinganisha na gharama za wenzetu wazawa ambazo wanatumia malighafi za kichina.
gharama ya kazi yangu endapo ningetumia aluminium ingekua kama 4.5M, lakini kwa pvc ya waturuki hesabu zilikua zinacheza kwenye 14M, bado najaza kibubu kikijaa ntaenda kwa mturuki, ghali lakini you get the high quality products.
 
Last edited by a moderator:
mjomba mbona hujatoa ushauri wa kitaalam kama mleta mada alivyoomba/ umekimbilia kusaka tenda? hujui ushauri utasaidia wengimkuu uko wapi kwani!? Nipm namba yako sisi tunafunga hizo alluminium kwa affordable price!!
 
Madirisha ya Mbao mazuri yanakuwaje?maana nowadays ni mwendo wa aluminium. Plz niaaidien maana na mimi niko na mtihani huo.
 
Back
Top Bottom