Upunjaji wa Mafuta Kituo Cha Mbezi Kwenda Goba

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,416
12,618
Nimekuwa nikiweka mafuta mara nyingi sana kwenye hiko kituo cha mafuta kilichopo njia ya Kutoka Mbezi kuelekea Goba, kwa kipindi cha nyuma sikuwahi kuona tatizo.

Kama wiki 2 zimepita niliweka mafuta asubuhi ya sh 10,000/- ambayo kwa kawaida ninaendesha kama 50 km kama hakuna foleni, bahati mbaya sana gari ilizima baada ya kama km 29. Nikajua labda hesabu zangu siyo.

Leo nikaenda tena nikamwambia jamaa kuhusu hilo swala, akaniuliza tu kama dashboard yangu inasoma vizuri nikamwambia ndiyo, nikaweka tena sh 10,000/- story ikawa ile ile.

Inaweza kuwa tatizo ni gari langu lakini ningependa kutoa angalizo kwa watumiaji wengine wa hiyo center wawe makini. Cha kushangaza nikiweka mafuta vituo vingine hili tatizo sikutani nalo.
 
1.una gari gani?
2.condition ya barabara kila ukiendesha iko constant?
3.ulivyoweka ukatembea km 29 na siku iliotembea km 50 mshale kwenye gauge ulikuwa same position au chini?

Kesho nenda na gallon jaza 10,000 kweye gallon uone itafika wapi.
 
Ntawashtukiza siku moja kwa galoni nione itakapofika, kwa sababu baada ya siku ile ya kwanza nilijua ntakuwa nimekosea.

Ila nikawa makini kucheki kms kila ninapoweka mafuta, na mara nyingi ninakuwa na route ambayo ni consistent labda ningesema leo nimebadili njia ndo sababu.

Leo nimeenda kama kufanya uhakiki na kweli ikawa kama nilivyofikiri ndo maana nikawa na hizi doubts.
 
Kuna siku nilifikiri naibiwa mafuta kumbe mafuta yanavuja chini kwenye pipe inayotoka kwenye tenki.so gari ikawa inakula mafuta kinoma kumbe ukiwasha tu na kukanyaga kukanyaga moto mafuta yanaanza kumwagika...angalia gari yako kwanza
 
Nimekuwa nikiweka mafuta mara nyingi sana kwenye hiko kituo cha mafuta kilichopo njia ya Kutoka Mbezi kuelekea Goba, kwa kipindi cha nyuma sikuwahi kuona tatizo.

Kama wiki 2 zimepita niliweka mafuta asubuhi ya sh 10,000/- ambayo kwa kawaida ninaendesha kama 50 km kama hakuna foleni, bahati mbaya sana gari ilizima baada ya kama km 29. Nikajua labda hesabu zangu siyo.

Leo nikaenda tena nikamwambia jamaa kuhusu hilo swala, akaniuliza tu kama dashboard yangu inasoma vizuri nikamwambia ndiyo, nikaweka tena sh 10,000/- story ikawa ile ile.

Inaweza kuwa tatizo ni gari langu lakini ningependa kutoa angalizo kwa watumiaji wengine wa hiyo center wawe makini. Cha kushangaza nikiweka mafuta vituo vingine hili tatizo sikutani nalo.
Hata hivyo bado na gari yako inakula sana mafuta kiongozi ingawa sijajua ni gari aina gani coz hapo ni sawa na 10km/lt
 
Hata hivyo bado na gari yako inakula sana mafuta kiongozi ingawa sijajua ni gari aina gani coz hapo ni sawa na 10km/lt[/QUOTE

Mimi nina Gari Toyota sprinter Carib inatumia chini ya km 8 kwa lita na nikitumia AC ndiyo kabisa kms 6
Lakini kuhusu hicho kituo nami nimepata shaka.
Mtoa mada aweza kuwa sahihi kwenye tyhuma
Niliweka mafuta ya elfu 10 lakini nilienda kms 22 wakati, yakiyokuwa yanaishia ilikuwa 42 kms Lita 5+ sawa na ya hapo
 
Hata hivyo bado na gari yako inakula sana mafuta kiongozi ingawa sijajua ni gari aina gani coz hapo ni sawa na 10km/lt

Mimi nina Gari Toyota sprinter Carib inatumia chini ya km 8 kwa lita na nikitumia AC ndiyo kabisa kms 6
Lakini kuhusu hicho kituo nami nimepata shaka.
Mtoa mada aweza kuwa sahihi kwenye tyhuma
Niliweka mafuta ya elfu 10 lakini nilienda kms 22 wakati, yakiyokuwa yanaishia ilikuwa 42 kms Lita 5+ sawa na ya hapo
 
Nilijua mie tu ndo naona hili tatizo la kupunjwa, hiki kituo ni janga, ngoja nitahamia kile kipya nione nao wakoje.
 
Ntawashtukiza siku moja kwa galoni nione itakapofika, kwa sababu baada ya siku ile ya kwanza nilijua ntakuwa nimekosea.

Ila nikawa makini kucheki kms kila ninapoweka mafuta, na mara nyingi ninakuwa na route ambayo ni consistent labda ningesema leo nimebadili njia ndo sababu.

Leo nimeenda kama kufanya uhakiki na kweli ikawa kama nilivyofikiri ndo maana nikawa na hizi doubts.
Ahsante kwa angalizo.
Inabidi tuwe makini sana na hizi filling stations. Nimegundua kuhusu upungufu wa kiwango halisi cha mafuta katika usafiri wangu since two weeks sasa.

WMA ifanye ukaguzi wa ghafla kwenye hivi vituo ili kuhakiki mita za mashine za vituo
 
Leo nilifanya kama RRONDO alivyonishauri kwenda na galoni la lita 5, nikamwambia niwekee mafuta ya shilingi 10,000/-, katika hali ya kawaida mafuta yangemwagika, lakini cha kushangaza hata lita 4 na nusu haikufika.

Sikuongea kitu nikachukua mafuta yangu nikaondoka, kwenye pump bei ni 1,840/-, kwa shilingi 10,000/- nilitakiwa kupata lita 5.43 lakini hata lita 4.5 haikufika, almost lita nzima imepunjwa.

Inasikitisha sana, na nina uhakika kuna vituo vingine vingi vinacheza huu mchezo. Itabidi tuanze kuhabarishana wapi tunapata mafuta mazuri na kwa kipimo sahihi.
 
Hapo ndio ulitakiwa uchukue hatua......10,000/- ni lita 5.43 kama ulivyosema na gallon ni lita 4.6 hivi kwahio ilitakiwa imwagike lita nzima. Huo ni wizi na ushahidi unao hukutakiwa kuondoka tu hujasaidia chochote.
 
Kuna siku nilifikiri naibiwa mafuta kumbe mafuta yanavuja chini kwenye pipe inayotoka kwenye tenki.so gari ikawa inakula mafuta kinoma kumbe ukiwasha tu na kukanyaga kukanyaga moto mafuta yanaanza kumwagika...angalia gari yako kwanza

Mkuu ukisoma vizuri ni kwamba nikiweka mafuta kwingine hii shida sikutani nayo, na leo nimeenda na kidumu cha lita 5 akaniwekea mafuta ya sh 10,000 hayakufika lita 5 wakati bei kwa sasa nilitakiwa kupata 5.4 (mafuta yangemwagika kama nikiweka kwingine).
 
Hapo ndio ulitakiwa uchukue hatua......10,000/- ni lita 5.43 kama ulivyosema na gallon ni lita 4.6 hivi kwahio ilitakiwa imwagike lita nzima. Huo ni wizi na ushahidi unao hukutakiwa kuondoka tu hujasaidia chochote.

Nimwemweleza yule mhudumu kiutaratibu tu na yeye akasema hajui, pale hata bosi wake hakuwepo. Na hata sielewi unaanzia wapi kushtaki lakini nikaona ni vizuri tu kupeana angalizo kwa watumiaji.
 
Hilo ni jipu, haya mambo yapo sehemu nyingi sana, nafikiri ni muda muafaka kwa cc wateja/watumiaji kuchukua hatua stahiki
 
Nimekuwa nikiweka mafuta mara nyingi sana kwenye hiko kituo cha mafuta kilichopo njia ya Kutoka Mbezi kuelekea Goba, kwa kipindi cha nyuma sikuwahi kuona tatizo.

Kama wiki 2 zimepita niliweka mafuta asubuhi ya sh 10,000/- ambayo kwa kawaida ninaendesha kama 50 km kama hakuna foleni, bahati mbaya sana gari ilizima baada ya kama km 29. Nikajua labda hesabu zangu siyo.

Leo nikaenda tena nikamwambia jamaa kuhusu hilo swala, akaniuliza tu kama dashboard yangu inasoma vizuri nikamwambia ndiyo, nikaweka tena sh 10,000/- story ikawa ile ile.

Inaweza kuwa tatizo ni gari langu lakini ningependa kutoa angalizo kwa watumiaji wengine wa hiyo center wawe makini. Cha kushangaza nikiweka mafuta vituo vingine hili tatizo sikutani nalo.
mkuu embu eleza ni kituo gani cha kampuni ya mafuta zisije kuwa zile kampuni uchwara ambazo zimejengwa hivi karibuni baada ya lami kupita huko mbezi-goba road....
 
mimi naweka VICTORIA PETROL STATION...... sijutii
niliwahi jaribu station nyingine majanga tu
OILCOM ndo usijaribu kabisaaaaa

tena Oilcom hata kuweka mafuta kwenye vidumu hawakubali
...
 
mkuu embu eleza ni kituo gani cha kampuni ya mafuta zisije kuwa zile kampuni uchwara ambazo zimejengwa hivi karibuni baada ya lami kupita huko mbezi-goba road....

Mkuu ukitoka Goba Mwisho kuelekea Mbezi Luis ni kituo pekee cha kwanza upande wako wa kulia kama km 2 na mita kadhaa tu hivi, sidhani kama kuna kituo kingine uelekeo huo. Hiki kilianza kutengenezwa siku nyingi tu kabla hata ya lami.
 
Leo nilifanya kama RRONDO alivyonishauri kwenda na galoni la lita 5, nikamwambia niwekee mafuta ya shilingi 10,000/-, katika hali ya kawaida mafuta yangemwagika, lakini cha kushangaza hata lita 4 na nusu haikufika.

Sikuongea kitu nikachukua mafuta yangu nikaondoka, kwenye pump bei ni 1,840/-, kwa shilingi 10,000/- nilitakiwa kupata lita 5.43 lakini hata lita 4.5 haikufika, almost lita nzima imepunjwa.

Inasikitisha sana, na nina uhakika kuna vituo vingine vingi vinacheza huu mchezo. Itabidi tuanze kuhabarishana wapi tunapata mafuta mazuri na kwa kipimo sahihi.
Sasa nielewe kuwa hili limeanza kama wiki mbili tatu hadi sasa.
Kwa mfano niliweka mafuta vituo tofauti katika kata ninayoishi nikagundua ni kama wameambizana kupunguza ujanzo.

Lakini nilipokaza macho zaidi nikagundua vituo zaidi ya asilimia 90 vipo chini ya mmiliki mmoja ambaye hivi majuzi amekuwa ni gumzo wa wizi wa mafuta na masuala ya forodha bandarini.

Nahisi kodi wanyodaiwa ndivyo inakusanywa kiaina.
Stealing from marginalized
Make them pay for your mistakes
 
Back
Top Bottom