Mkuu wa mkoa Mororgoro Adam Malima amedhiinisha kuwepo upungufu wa waalimu 800 na watumkishi zaidi ya 500 sekta ya Afya, amesema hayo katika baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba leo Juni 11, 2025
====
Kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kimeibua changamoto ya upungufu wa watumishi wa umma katika sekta za elimu na afya, hali inayotajwa kudhoofisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kikao maalum cha kupitia na kutathmini hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, ameeleza kuwa sekta ya elimu inakabiliwa na upungufu wa walimu 800, sawa na asilimia 41 kwa shule za msingi na sekondari, huku sekta ya afya ikiwa na upungufu wa zaidi ya watumishi 500, sawa na asilimia 70 ya mahitaji.
RC Malima amesema changamoto hiyo imeathiri sana utoaji wa huduma bora kwa wananchi, na kutoa wito kwa menejimenti ya halmashauri kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa ili kuandaa hoja ya pamoja ya kudai watumishi wapya kutoka serikali kuu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba, Innocent Mwangasa, ameeleza kuwa licha ya changamoto hizo, halmashauri imefanikiwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo.
Nao baadhi ya madiwani wamesema kuwa vituo vya afya vinaelemewa kutokana na uhaba wa vifaa tiba na wataalam, huku uhaba wa walimu ukiathiri umakini wa wanafunzi na ubora wa elimu hivyo wameiomba Serikali kutupia jicho changamoto hizo
See translation