Upotoshaji wa padre kuoa watolewa ufafanuzi

mtanganyika wa kweli

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,420
1,720
UPOTOSHAJI WA MITANDAO KUWA PADRE AOA WATOLEWA UFAFANUZI

BAADA ya mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari kupotosha kuwa Kanisa Katoliki limemfungisha ndoa padri wake, imefafanuliwa kuwa, Padri akiomba kuondolewa upadri wake anaruhusiwa kuoa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini ameeleza kuwa,katika wito wa Upadri katika Kanisa Katoliki , mapadri hawaoi na hiyo ni sheria ama nidhamu ya Kanisa siyo ya Mungu hivyo Papa ana uwezo wa kuitengua.

“Katika Kanisa Katoliki Padri ni kasisi, ni kuhani anayetolea sadaka altareni. Kutokana na nidhamu ya Kanisa Padri haruhusiwi kuoa lakini pale anaposhindwa kuendelea na wito wake ama anapoonekana kwamba anashindwa kuuishi upadri wake anaruhusiwa kuomba kuacha na anaruhusiwa kulingana na taratibu za Kanisa.

Mapadri ambao mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari vinazungumzia siyo mapadri walishafuata taratibu zote na kupata kibali kutoka kwa Baba Mtakatifu kuwa wamefunguliwa na upadri wao umeondolewa hivyo wana uhuru wa kuoa kwani wamefanywa walei si mapadri.

Padri akishavuliwa upadri haitwi tena Padri wala hawezi kutoa huduma kama padri, ana haki za kuishi ulei wake. Kulingana na taratibu za imani ya Kanisa Katoliki mlei anafunga ndoa aishi na mume ama mke wake kwa uhalali na kuweka maagano yao mbele ya Mungu na hapo hakuna kosa.

Tatizo ni tafsiri ya wanahabari kukuza mambo na kusema padri wa Kanisa Katoliki kaoa wakati alishaondolewa upadri.

Dr Wilbroad Slaa alikuwa Padri wetu tena Katibu Mkuu wa TEC ambaye nilimrithi lakini aliacha upadri kulingana na taratibu za Kanisa akaoa, huyu mwingine Kalugendo naye vilevile alifuata taratibu yupo huru na wako sahihi.

Hakuna aibu Kanisa Katoliki iliyopata wala halijakosea. Tuna taratibu zetu ni mambo tu ya kuelewa,” amesema Askofu Kilaini.

Kwa upande wake Padri Stefano Kaombe aliyefungisha ndoa hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Petro Osterbay amesema kuwa, vyombo vya habari haviko sahihi kusema Padri wa Kanisa Katoliki ameoa kwani Kanisa likishamaliza taratibu zake za kumfanya padri mlei yaani kumuondolea ukasisi wake linamuondolea hadhi yake ya upadri.

“Kuna kuondolewa hadhi ya upadri na kufunguliwa kifungo cha useja. Mtu anaweza kufanywa mlei lakini kifungo cha useja kikabaki au unaweza kufunguliwa vyote.

Bw. Privatus Kalugendo alifunguliwa vyote Septemba 14 mwaka 2008 kwa hati ya Papa yenye Protokali No.4182/08.

Hivyo Bw. Kalugendo alikuwa huru tokea siku hiyo kufunga ndoa kwani hakuwa padri na hakufungwa useja.
 
Bahati mbaya sana ya watanzania wanaaminishwa mambo wasiyoyajuwa kwahiyo wanapokea tu kama dodoki.

Kuna kitu sio askofu Kilaini wala pd Kaombe amekisema. Ukishapewa upadre wewe ni padre milele si papa wala nani anayeweza kukuondolea kwa sbb upadre ni sakramenti.

Upadre sawa na ubatizo vinaacha indelible mark kwa muhusika chapa isiyofutika milele. Mf ukishabatizwa halafu ukaingia imani ya kislamu wewe bado ni mkristu kwa sbb ya ile chapa isiyofutika milele.

Kwa sababu hiyo Dr Slaa na Karugendo wote ni bado ni mapd wa kanisa katoliki tena wanaruhusiwa ktk mazingira maalum kutoa huduma za kanisa yakiwemo masakramenti.

Tofauti ya hawa ni kwamba wenyewe wameomba ruhusa inaitwa laicization kumbe kilichoondolewa ni hadhi tu ila sio essence ya upadre wenyewe.

Ni makosa makubwa kufikiri kwamba upadre ni kutokuoa au kutokuoa ni upadre.

Waulizeni tena waliowapa majibu hayo. Nitarudi tena na vifungu vya sheria mjisomee wenyewe
 
Yaani hata Askofu Kilaini anapotosha ukweli? Dah! Mimi nimesoma Seminari Likonde iliyopo Wilaya ya Mbinga jirani na Kigonsera na tumesoma na kifundishwa kwamba upadre ni moja ya sacrament ambayo haifutiki na huwezi kuwa na sacrament ya upadre na ndoa hata kama umeacha upadre. Leo anasema hivi? Ndo maana niliachana nao na kuacha kabisa kuamini dini yoyote duniani. Wanachotufundisha ni tofauti na ukweli halisi?
 
Upo sahihi mkuu, mimi mwenyewe nimepita huko......

Nikiongezea nyama kidogo kwenye "unyunyu" wako huu, ni kweli upadre ni sakramenti kama zilivyo sakramenti nyingine; Hivyo ni ishara wazi iliyowekwa na Yesu Kristu mwenyewe, isiyofutika milele,.........

Dr Slaa, hata na huyo ndugu Karugendo, hawa bado wana sakramenti ya upadre, ila hawaruhusiwi kufanya adhimisho la misa takatifu, au kutoa sakramenti yoyote. Ila kwenye hatari ya kufa, kwa ruhusa ya askofu mahalia wanaweza kutoa sakramenti hizo kwa mfano, kitubio na mpako wa wagonjwa.
Asante!
 
Yaani hata Askofu Kilaini anapotosha ukweli? Dah! Mimi nimesoma Seminari Likonde iliyopo Wilaya ya Mbinga jirani na Kigonsera na tumesoma na kifundishwa kwamba upadre ni moja ya sacrament ambayo haifutiki na huwezi kuwa na sacrament ya upadre na ndoa hata kama umeacha upadre. Leo anasema hivi? Ndo maana niliachana nao na kuacha kabisa kuamini dini yoyote duniani. Wanachotufundisha ni tofauti na ukweli halisi?

Mkuu usipotoshe

Upadre una masharti yake. Ukiutaka, unalazimika uishi masharti ya upadre.

Ukiuacha Upadre unaachana na masharti yake. Hata wanaochagua kuwa Mapadre wanajua masharti na miiko ya hiyo kazi. Lakini kwa mapenzi yao wanaichagua, wanaisomea na kuifanya. Wakishindwa kuishi maisha ya Upadre Ndio hivyo tunaona wanatoka. Ndio maisha.

Simple like that.
 
Ni kweli kabisa kuwa Upadre, kama sakramenti nyingine yeyote ile ni alama isiyofutika. Padre anapooa sakramenti haifutiki, inabaki pale pale ila ile hadhi ya Upadre, aliyopewa na Kanisa inasitishwa.

Hatupaswi kumuita Padre, japo ana alama ya Upadri isiyofutika. Haruhusiwi kutoa huduma kama Padri. Upadre upo katika kujitoa kwa huduma, hii inatokana na maagizo ya Yesu siku ya Alhamisi Kuu alipoweka Sakramenti ya Upadre. Aliwaagiza wawe wahudumu, akitoa mfano kwa kuwamegea Mkate na divai na kwa kuwaosha miguu, akiwapa mfano na kuwaagiza kuwa watumishi, wahudumu.

Kwa kifupi, anakuwa Mlei wa kawaida ambae katika mazingira fulani anaweza kutoa huduma za Kipadre, ingekuwa hiyo Sakramenti inafutika, mhusika asingeweza kutoa huduma katika hayo mazingira. Ili kuondoa mkanganyiko huu wote, ndio maana hatumuiti Padre. Maana katika uhalisia yeye sio Padre, hatoi huduma za Kipadre.

Kimsingi Upadre sio alama isiyofutika pekee, bali pia ni Sakramenti ya huduma, kujidhiri na kutumika, kwa ujumla.

Aidha, hatuwezi kumuita Padre msitaafu, maana hajastaafu.
 
Kwa kuwa sheria hizi ni zile za kufikirika za kibinadamu ndo maana hii mikanganyiko hutokea. Akitokea mmoja kutaka halalisha jambo likae atakavyo yeye wala si Mungu, haya ndo hutokea.
Nilifundishwa kuwa kuna sakramenti ambazo mtu hawezi kuzipewa mara mbili au baada ya mojawapo kupokewa. Mfano:
Huwezi kupokea sakramenti ya ndoa na ya Upadre. Niliambiwa HAIWEZEKANI. Lakini leo haya ni kawaida kabisa.
Nikaambiwa. Huwezi kubatizwa mara ya pili. Ndo maana akija Mlutheri kajiunga Katoliki, habatizwi tena kwani bado tunaamini kuwa Luther aliipokea sakrament ya milele hivyo alio wabatiza (Walibatizika) kweli.
Huwezi kuoa/kuolewa tena mwenzi wako akiwa bado hai. Lakini leo, ati Papa anakufungua uoe/uolewe tena harusi ya kukata na shoka kanisani mbele ya altare ya Bwana. Huu ni upotoshaji wa imani yetu.
Lakini, kwa vile Kristu wa wakatoliki anaenda na wakati. Sasa haya yanakubalika. Soon, tutaoa masista na vlemba vyao. Naingoja hiyo siku kwani kuna ka sista nakamezea mate. Dominos vobis cum
 
Hujui chochote kaa kimya
Mkuu usipotoshe

Upadre una masharti yake. Ukiutaka, unalazimika uishi masharti ya upadre.

Ukiuacha Upadre unaachana na masharti yake. Hata wanaochagua kuwa Mapadre wanajua masharti na miiko ya hiyo kazi. Lakini kwa mapenzi yao wanaichagua, wanaisomea na kuifanya. Wakishindwa kuishi maisha ya Upadre Ndio hivyo tunaona wanatoka. Ndio maisha.

Simple like that.
 
Hakuna cha sakramenti wala sakramento,, Askofu Kilaini yupo sahihi kabisa.

Hakuna sehemu kwenye biblia zilipoandikwa sakramenti,, sakramenti ni mapokeo tu ya kanisa. Tatizo ni kutokusoma biblia na kuishia kusoma mapokeo ya kanisa.

Someni neno la Mungu muifahamu kweli, nayo itawaweka huru kweli kweli
.

Ahsante Askofu kwa kufunguka bila kuwaficha waumini wako.
 
Kwa kuwa sheria hizi ni zile za kufikirika za kibinadamu ndo maana hii mikanganyiko hutokea. Akitokea mmoja kutaka halalisha jambo likae atakavyo yeye wala si Mungu, haya ndo hutokea.
Nilifundishwa kuwa kuna sakramenti ambazo mtu hawezi kuzipewa mara mbili au baada ya mojawapo kupokewa. Mfano:
Huwezi kupokea sakramenti ya ndoa na ya Upadre. Niliambiwa HAIWEZEKANI. Lakini leo haya ni kawaida kabisa.
Nikaambiwa. Huwezi kubatizwa mara ya pili. Ndo maana akija Mlutheri kajiunga Katoliki, habatizwi tena kwani bado tunaamini kuwa Luther aliipokea sakrament ya milele hivyo alio wabatiza (Walibatizika) kweli.
Huwezi kuoa/kuolewa tena mwenzi wako akiwa bado hai. Lakini leo, ati Papa anakufungua uoe/uolewe tena harusi ya kukata na shoka kanisani mbele ya altare ya Bwana. Huu ni upotoshaji wa imani yetu.
Lakini, kwa vile Kristu wa wakatoliki anaenda na wakati. Sasa haya yanakubalika. Soon, tutaoa masista na vlemba vyao. Naingoja hiyo siku kwani kuna ka sista nakamezea mate. Dominos vobis cum
Upo sahihi mkuu, haya mambo yanaleta shida ukitaka kuyaelewa unavyotaka. Kimsingi agizo la kutokuoa lipo Kikanisa zaidi (Kanisa la Magharibi tukiwemo na sie), kwaajili ya nidhamu.

Je, unajua kuwa kuna mapadre (wa Kanisa la Mashariki) wanaooa, na hivyo kupokea Sakramenti zote mbili, ya Upadre na Ndoa isipokuwa kwa wale wenye mipango ya kuwa Maaskofu?

Kwasababu lipo Kikanisa zaidi, ndio maana Mwenyezi Mungu kupitia Kanisa, hili jambo linawezekana. Anapooa hatendi dhambi. Na sidhani kama inapaswa kuwa mada kubwa hivi.

Ishu inakuja tunapoeneza uzushi wa mambo tusiyoyajua na kujikuta tukipotisha ukweli.
 
Kwa kuwa sheria hizi ni zile za kufikirika za kibinadamu ndo maana hii mikanganyiko hutokea. Akitokea mmoja kutaka halalisha jambo likae atakavyo yeye wala si Mungu, haya ndo hutokea.
Nilifundishwa kuwa kuna sakramenti ambazo mtu hawezi kuzipewa mara mbili au baada ya mojawapo kupokewa. Mfano:
Huwezi kupokea sakramenti ya ndoa na ya Upadre. Niliambiwa HAIWEZEKANI. Lakini leo haya ni kawaida kabisa.
Nikaambiwa. Huwezi kubatizwa mara ya pili. Ndo maana akija Mlutheri kajiunga Katoliki, habatizwi tena kwani bado tunaamini kuwa Luther aliipokea sakrament ya milele hivyo alio wabatiza (Walibatizika) kweli.
Huwezi kuoa/kuolewa tena mwenzi wako akiwa bado hai. Lakini leo, ati Papa anakufungua uoe/uolewe tena harusi ya kukata na shoka kanisani mbele ya altare ya Bwana. Huu ni upotoshaji wa imani yetu.
Lakini, kwa vile Kristu wa wakatoliki anaenda na wakati. Sasa haya yanakubalika. Soon, tutaoa masista na vlemba vyao. Naingoja hiyo siku kwani kuna ka sista nakamezea mate. Dominos vobis cum
Hahahaa! We jamaa umenikumbusha kabinti fulani hapa tunapendana ila kapo utawani mwezi wa nane katavalishwa kitambaa (endapo kataridhia). Kwa hapo watanisamehe, nitaendelea kukomaa kwa maana nakakubali sanaa!
 
Hakuna cha sakramenti wala sakramento,, Askofu Kilaini yupo sahihi kabisa.

Hakuna sehemu kwenye biblia zilipoandikwa sakramenti,, sakramenti ni mapokeo tu ya kanisa. Tatizo ni kutokusoma biblia na kuishia kusoma mapokeo ya kanisa.

Someni neno la Mungu muifahamu kweli, nayo itawaweka huru kweli kweli
.

Ahsante Askofu kwa kufunguka bila kuwaficha waumini wako.
Hongera kwa kuwaambia ukweli.
Tatizo watu wanapenda kusomewa vitabu/bible na kusimuliwa badala ya wao wenyewe kusoma ili wawe huru.
 
kuna kiapo anaapishwa hivi nitatumia kifaransa:VOUS ÈTES PRETRE A JAMAIS maana yake WE NI PADRI WA MILELE
 
Back
Top Bottom