ILAN RAMON
JF-Expert Member
- Sep 10, 2013
- 9,574
- 4,347
Baada ya Marekani kuzuia pesa za MCC kwa sababu ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya mitandao, CCM hawakukubali ukweli huo. Hawakuamini kama Marekani inaweza kufuta msaada huo kwa sababu ya uchaguzi wa Zanzibar na Cyber Law. Kwahiyo wakaanza kutafuta "vijisababu" vyao.
Wakasema "haiwezekani Marekani wafute msaada kwa sababu ya Zanzibar tu. Lazima watakua na agenda ya siri hawataki kusema.." Nikacheka sana. Yani vijana wa CCM wanaona suala la Zanzibar kama vile si kitu.. yani haiwezeni Zanzibar isababishe tukose hela.
Wao wanaona uchaguzi wa Zanzibar ni sawa na uchaguzi mdogo wa udiwani pale kwetu "Kibosho Manushi" wakasahau kwamba Zanzibar ni nchi na ilikua na kiti Umoja wa mataifa hadi mwaka 1964 kilipofutwa.
Lakini vijana wa CCM wanaipuuza Zanzibar.. Wao wanaona Zanzibar ni kitu kidogo ambacho hakiwezi kusababisha tukose "mabilioni ya Wamarekani"..
Kwa hiyo wakaanza kutafuta sababu zingine ambazo wanaamimi "zinasound" zaidi kiuliko Uchaguzi wa Zanzibar. Na hapa ndipo uzwazwa ulipoanzia.
Mmoja wa makada wa CCM Hamprey Polepole pamoja na "Accorders" wenzie wakaanza kupotosha sababu ya kunyimwa fedha hizo. Wakasema si kwa sababu ya Zanzibar wala Cyber Law ila ni kwa sababu ya Symbion (kampuni ya kuzalisha umeme ya Marekani).
Polepole amenukuliwa mara kadhaa mitandaoni na kwenye runinga akidai Marekani wametunyima pesa za MCC kwa sababu wanajua tutawanyima dili la kuzalisha umeme kwa kampuni yao ya Symbion.
Alifika mbali na kusema "Marekani wanatuonea wivu kwa kuwa Symbion haitapata ulaji wa umeme"!
Nikamuonea huruma sana kijana huyu aliyejingea imani kwa watanzania wakati wa Tume ya Warioba. Huyu ni Accorder type one.. Wale wanaosofia kwa kujipendekeza. Eti kwamba Marekani wanatuonea wivu?? Hahahaah..
Kuna "Facts" ambazo Accorders hawazijui; ngoja niwasaidie halafu tuone kama kweli Marekani wanatuonea wivu.
#Fact_number1
Mradi wa kuzalisha umeme wa Symbion ni wa dola milioni 900 ambapo kwa sasa wametekeleza kwa kiwango cha kama dola milioni 350 hivi. Hizi ni sawa na Shilingi Bilioni 800 za kitanzania (haijafika hata trilioni moja).
#Fact_number2
Pesa za MCC walizotunyima Marekani ni takribani Shilingi Trilioni 1.2 za Kitanzania.
Sasa inawezekanaje mtu akunyime Trilioni 1.2 kwa hofu kwamba utamnyima dili la Bilioni 800? Uzwazwa mkubwa sana huu. Yani unaogopa kumpa mtu viatu vya laki moja kwa sababu unahofia atakunyima kandambili za jero.?
#Fact_number3
Bajeti ya Tanzania (ambayo haijawahi kutekelezwa kwa hata 75%) ni shilingi TRLIONI 22 kwa mwaka!
#Fact_number4
Bajeti ya jimbo la California pekee ni Dola Bilioni 122.6 kwa mwaka, sawa na shilingi TRILIONI 245.2 (exchange rate ya $1 kwa TZS 2,000). Maana yake ni kwamba bajeti ya jimno la Carlifonia peke yake ni sawa na Bajeti ya Tanzania kwa miaka 11.15 (under ceteris peribus).
Sasa jiulize hapa Marekani wanatuoneaje wivu? Bado simuelewi Polepole na genge lake la Mazwazwa. Hivi dereva wa "Range Rover sport" anamuoneaje wivu dereva wa "Starlet Old model"?
#Fact_number5
Bajeti ya ujumla ya Serikali ya Marekani (US Federal Budget) kwa mwaka 2015/16 ni Dola Trilioni 3.8 ambazo ni sawa na shilingi TRILIONI 7,600 za kitanzania. Hiki kiasi ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa MIAKA 345 NA MIEZI 6.
Yani tukipewa bajeti ya Marekani kwa mwaka mmoja tu tunaitumia hadi mwaka 2361 (under ceteris peribus). Yani Yesu anaweza kurudi akatukuta tunakula tu pesa ya Mmarekani ya mwaka mmoja. Na ukumbuke kuwa bajeti ya Marekani ni asilimia 21% tu ya GDP ya nchi yao. Bado wana reserve ya mabilioni ya dola.!
Sasa hebu tusaidiane hapa Marekani wanatuoneaje wivu?
Kichwa kinaniuma sana sijui kwa nini hawa Wamarekani wanatuonea wivu kwa ajili ya ki-Symbion chao..!
Kichwa kinaniuma sana, nimemwomba Daktari aniandikie "Brufen" kabisa maana "Diclofenac" imebuma.!